Wafanyakazi hewa Shinyanga mpaka sasa (Aprili 19, 2016) ni 226

Qualcomm

Senior Member
Nov 27, 2013
177
138
UPDATES
Watumishi hewa katika mkoa wa Shinyanga wafikia 226 takwimu hiyo ni kwa mujibu wa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa daraja la Mwalim Nyerere.

Ikumbukwe mkoa wa Shinyanga hapo awali uliripotiwa kuwa na watumishi hewa kuwa ni 0, baada ya mheshimiwa rais kuituma tume maalumu kuchunguza wakaonekana kufikia 45, kisha 102 na sasa 226.

Pia rais John Magufuli akasisitiza kuwa serilali haitamvumilia mtu yeyote anafuja fedha za umma na watumishi wa umma na viongozi wanatakiwa kuwatumiakia wananchi wa hali ya chini.

==============================================

image.jpeg
Kile Kikosi cha Magufuli kinaendelea na operation huko Shinyanga mpaka sasa imethibitika wafanyakazi hewa wapo 102 na kazi inaendelea.

Wilaya/ Halmashauri, Wafanyakazi Hewa
1. Mkoa wa Shinyanga, Kiutawala (3)
2. Manispaa ya Shinyanga (19)
3. Wilaya ya Shinyanga (8)
4. Wilaya ya Kishapu (20)
5. Wilaya ya Kahama (46)
6. Wilaya ya Ushetu (6)

Jumla 102
 
Huyu mama alikurupuka sana alidhan ana kinga ya kibunge kuongea hata uongo unalindwa na kanuni sasa ndio katumbuliwa
 
View attachment 337005 Kile Kikosi cha Magufuli kinaendelea na operation huko Shinyanga mpaka sasa imethibitika wafanyakazi hewa wapo 102 na kazi inaendelea.

Wilaya/ Halmashauri , Wafanyakazi Hews
1. Mkoa wa Shinyanga ,Kiutawala (3)
2. Manispaa ya Shinyanga (19)
3. Wilaya ya Shinyanga (8)
4. Wilaya ya Kishapu (20)
5. Wilaya ya Kahama (46)
6. Wilaya ya Ushetu (6)

Jumla 102

Na wa IKULU nao mpaka sasa wamefikia Elfu ngapi labda?
 
Yani nikitafakari Mzee John Marecela alivyo kuwa akihangaika Na uzee ule kwenye uchaguzi kwajili ya JPM ,Na hiki kilicho mpata mke wake hakika Jamaa kadhamilia wacha waisomeee nambaaa eeeheeee
 
Mama alijua labda hewa kwa maana ya ile inayoweza kuzalisha umeme wa upepo
Labda wangemsikiliza utetezi wake..!
 
View attachment 337005 Kile Kikosi cha Magufuli kinaendelea na operation huko Shinyanga mpaka sasa imethibitika wafanyakazi hewa wapo 102 na kazi inaendelea.

Wilaya/ Halmashauri, Wafanyakazi Hewa
1. Mkoa wa Shinyanga, Kiutawala (3)
2. Manispaa ya Shinyanga (19)
3. Wilaya ya Shinyanga (8)
4. Wilaya ya Kishapu (20)
5. Wilaya ya Kahama (46)
6. Wilaya ya Ushetu (6)

Jumla 102
Huyu maza hizo takwimu zake kuwa hkn wafanyakazi hewa yeye alizitoa wapi? Huyu mama wala asimlaumu Magu wala mtu yyt kajitakia mwenyewe alijisahau akidhani Magu anatania au anachokisema hamaanishi.mlimzowea mkwere anawachekea chekea eeh! Fanya kweli Maguuu.
 
Au huyu mama hakuelewa neno "Hewa"
Shinyanga wanajua maana ya hewa, wanunuzi wa pamba ya Shirecu wanajua saana maana ya hewa. Ukiangalia ghala la pamba unaambiwa kuna kilo 100,000 kumbe ni kilo 70,000 zingine 30,000 pamba hewa. sembuse issue ya wafanya-job tena sirikalini.
 
Back
Top Bottom