Wafanyakazi hawa wafanyiwe mabadiliko

mickh5050

Member
Mar 26, 2017
19
10
Kwa wanajukwaa wote na wapenda maendeleo.

Ni mtazamo wangu tu ! Na sijui wewe utauonaje?

Kuna baadhi ya kazi ambazo mimi nafikiri zinahitaji sana watu ambao ni watendaji haswa (ambao wanapractice elimu zao) na siyo wenye vyeti vya ufaulu darasani tu ambao hawafanyi kitu chochote kuleta maendeleo;

(1)Maofisa wa mifugo(Bwana mifugo),inakuwaje mtu amepewa kazi ya afisa wa mifugo huku yeye mwenyewe hata kuku hajui kufuga?
Utakuta mtu kama huyu eti anasimamia chanjo za mifugo tu ndo kazi hiyo inayoweza kuleta maendeleo?

Ushauri wangu hapa ,Serikali ingewachukua baadhi ya wazee katika makabila ambayo ni wataalamu wa ufugaji ikawaelimisha na kuwaajili maeneo mbalimbali ya nchi yetu kuwafundisha wengine ufugaji kwa vitendo.

(2)Maofisa wa kilimo(Bwana shamba) hawa ni wengi sana na nchi yetu bado inategemea uchumi wa kilimo.Lakini cha ajabu utakuta Bwana shamba ni mlevi wa kupindukia kijijini ,hana shamba la maana waka elimu ya kilimo hatoi kwa akulima.
Kibaya zaidi hata aina za udongo na mazao ambayo yanaweza kuzalishwa kiufanusi katika maeneo wafanyayo kazi hawajui ,lakini wanalipwa mishahara kila mwezi ,Je tuendelee tu bila kufanya mabadiliko?

(3)Mabwana Afya ,hili jipu ni kubwa sana ,maeneo mengi ya miji ni machafu sana cha ajabu sijawahi kuwasikia wakifanya hata mikutano tu ya kuwaelimisha wananchi michanganuo ya taka na namna ya kuzihandle zisisababishe madhara kwa wananchi ,unasemaje hapo?

Tujadiliane hapo jamani siyo kutaka mtu afukuzwe kazi bali awajibike kwa kazi aifanyayo kuleta maendeleo Tanzania.
 
una umri gani? elimu yako ?
bora pasaka imalizike tu,hawa watoto warudi shule
 
SI BORA HAWA WANA VYETI, MBONA DAB HANA CHETI NA ANAONGOZA MAPROFESA HUWEZI KUSHANGAA..
 
naona ujielewi

mimi ni mmoja wao katika hizo chaguzi zako.

TATIZO LETU WATANZANIA TUNAPENDA SIASA MPAKA KWENYE TAALUMA.

kwenye nyama unakuta haifai kwwa matumizi lakini watu wanalazimisha itumike. chanjo tu ni shida, maana zina gharama na rahisi kuharibika.
wakipewa maelezo namna ya kufuga hawataki. wanafanya kama wazee wao walivyokuwa wanafanya

hawa wa kilimo naona ujajielewa ni kama vile mhasibu wa benki na yeye afungue benki yake. fuateni maelezo... watu wa kaskazini huwa waelewa ila kama wahaya, waha, ngoni maana nimekaa nao ni wabishi kila kitu wanajua. bora uwaache na ujuaji wao

mabwana afya.... mji kuwa mchafu kwani wanachafua wao. kuna poster na mabango ya kuhimiza KEEP YOUR CITY CLEAN. VINYWAJI VYA TAKE WAY VINAKUKUMBUSHA WEKA MJI SAFI.

Kama unachafua mji nani akufanyie usafi ni sawa unachatupa tupa uchafu ndani kwako, unakojolea vibobo nk. unadhani nani atakusafishia

MY TAKE: ELIMIKA, TUNZA MAZINGIRA, FUATA USHAURI, TANZANIA ITAKUWA SALAMA
 
Hivi hapo ulipo mleta uzi umerudi karne moja nyuma kifikra. Unahitaji ukombozi. Soma tena ulichoandika na tia tafakuri ya kina.
 
Mleta Mada Afisa mifugo ni muhimu sana kipekee kwenye kukagua Nyama kabla haijapelekwa kwa wananchi kuuzwa. Vinginevyo tungeugua magonjwa ya mifugo kama Kimeta, tegu, minyoo na rift valley diseases. Ila kwa Bwana Afya wa Dar wapelekwe tu kutibu hospitalini.
 
Back
Top Bottom