Wafanyabiashara wa mafuta waikosesha TRA mapato | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyabiashara wa mafuta waikosesha TRA mapato

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,135
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Wafanyabiashara wa mafuta waikosesha TRA mapato
  Na Lulu George
  27th November 2009B-pepeChapaMaoni
  Mamlaka ya Mapato (TRA).
  Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi kwa kipindi cha miezi minne kutokana na waingizaji wa mafuta nchini kuacha kutumia Bandari ya Tanga.

  Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Nyonge Juma Mahanyu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Wiki ya mlipa kodi iliyoanza Novemba 23 hadi 26, mwaka huu.

  Mahanyu, alisema katika kipindi hicho cha kuanzia Julai hadi Oktoba, mwaka huu ilikusanya kiasi cha Sh bilioni 27 badala ya lengo walilojiwekea la kupata Sh bilioni 30.3.

  Alisema katika kipindi hicho mwaka jana ilikusanya kiasi cha Sh bilioni 30.7 badala ya Sh bilioni 35.5.

  Mahanyu hakuelezea sababu za wafanyabiashara hao kuacha kupitisha mafuta yao kwenye bandari hiyo na kusisitiza kuwa TRA haina mamlaka ya kumlazimisha au kumchagulia mtu bandari ya kupitisha mzigo wake.

  Nayo TRA Mkoa wa Morogoro, imeweka mikakati ya kukusanya zaidi ya Sh bilion 23.6 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/10 .

  Kaimu Meneja wake, Kilomba Kanse aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu ya kodi kwa walipakodi, kuwatembelea sehemu zao za biashara.

  Alizitaja changamoto zinazijitokeza katika utendaji wao wa kazi kuwa ni wafanyabiashara wengi kushindwa kutofautisha kodi ya mapato na ushuru kutokana na uelewa mdogo wa sheria za kodi.

  Nyingine ni wafanyabiashara kutotoa stakabadhi kwa wanunuzi ambao nao wamekuwa wakishindwa kuwadai na kuikosesha Serikali mapato kutokana na wafanyabiashara hao kukwepa kulipa kodi.

  Vilevile, alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiwakimbia maofisa wa TRA kwa kufunga maduka yao wanapokwenda kufuatilia ulipaji kodi.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,135
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Hamkujua wanatafuta "profit" na sio kupitisha wapi nendeni wanapopitishia mjiulizie wapi mmekosea kufanya wanapitishia huko...acheni tamaa punguzeni kodi zenu chafu
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0


  Penye bold ndipo penye mzizi wote wa fitna.Inaelekea unholy alliance kati ya TRA officials na wauza mafuta imekufa? Mbona inajulikana kabisa kuwa maafisa TRA wengi wametajirika kutokana na ubia huu usio rasmi wala halali?
  Vita dhidi ya rushwa itazidi kuwa ngumu sana kwa vile pale mtoaji anapokataa kutoa, basi ndio kuamndamwa kama anavyojaribu kuelezea huyu bwana Mahanyu!
  Hiyo Elimu ya kodi itasaidia nini kama wenyewe TRA ndio kero kubwa inayofanya walipa kodi kukimbia kulipa?Ndugu yangu mmoja alijituma kwenda TRA kulipa kodi, ajabu na kweli wakawa wanamzungusha na kumwambia aende asubiri hadi watakapomfuata! Hii maana yake ni kuwa kwa kwenda moja kwa moja TRA kulipia, watakosa kitu kidogo... ndio maana wakawa wanamzungushazungusha... sasa elimu ya nini wakati wenyewe hawataki mtu mwenye kujituma kulipia?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tanga TRA ni kichefuchefu. Wanapenda ku inflate kodi ili wapewe rushwa na wanahangaisha sana watu. Nani anayependa ghasia siku hizi?
   
Loading...