Wafanya biashara k.koo wagomea mashine za EFD

Wafanya biashara k.koo wagomea mashine za EFD

Mkuu inasemekana wafanyabiashara wamefunga maduka kariakoo kugomea mashine za TRA sasa nadhani hizo fujo itakua labda kuna wasaliti waliotaka kufungua ndo wanachezea kichapo.
 
Ilianza Mbeya,Morogoro na sasa Dar baada ya hapo sijuwi wapi itafuatia???

Aaaaaaahhhh hivi wakuu CHADEMA hawahusiki hapo eti MaCCM?
 
Hakuna vurugu bwana ila wengi wamegoma kufungua maduka

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
wafanya biashara wote k.koo asubuhi ya leo wamegoma kufungua maduka yao kwa madai ya bei juu ya mashine za EFD
source mimi mwenyewe nipo eneo la tukio
Hii nchi watu wanataka kumnyonya mlala hoi kila siku iendayo kwa mungu,kwanza wanashangaza zaidi wanapomlazimisha kila mfanya biashara mwenye mauzo ya kuanzia shs 45,000 kwa siku kununua hicho kifaa lakini hawajali mtu huyu anapata faida shs ngapi kutoka katika mauzo hayo, halafu ana mtaji kiasi gani kwao siyo issue kabisa na atapata wapi pesa ili ununue hicho kifaa wao siyo issue kwao ikibidi hata mtaji wa mtu upungue au uishe kabisa wao hawajali wanachotaka ni wewe kununua kifaa hicho kwa laki nane ili mradi wauze hayo mavifaa yao.Vifaa hivyo mbaya zaidi siyo imara na maintenance coast once kikiharibika ni tshs 50000/=ambayo ni gharama ya mfanya biashara,huu ni unyonyaji wa kutisha.

Nawashauri TRA wanunue hizo device na wazigawe kwa wafanya biashara kwa sababu wao ndiyo wanaotaka kurahisisha ukusanyaji wa mapato, kwa nini wambebeshe mfanya biashara mzigo huo? halafu waseme watakatana kupitia mapato atakayokuwa analipa mfanyabiashara, hii ni haki kweli? kwa makubaliano yapi?Mbaya zaidi watanzania wengi hata umuhimu wa kulipa kodi hatuuoni kabisa kufuatia kwamba huduma za jamii hakuna na kama zipo ni mbovu kabisa, sijui hayo mahela wanayo kusanya kila siku wanayapeleka wapi.
Nawashauri TRA waongee na serikali waboreshe huduma za jamii hali hiyo itamfanya kila mfanya biashara kulipa kodi bila shuruti kwa sababu faida atakuwa anaiona.Halafu wazingatie faida anayopata mfanya biashara na siyo mauzo ili kuamua ni nani atumie hiyo device na nani asitumie. Halafu wazingatie na kiasi cha mtaji alichonacho mfanyabiashara maana mwingine mtaji tu ndiyo hiyo hiyo laki nane na mbaya zaidi kakopa si wanataka kuchanganya watu? Gaweni hizo device bure ili msilete usumbufu na kuharibia watu biashara.
 
TRA wabadilike haraka na mashine zao
mambo haya yameanza Mbeya,Moro,
sasa Dar mwisho nchi nzima



Halafu tatizo lao ni porojo tu wakati
wafanyabiashara wamegundua kuwa
bei hii ya laki nane sio sahihi kabisa

Maana Kenya laki mbili,Dubai ndiyo
kama unakwenda kununua Toy.

''mashine zina tatizo gani?wanatakiwa wapate wafanya biashara wa aina gani?''
''laki 2 ya kenya?hebu nielimishe ili tupinge vizuri.''
 
Mtaji 500,000,mashine >800,000,Aisee MUNGU hebu shusha gharika tufe maana tumechoka na uonevu!
 
wafanyabiashara nchi nzima wagome kama madereva wa malori. Zikifika siku mbili kuna hao TRA watakusanya kodi toka ma.ka.li.o.ni kwao.
 
Vijana wenyewe wako wapi? Watoto laini akili ndogo wanawaza kupakatwa wanunuliwe magari.
TRA kuna watu ambao wako ki rushwa zaidi. hawawezi kubuni mbinu mpya za kuongeza mapato. waachie ngazi damu changa ije na new ideas. makampuni ya simu yanakua na mkurugenzi mmpya every three four years wanaoleta new ideas mpaka bei ya kutwanga simu zimepungua sana. TRA the same old dogs miaka nenda miaka rudi. wanataka wafie ofcn bila hata kufaidi rushwa iliyolimbikizwa uswiss
 
mkuu tunatakiwa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa. mbona waajiriwa wanakatwa kodi hawalalamiki
 
Unajua wanapokesea TRA ni hapa;

Mfano wewe umekopa bank mil.20 ukaenda kununua mzigo wa kuuza, labda ndani ya mwezi mzigo umeisha mara 2 so umenunua mzigo mara 2, kwenye mauzo hii EFD itakuwa imetuma taarifa ya mauzo yote ya mwezi (20 mil x 2) wakati hapa unatarajia kurudisha mkopo wa bank na riba, ulipie kodi ya frem na umeme, ulipe wafanyakazi na bado wewe ubaki na faida. Sasa kwa sababu kila ninapoandika electronic receipt inatumwa wirelessly TRA (18% ya kila unachouza na kutoa risiti), wao wakija mwisho wa mwezi watasema nina mauzo ya mil 40 kitu ambacho sio sawa maana tunatakiwa tulipe kodi kutokana na faida mtu anayopata na siyo kutokana na mauzo, so hapa mtu alitakiwa ile faida ndo ipigiwe 18% ya TRA na sio huu utaratibu wa kila item kukatwa 18%

So leo hakuna mapato yoyote yaliyoingia TRA toka kwa wafanyabiashara wa Kariakoo maana mashine za wale walio nazo si wamefunga hawajauza? Wajipange.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Tatizo hapa c kutotaka
kulipa kodi, tatizo ni bei ya hizo mashine na inakuwaje muuzaji awe ni
yule tu aliyeamuliwa na tra? Na kuwa kila mwenye mauzo ghafi yanayofikia
tsh.45,000 kwa cku lazima awe na mashine hata mwenye genge, mama lishe ,
muuza mkaa anatakiwa awe nayo, na kuna wengine kama ni bar sehemu ya
bia iwe na mashine yake,jikoni hivyo hivyo! Na tatizo kubwa kuliko yote
ni kutoona manufaa ya hizo kodi wanazolipa zinakwenda wapi? Kila cku
mala bilioni 50 zimeliwa, akienda hospital hata panadol hamna!

Kweli mkuu walakini wa kulipa kodi lazima uwepo maana manufaa kwetu ni hamna kabisa
 
mgomo bado unaendelea kupamba mitaa ya k.koo wanadai ni mgomo mpaka kieleweke
 
Kina Diamond wanalipa Kodi?wachezaji wa vilabu vya simba na Yanga je nao wanalipa
 
Updates vip mliopo k/koo leo maduka yamefunguliwa?
 
Unajua wanapokesea TRA ni hapa;

Mfano wewe umekopa bank mil.20 ukaenda kununua mzigo wa kuuza, labda ndani ya mwezi mzigo umeisha mara 2 so umenunua mzigo mara 2, kwenye mauzo hii EFD itakuwa imetuma taarifa ya mauzo yote ya mwezi (20 mil x 2) wakati hapa unatarajia kurudisha mkopo wa bank na riba, ulipie kodi ya frem na umeme, ulipe wafanyakazi na bado wewe ubaki na faida. Sasa kwa sababu kila ninapoandika electronic receipt inatumwa wirelessly TRA (18% ya kila unachouza na kutoa risiti), wao wakija mwisho wa mwezi watasema nina mauzo ya mil 40 kitu ambacho sio sawa maana tunatakiwa tulipe kodi kutokana na faida mtu anayopata na siyo kutokana na mauzo, so hapa mtu alitakiwa ile faida ndo ipigiwe 18% ya TRA na sio huu utaratibu wa kila item kukatwa 18%

So leo hakuna mapato yoyote yaliyoingia TRA toka kwa wafanyabiashara wa Kariakoo maana mashine za wale walio nazo si wamefunga hawajauza? Wajipange.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Hivi mbona tunapenda kumung'unya maneno?
1 Ukweli hii kodi hulipwa na sisi wateja na wafanyabiashara wanakuwa kama maajent wa TRA
2. Mashine hizi huweza kukopeshwa kwa wale ambao hawana uwezo wa kununua moja kwa moja
3. Pesa ambazo mfanyabiashara ametumia kununua mashine hizi hupunguzwa kwenye kodi ambayo alipaswa kulipa
Tatizo ambalo tunajaribu kukwepa kulizungumza ni kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakitumia pesa ambazo zilipaswa kupelekwa TRA kwa faida yao
Kariakoo ni kitovu kikubwa cha ukwepaji kodi kwani wafanyabiashara hawapendi taarifa zao za biashara zijulikane ili waseme uongo.
Wamachinga wote wanaouza vifaaa vipya kama radio nk wanapewa mali kauli na wafanyabiashara hao ili kukwepa kulipa hiyo kodi.
Sisi wateja tunajiingiza kwenye mtego wa wafanyabiashara kwa kutodai risiti
Jamani kodi hiyo tunakamuliwa sisi wateja na wafanyabiashara wanatia ndani
 
Hivi kwanini watanzania hatupendi kulipa kodi? Sijui tunafikiri maendeleo yatashuka kutoka mbinguni?
watu wote wanapenda kulipa kodi , lakini huwezi hela zako zikaenda katika mtiririko ambao siyo , wao wawauzie hivyo vimashine ila si kwenda kununua kwa watu wengine tofauti na tra , hapo ndiyo tatizo na wawaajiri wataalamu wakuzitengeneza wa kwao wenyewe
 
Back
Top Bottom