Mkuu juzi nilikuwa nikitizama video moja ya business forums iliyofanyika Dubai ambapo ilikuwa na makamu wa rais wa Ghana na upande wa pili ilikuwa Mo. Sasa sijui kwanini serikali haikuwa na mtu wa kuiwakilisha?Ghana iliwakilishwa na makamu wa rais, sisi Mo mwenyewe sidhani kama hata alikuwa akiwakilisha nchi, kwa maana ya kwamba pengine serikali haikuwa na taarifa za tukio hilo?! Anyways, kuna saa nilisikia akisema kuwa "Mimi nashindana na China", as if yeye alikuwa taifa. Nadhani pengine labda ni lugha tu, pengine alitakiwa kusema kuwa anashindana na wafanyabiashara wa China nk. Pia kwenye mjadala ule,walikuwa wakizungumzia kuhusiana na sera za viwanda Africa, na ni mambo gani yanakwamisha. Nakumbuka vyema tu alitaja kuhusiana na "utawala wa sheria" kuwa ni jambo muhimu sana kwenye uwekezaji pahala popote na this time Africa. It was very interesting, ndiyo maana nikaamini kuwa serikali ilikuwa ikimfuatilia kw akaribu sana na kuna mengi ambayo hatuyafahamu. Pengine waliona kuwa hatoi ushirikiano kama walivyokuwa wakitaka.
Wao wanaamini kuwa serikali ndiyo ilimtajirisha, na kwahiyo, wanaamini kuwa anatakiwa atoe ushirikiano bila shurti. Maana kuna wakati serikali ilikuwa ikimtaka aendane na sera za viwanda. Na kuna wakati alisema wengine watafungua, akatoa mfano wa Dangote nk.