Wafanyakazi 597 wa NIDA walioachishwa kazi kuanza kulipwa kesho

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini (Nida) imesema itaanza kufanya malipo ya madai ya wafanyakazi wake 597 waliokatishwa mkataba na mamlaka hiyo hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Modestus Kipilimba, ilisema malipo hayo yataanza kulipwa leo asubuhi kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katika jengo la BMTL.

Malipo hayo yatafanywa kwa mgawanyo. Mgawanyo wa kwanza utakuwa na kundi la kwanza, pili na tatu, ambao watalipwa kesho na mgawanyo wa pili, utakuwa na kundi la nne na tano ambao watalipwa keshokutwa.

Mgawanyo wa tatu utakuwa na kundi la sita litakalo lipwa Alhamisi, mgawanyo wa nne utahusisha kundi la 7 na 8 litakalolipwa Aprili 16 na kundi la tano litajumuisha madereva na kada nyingine, litalipwa Aprili 17.

Aidha, taarifa hiyo iliwataka wadai hao kufika kwa wakati sambamba na kuwa na vielelezo na nakala halisi za mikataba yao ya kazi.

Awali, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao walioandamana baada ya tangazo la kufutwa kazi kuwa malipo yanayotarajiwa kutolewa na Nida hayasadifu uhalisia wa kile wanachokidai.
 
Kipilimba hizo hela ametoa wapi au ni lile salio la Infospy...Huyu mkurugenzi atatumbuliwa soon
 
Wa mikoani tunasubiri vitambulisho hatutaki sanaa za huyu mkurugenzi, toka amechaguliwa yeye ni media tu kila kukicha,,, kwa maoni yngu rais huyu bwana hii nafasi haiwezi mtoe mteue mwingine ambaye ataendana na kasi yako ya hapa kazi tu,,
 
Back
Top Bottom