Wafanyakazi 16 wa manispaa ya Morogoro 'wasalenda vizimba' wamo viongozi wa zamani wa soko waliohodhi zaidi ya kimoja ni kufuatia agizo la Magufuli

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,987
9,815
Watumishi 16 wa halmashauri ya Manispaa waliokuwa wanamiliki vizimba kwenye soko kuu jipya la Chifu Kingalu la Morogoro ( zamani soko kuu jipya la Morogoro) na kuwakodishi wafanyabishara wadogo kwa Sh 50,000 kwa mwezi badala ya sh 20,000 kiwango kilichowekwa na Manispaa hiyo wamevirejesha (kusalenda) na fedha walizochukua baada ya agizo la Rais John Magufuli.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli, ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, watendaji wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Meya na Mkurugenzi kuanzia Februari 13, mwaka huu alianza kufanyia kazi maagizo hayo kwa kuendesha zoezi kuhakiki vizimba vyote 900 na kubainika watumishi 16 wa Manispaa wamejimilikisha na kupangisha kwa wafanyanishara wadogo kwa bei ya juu.

Mkuu wa wilaya alisema baada ya Rais kuondoka walifanya mambo ya kuhakikisha aliyepewa agizo la kutapika fedha ( Aika ) amefanya hivyo na amefanya hivyo haraka iwezekanavyo na bahati nzuri alikiri kwa maandishi na kwa sababu Rais alimwabia au achague kazi au atoe kutoa hizo fedha na amezitoa fedha hizo.

Mkuu wa wilaya, alisema walikaa na watumishi wa Manispaa hiyo na kuwaambia ama wachague kuendelea na ajira au kufuatilia masuala ya vizimba.

“ Napenda kuwaambieni katika kipindi cha saa tatu tumepata orodha ya wafanyakazi wa Mansipaa 16 ambao wenyewe wameandika majina yao na kusema wazi kabisa kuwa sisi ulikuwa na vizimba hivi na sasa tunavitoa na wapo wengine wachache walipata kuwa na vioksi na wengine maeneo mengine ya kibiashara lakini kwa ujumla wao wapo 16” alisema Msulwa.

Mkuu wa wilaya, alisema ; “ Na ninavyozungumza sasa hivi kuna nafasi 16 ambazo tutazigawa kwa wafanyabiashara wanaostahiki” alisema Msulwa.

Hata hivyo alisema , wamebadirisha kabisa uongozi wa soko kuu jipya hilo kwani kulikuwa na makundi mengi , kulikuwa makundi zaidi ya saba na hilo limeleta matatizo makubwa na kila mtu alikuwa akilalamika kwa upande wake na hakukuwa na uratibu wa pamoja wa uendeshaji wa soko hilo.

“ Tulichokubaliana na kumefanyika kuanzia Februari 13 mwaka huu maeneo yote haya ya biashara na wafanyabiashara wote kila mahali yamechagua viongozi wao na viongozi wao wakaunda kamati ya uendeshaji wa soko na kuchanguliwa mwenyekiti mmoja na katibu mmoja wa soko “ alisema

Mkuu wa wilaya alisema ; “ ninachoweza kusema tunachofanya ni uhakiki wa moja kwa moja na tumeanza na kundi la waasisi ambao ni wale waliokuwa wafanyabiashara kabla ya kufunjwa na na baada ya kuvunjwa …tumechukua orodha ya mwaka 2013 tunahakiki mfanyabiashara mmoja baada ya mwingine na katika muda mfupi na hatua inayofuata ni kwa wafanyabiashara waliokuwa soko la Manzese na kubalizia timu ya wafanyabiashara wapya” alisisitiza Msulwa.

Alisema katika kipindi cha siku mbili wamepata mafanikio makubwa na kumshukuru Rais kwa kuwezeasha kuwapa msukumo kwa kufanya kazi hiyo kwa kasi kubwa na ndani ya kipindi cha wiki moja kutakuwa na utulivu mkubwa katika soko hilo.

Mkuu wa wilaya alisema, pia bado kuna vioksi 70 hadi sasa havina watu, hivyo aliwaomba wananchi na wafanyabiashara kuisaidia serikali kuona kama kuna mianya ya rushwa kwenye mchakato huo wa vioski na kwamba timu yake ipo kazini kuanzia asubuhi hadi usiku kuona changamoto zote katika soko hilo zinapatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo alisema ,katika uhakiki huo umebaini wapo baadhi ya viongozi wa zamani wa soko wamechukua visimba vingi na wameambiwa wavirejeshe na tayari wameviachia na baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kutakuwa na vizimba vingi ambavyo vitagawiwa wafanyabiashara wadogo wengine kwa njia ya uwazi .

Naye Mwenyekiti wa soko la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele aliyechaguliwa juzi baada ya kuvunjwa wa uongozi wa zamani wa soko, alimshukuru Rais Magufuli, kwa mchango mkubwa waliowaachia naMorogoro na ukumbusho mkubwa na pia kulifungua soko hilo na kuona hali halisi ya wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa soko jipya hilo kwa niaba ya wafanyabiashara pia alimshukuru Rais kwa kuwaondolea ushuru waliokuwa wakitozwa na Manispaa wanapoingiza bidhaa zao ndani ya soko hilo na kuanzia siku hiyo wawatozwi tena ushuru hukua kiomba kupunguziwa gharama za vioksi.
 
Hapo ni vizimba tu bado ardhi na vitu vingine kilichokua kinatakiwa ni kuwa na taasisi itakayosimamia hayo mambo sio kauli ya Rais huko kwingine ambako hajatoa kauli watu bado wanaendelea kuhodhi hivyo vizimba na ardhi na upigaji mwingine unaendelea kama kawaida.
 
🦍 kasema, nyie 🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐵🐵🐵🐵🐵🐵🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒🐒 ni kutii tu
 
Kama changamoto za solo tu, zilikuwa juu ya uwezo wa RC, DC MKURUGENZI, RAS NA DAS, mpaka Rais aseme ndo yafanyiwe kazi basi changamoto ni kubwa kuliko tunavyoweza kudhani.
 
Kwa mtindo huu Rais ana kazi kubwa sana ya kufanya. Maana hata mambo madogo mpaka afike yeye ndio yatatuliwe.
 
Mkuu wa wilaya alisema baada ya Rais kuondoka walifanya mambo ya kuhakikisha aliyepewa agizo la kutapika fedha ( Aika ) amefanya hivyo na amefanya hivyo haraka iwezekanavyo na bahati nzuri alikiri kwa maandishi na kwa sababu Rais alimwabia au achague kazi au atoe kutoa hizo fedha na amezitoa fedha hizo...
Wewe DC kichwa mbovu kabisa, ina maana hukuliona hilp tatizo kabla Rais hajaja?

Je ni hao watumishi wa Manispaa peke yao ndiyo walifanya huo mchezo mbovu, hakuna viongozi wa juu kule ofisi ya Mkoa na Wilaya ambao wanamiliki vizimba kwa kutumia nafasi zao? au tuwataje?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom