Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani awatoa hofu wafanyakazi 597 wa NIDA

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
238.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo katika Jengo la BMTL, jijini Dar es Salaam, jana. Katika hotuba yake, Rwegasira aliwataka watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao waondoe hofu kwani hivi karibuni Serikali itaanza kuwalipa fedha zao baada ya taratibu chache za kiutendaji kukamilika.



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.

Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.

Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo kabla ya kuanza kuwalipa.

“Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.

Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.

Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

“Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk. Kipilimba

Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.
 
Kama wapo walioichagua ccm hayo ndo malipo yao acha waisome namba
 
Kama wapo walioichagua ccm hayo ndo malipo yao acha waisome namba
Hawawezi kukosa si unajua kazi zilikuwa za mjuano hazikutangazwa mahali?
Na wazazi wao ndio waliokuwa kwenye system na wakawachomeka.
Ni CCM hao inawezekana na kale kawimbo walikaimba bila ya kujua maana yake
 
Kwanza kapilimba ameshawakomoa ameenda kuwachongea tra kama wakatwe kodi ktk hiyo mishahara yao wanayodai ya miezi 3 na pia akaenda bodi ya mikopo wakate hela zao kwa wale wanufaika wa mikopo lengo lake ni kuwakomoa hao vijana wasipate chochote
HATIMA YA KISASI CHAKE
Kwenye body ya mikopo wamempuuza.
Ila tra wenyewe wamekomalia wanataka chao hivyo kama wizara isipoingilia vijana hawatapata kitu

HASARA ATAKAYO ISABABISHIA NIDA
Tra wamekoma wanataka kodi sio tu ya miezi mitatu aliyowachongea Bali wanataka toka walipoajiriwa na kosa halipo kwa hao vijana Bali mamkaka ndio walikuwa hawakati na hata kwenye mikataba yao hawakuainisha kwamba watakatwa kodi zaidi ya mfuko wa jamii tu.
Hivyo mamlaka itapaswa kulipa hizo kodi zote

Pia imegundulika kuwa kuna wafanyakazi wengi zaidi ya 600 ambao walioajiriwa hivi karibuni hawana zaidi ya miezi 6 nao walikuwa vibarua kama hawa waliosimamishwa tena wengi wao wamefanya vibarua zaidi ya miaka 4 na wao walikuwa hawakatwi kodi hivyo tra nao wanakomalia kodi zao wote toka wameanza vibarua mpaka wameajiriwa
Na ni mamlaka ndio inawajibika kulipa kwani hao vibarua hawakuwa na makosa
So kapilimba aliicheza ngoma bila ya kuangalia mwisho wake
 
Mkuu namba lazima waisome na sasa hivi si unajua fao la kujitoa kwenye mfuko wa jamii lemetolewa
Ewaaaa yaan ndo maendeleo yenyewe hayo ha ha ha ha makusanyo ya kodi yameongezeka sukari musoma kilo Tsh 4300 naniliii mbele kwa mbeleeeee
 
Back
Top Bottom