Wafanyakazi hawajalipwa mishahara kwa miezi 6

Wanu

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
353
223
Msaada kwa wanasheria.

Kuna kampuni moja mdogo wangu anafanya kazi kampuni hiyo inaitwa KIMANI MINERALS ofisi zake zipo ubungo plaza gorofa ya kumi. Mmiliki wake ni mwalim wa chuo kikuu cha Dar es salaam.

Kampuni ni kubwa sana ila inaelekea kufirisika, wafanya kazi wake hawajalipwa mishahara yao toka mwaka jana mwezi wa 7 cha ajabu jamaa hataki kuwafukuza kazi na kuwapa stahiki zao.

Kuna baadhi kawaachisha kazi na kuwaahidi atawalipa baada ya miezi miwili na hajafanya hivyo na kuna baadhi wamepeleka malalamiko yao katika baraza la usuruhishi ila hadi sasa hakuna kinachoendelea.

Please wanasheria saidieni watu hawa kabla jamaa hajauza mali zake zote na kutokomea kusiko julikana.
 
Hatokimbia popote na wala mali zake haziwezi shikwa kwa sababu kampuni ikifilisika ambayo ipo registered basi mali za wakurugenzi hazishikwi wala hazihusishwi.
 
kampuni nikama binadamu asiye na viungo sawa na binadam kamili kisheria hivyo wafanyakaz wanahaki kuishtaki na kupewa madai yao...hapo kazi nikwao
 
Back
Top Bottom