Wafanyakazi na kuongezewa mishahara

Supervision

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
265
203
Hey jambo watanzania wenzangu ! Ebwana nimefuatilia habari mbalimbali na mijadala mingi mikali nimegundua kwmba raisi kuna mambo machache tu, akiyafanya malalamiko ya watumishi yatapungua na uchumi kukua kutokana na vitu vichache akivifanya na mchango wa moja kwa moja kutoka kwa watumishi hadi kuathiri jamii hasa kiuchumi:

Mambo hayo ni kama yafuatayo:

1.Kuachilia ajira zile ambazo hazieleweki zitatoka lini?

2.Kupandisha wafanyakazi madaraja na kuachia uhamisho.

3.Kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa serikali.Hili la tatu ni muhimu na linaweza kuchangia uwepo wa pesa kurudi mtaani kwasababu,'Kuna wafanyakazi wa serikali kila sehemu mjini na vijijini.

Kama kijiji kinawafanyakazi 20 ama 30 yaani hapo manesi,mabwanashamba na walimu kila mtu anapata mshahara mkononi siyo chini ya laki sita maana yake ukizidisha mara 30 unakuwa na siyo chini ya milioni kumi na tano inayozunguka hapo kijijini.

Watu hawa watachangia kuongeza mzunguko wa pesa kwa kununua bidhaa vijijini na mijini(mitaani)na hata kuanzisha vimiradi kama kujenga nyumba ama kufanya shughuli za kilimo hivyo kuongeza upatikanaji wa pesa hata kwa watu wa chini.Kwani akiweka mtu wa chini amfanyie kazi yake anakuwa anamwajiri yule mtu hivyo kufanya iwe rahisi kuajiri wengine na watu kupata pesa za kusongesha maisha.

Licha ya kuongeza ajira kwa watu na kupunguza malalamiko kwa wafanyakazi kitaifa atakuwa anakuza uchumi kwani kila mwezi mtaani au kijijini kuwa na pesa inayozunguka kuanzia milioni kumi ukiongeza na ile ya wanakijiji wa kipato cha kawaida basi maeneo hayo yatapanuka kiuchumi.

Akimaliza kufanya haya atakuwa amepunguza malalamiko na kuongeza pesa kuzunguka mtaani na hata kuongeza kodi kwa taifa.

Zaidizaidi yatabaki maswala ya kisiasa lakini kwa wananchi wengi pesa itakuwa imerudi na kuhitaji tu maswala machache kama vile kilimo,kusimamia ununuzi wa mazao ili wananchi wanufaike,ukusanyaji mzuri wa mapato na kuziba mirijanya kinyonyaji.


Da,tuache unafiki kama kazi aise,kweli tunapiga haswa !
 
Katika awamu hii chombo ambacho kinastahili kulaumiwa bunge cjaona popote ambapo bunge limemtetea mwananchi kuanzia fao la kujitoa, ongezeko la makato ya bodi ya mkopo na mishahara kwa watumishi! Kwa mtazamo huu wafanyakaz waandike wameumia!
 
Back
Top Bottom