bakundande jr
JF-Expert Member
- Oct 22, 2021
- 507
- 670
Moja kwa moja kwenye mada.
Kutokana na sababu tofauti kumekuwa na panda shuka ya bei ya bidhaa tofauti kuanzia vinywaji hata vyakula.
Kitu cha kushangaza ni kuwa wafanyabiashara wanakuwa wepesi kubadilisha bei ya bidhaa pale wanaposikia bidhaa hiyo imepanda bei hata kama ndio ametoka kununua bidhaa hiyo kwa bei chee jana yake ila imekuwa tofauti pale ambapo bidhaa hushuka bei.
Kwa mfano upande wa vinywaji hususani soda imepita kama wiki naona matangazo na mabango ya kampuni flani kushusha bei ya vinywaji vyake ila kila nikienda kununua bidhaa hizo nakuta bei ni ile ile. Kitu cha kushangaza zaidi ni kuwa kwenye duka hilo hilo unaweza kuta bango ambalo lina onesha kushuka kwa bei ya bidhaa husika.
Sasa kama bado mnakuwa na mzigo mkubwa kwanini msikatae kuweka hayo matangazo?