Wafanyakazi 597 wa NIDA wafutwa kazi. Waliofutwa wadai hawakulipwa mshahara kwa miezi 3

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
240
267
"NIDA chini ya malengo yake ilitarajia kuzalisha vitambulisho 24,000 kwa siku kukiwa na wafanyakazi 802 wenyemkataba wa kudumu na 597 mikataba ya muda,tumekuwa tukizalisha chini ya 10% kwa siku tuko jumla 1399 ukigawanya tu kwa sisi wote ukweli kunawengine wanabaki bila uzalishaji.haiwezeka"Alifafanua Dr.Kipilimba Mkurugezi wa NIDA

IMG_9033.jpg

IMG_9034.jpg

===============

UPDATE

Vijana waliofutwa kazi NIDA watakutana Victoria jengo la BMTL.

Wanadai kwamba wamefukuzwa kazi kabla ya mikataba yao kuisha na pia hawajalipwa mishahara kwa miezi 3, Watakuwa Makumbusho leo saa nne asubuhi, wanataka kukutana na kuongea na Waandishi wa Habari.
 
"NIDA chini ya malengo yake ilitarajia kuzalisha vitambulisho 24,000 kwa siku kukiwa na wafanyakazi 802 wenyemkataba wa kudumu na 597 mikataba ya muda,tumekuwa tukizalisha chini ya 10% kwa siku tuko jumla 1399 ukigawanya tu kwa sisi wote ukweli kunawengine wanabaki bila uzalishaji.haiwezeka"Alifafanua Dr.Kipilimba Mkurugezi wa NIDA
Fafanua habari hii ili ikamilike na kutuhabarisha kwa kina bila ya kuacha mwanya ...
 
Ukisikia kuisoma namba ndo hii sasa... hapo hujamalizia mkopo, na mkeo anamimba ya mapacha, mshahara ulienda kununua passo ambayo bado hujaitoa bandarini!!!

Lazima akiri ikurudi, utatamani Lowassa angepita bila kupingwa lol!!!

Tangu nianze kusikia NIDA wapo kwenye mchakato wa kuandikisha vitambulisho vya TAIFA siyo chini ya miaka 4 na hakuna kilichofanyika sasa hao watumishi 500+ walikuwa wanalipwa kwa kazi zipi hasa kama siyo matumizi mabaya ya fedha?

Asante Dr Magu
 
Ukisikia kuisoma namba ndo hii sasa... hapo hujamalizia mkopo, na mkeo anamimba ya mapacha, mshahara ulienda kununua passo ambayo bado hujaitoa bandarini!!!

Lazima akiri ikurudi, utatamani Lowassa angepita bila kupingwa lol!!!

Hahahaa mkuu hatariii,na bandarini hakuna tena njia za magumashi kutoa gari, bado masela waliomchangia harusi wanakaribia kuoa urudishe fadhila. Mdogo wake alipata div zero inabidi aende private school. Ebana eeeh namba inasomwa si mchezo.
 
Ukisikia kuisoma namba ndo hii sasa... hapo hujamalizia mkopo, na mkeo anamimba ya mapacha, mshahara ulienda kununua passo ambayo bado hujaitoa bandarini!!!

Lazima akiri ikurudi, utatamani Lowassa angepita bila kupingwa lol!!!
Ndugu, ebu fikiria kidogo usiwe mvivu hivyo, angalia idadi yao ya mwanzo na projection ilikuwa nini na wamezalisha nini mpaka sasa na wametimiza kiasi gani malengo ya mwanzo mpaka sasa na kwa muda gani wamekuwapo? Jaribu kujiuliza maswali ya msingi kwanza kabla ya kukurupuka.
 
Back
Top Bottom