Wafanyabiashara wa nyama machinjio ya Babati wabeba nyama kichwani

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Wafanyabiashara wa nyama machinjio ya babati wabeba nyama kichwani

baadhi ya wakazi wa mji wa Babati walioshuhudia ubebaji huo wa nyama wameeleza kutoridhishwa na hali hiyo huku wakiitaka halmashauri hiyo kusitisha biashara hiyo kwa muda kupisha ukarabati wa barabara hiyo ili kuepusha madhara ya afya kwa walaji na kuepusha milipuko ya magonjwa hasa wakirejea wa kipindupindu ulioanza januari 26 na kusababisha kulazwa kwa wagonjwa 47 katika hospitali ya Mrara ya halmashauri ya mji huo.

Nae kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo Bi Rena Urio ambaye pia ni mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi amekiri kutokea kwa hali hiyo huku akidai halmashauri inakabiliwa na miundo mbinu ya barabara kadha wa kadha za mji huo zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha na imeshafanya tathimi ya matengenezo ya barabara hiyo.


12733455_918983134866029_5413152403497583127_n.png


12743577_918983144866028_3372738095543250932_n.png


12745812_918983138199362_2743088410400231132_n.png


Na ITV
 
Back
Top Bottom