wafanyaji fujo ni kina nani Zanzibar?

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,182
6,214
Mimi nimekaa nimefuarioia kwa umakini fujo zinazoendelea Zanzibar. Ikiwa mimi kama mzanzibari nimesikitishwa na vitendo wanavofanya wazanzibari wenzangu. Mambo mengine lazima tukae tufikiri vyema matunda yake yatakuaje?

Wafanyaji fujo katika visiwa vya zanzibar sio UAMSHO bali ni vijana ambao wanatumia fursa hiyo. UAMSHO hufanya maandamano ya amani siku zote lakini kuna hawa vijana ambao hawaridhiki kama hawajachokoza mapolisi na hapo ndiopo wanapochanganywa wote. Kuna kikundi kinaitwa UBAYA UBAYA, kikundi ni cha wahuni watupu, ambao hugamia mtaa na kuharibu haribu na kutisha watu, serikali iliombwa itumie vikosi kama KMKM,Jku,FFU kuwadhibiti watu hawa lakini ikasema kuwa haiwezi kutumia vikosi ivo maana vikosi ivo vikiingia mtaani havichagui vinapiga yoyote tu, kwaiyo watapeleka askari wa kawaida, sasa askari mwenye kirungu atamsogelea mwenye panga? Serikali inalea hichi kikundi ambacho baadae ndio kitakuja kuwa kikubwa. Kikundi hichi ndicho kilichochoma moto maskani ya kisonge na vurugu nyengi wao walikua wahusika jana.

Vile vile mi naona kuna watu wanajifanya waislam lakini sio lolote, kama mwendeshaji ukurasa wa UAMSHO katika FB, ameandika kitu kimeniuma na sikusita kumpa jibu apo apo, anahimiza kuwa watachinjachinja, na anajisifia eti mfano umetolewa bububu, nilimuona kama mhuni flani asiejua dini kabisa. Yule aliemuua askari huyo atafute la kumjibu siku ya kiama, mana hukumu ya muuaji na yeye auliwe, sasa je Koplo Said ameua? Nataka nijibiwe na wazanzibari wenzangu wanaosapoti mauaji yake. Mtume hakuhubiro chuki dhidi ya wasi waislam, mtume aliongoza taifa ambalo ndani yake kulikua na manasara na mayahudi, hakuwahi kuwachomea moto nyumba zao za ibada hata pale wanapokorofisha wala hakuwafukuza katika ardhi ya waislam, tukinganishe na matendo yetu leo, mtume alikua na subra, na subra katika uislam ni kitu muhimu sana ukikosa icho ndugu yangu huji kupata jema.

Ukichungua fujo zinazofanywa zanzibar utajua hasa kama wafanyaji fujo ni wahuni, wenzangu wa zanzibar mnawajua watu wa MBORIBORINI, haya hawa ndo uamsho? Ukipita mtaa wao na vespa unarudi nyumban kwa miguu, kisha eti tunawakuta katika maandamano ya UAMSHO.

SMZ isipowashughulikia hawa jamaa kwa kutumia risasi za moto, hichi kisowa kitaharibika sana tu, kitakuwa na wahuni tele, wewe watu wanambaka mwanamke njiani mchana tena hadhara wanamfanyia nyuma na mbele, kisha unasema wasipelekewe vikosi au wasitumiliwe risasi za moto? Ebo ujinga huo

Inapoelekea zanzibar ni kule kama CONGO, kama hatujaishinikiza serikali ku deal na hawa wahuni wa mboriborini na UBAYA UBAYA tutashuhudia vita vya raia dhidi ya hawa jamaa, na uku dhidi ya serikali matokeo yake machafuko makubwa na mmarekani kupata fursa ya mutia mirija katika hayo mafuta tunayoringia!
 
"wewe watu
wanambaka mwanamke njiani mchana tena
hadhara wanamfanyia nyuma na mbele, kisha
unasema wasipelekewe vikosi au wasitumiliwe risasi za moto? Ebo ujinga huo"


Lahaula laqwati
 
Serikali hii yetu mpk ikulu ya Shein pale migombani itiwe moto ndo labda wanaweza kushtuka!!

Ni huzuni kukalia kimya unyama huu
 
si huko kwenu tu! hata huku kwetu bara radio iman ipo tu, wanaikenulia meno! siku ITAKAPOTANGAZA JIHAD LIVE! tuanze kuchinjana, ndio RAIS ATASTUKA! yaani ni madudu tu yanayoendelea!
 
Back
Top Bottom