Updates vip mliopo k/koo leo maduka yamefunguliwa?
Sahii ni saa tano na dkk 5 hakuna duka hata moja liko wazi.. yaliyowazi ni yqnayouza nyanya na vitunguu.. balaaaaaaaaa nimekuja kununua vitu muhimu kwa leo lkn ndio hivyo tena.
Updates vip mliopo k/koo leo maduka yamefunguliwa?
Unajua wanapokesea TRA ni hapa;
Mfano wewe umekopa bank mil.20 ukaenda kununua mzigo wa kuuza, labda ndani ya mwezi mzigo umeisha mara 2 so umenunua mzigo mara 2, kwenye mauzo hii EFD itakuwa imetuma taarifa ya mauzo yote ya mwezi (20 mil x 2) wakati hapa unatarajia kurudisha mkopo wa bank na riba, ulipie kodi ya frem na umeme, ulipe wafanyakazi na bado wewe ubaki na faida. Sasa kwa sababu kila ninapoandika electronic receipt inatumwa wirelessly TRA (18% ya kila unachouza na kutoa risiti), wao wakija mwisho wa mwezi watasema nina mauzo ya mil 40 kitu ambacho sio sawa maana tunatakiwa tulipe kodi kutokana na faida mtu anayopata na siyo kutokana na mauzo, so hapa mtu alitakiwa ile faida ndo ipigiwe 18% ya TRA na sio huu utaratibu wa kila item kukatwa 18%
So leo hakuna mapato yoyote yaliyoingia TRA toka kwa wafanyabiashara wa Kariakoo maana mashine za wale walio nazo si wamefunga hawajauza? Wajipange.
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
mkuu inaonekana hujui system ya VAT inavofanya kazi....VAT is charged on taxable supplies na sio kweny net profit....tatizo nililiona hapo labda ni bei ya hizo mashine