Wadau wahoji busara ya kuuza umeme nje

Wadau wahoji busara ya kuuza umeme nje

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Profesa%20Sospeter%20Muhongo.jpeg

Profesa Sospeter Muhongo

Wasomi na wadau mbalimbali nchini wameshangazwa na tamko la serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ya kutaka kuuza umeme nje ya nchi wakati Watanzania wengi hawana huduma hiyo.

Wasomi hao walihoji busara ya kuuza umeme huo kama alivyosema Waziri wa wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, juzi wakati wa kutiliana saini na kampuni ya China ya Power Investment (CPI) juzi kuwa kuanzia mwakani kiasi cha megawati 500 kitauzwa ukiwa ni umeme wa ziada.

Jana Muhongo akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka cha Radio One, alisema wanakusudia kuuza nje ya nchi umeme kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali kila mwaka sambamba na kupanda kwa gharama za bidhaa mbalimbali.

Alibainisha kuwa wizara yake inao miradi ya aina tatu ambayo ni mradi wa kuzalisha umeme wakutosha kwa matumizi ya nchini, itakayofanya taifa lipate umeme wa ziada wa kuuza nje ya nchi; miradi ya kusafirisha umeme na wa tatu ni miradi ya kusambaza umeme.

Waziri Muhongo aliongeza kuwa kufikia mwakani Tanzania itakuwa inazalisha umeme mwingi kutokana na gesi asilia utakaotosha kutumia nyumbani na mwingine utakaouzwa, hivyo kukamilika kwa bomba la gesi nakujengwa kwa mitambo, nchi itakuwa na megawati zaidi ya mia tano na ifikapo mwaka 2015 Tanzania itakuwa na umeme wa ziada wa kuuza nje wa megawati1,500 na mwaka 2016 umeme waziada wa kuuza ambao hautakuwa chini ya megawati 1,800 .

Mchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi, alisema suala linaloelezwa na Wizara ya Nishati na Madini ni ndoto kwani kuamini kwamba ndani ya mwaka mmoja na nusu tutakuwa na umeme wa kutoshana kumaliza matatizo ya umeme nchini.

Nao wadau wa maendeleo wamelipigia kelele suala hilo kwakutaka wizara hiyo ihakikishe imetosheleza kwanza mahitaji ya nchi kabla ya kuanza kukimbilia kuiuza huduma hiyo kwa nchi nyingine.

Profesa Muhongo alisisitiza kuwa umeme na gesi vikitumiwa vizuri na kuuzwa nje ya nchi Tanzania itafuta umasikini kwa kipindi cha muda mfupi.

Waziri Muhongo alibainisha kuwatayari Kenya wamejitokeza mapema wakitaka huduma hiyo iuzwe kwao na majadiliano juu ya hilo tayari yamekwisha kuanza.

CHANZO: NIPASHE
 
wanaohoji ni mambulula kama taifa litazalisha umeme wa kutosha na kubaki na ziada baada ya kutumia kwa nini tusiuze halafu tukapata pesa za kufanyia mambo mengine.
 
itakuwa vigumu kwa serikali kuwa na ziada hiyo ya umeme ndani ya muda mfupi. Tuangalie hasa ni jinsi gani tuweze endesha shirika la umeme(Tanesco) kwa faida na sio tu kupiga kelele mara gesi mara ziada.
 
Kama umem unatosha mbona mkoa wa Kigoma na mikoa mingine umeme kwao ni ndoto miaka yote? Muhongo ajaribu kutumia busara kabla ya kutenda hapo kachapia xsana.
 
Ni umbulula wa hali ya juu kwa nchi yenye watu 45 million kufikiria kuuza umeme nchi za nje wakati watumiaji umeme nchini hawafiki hata laki 8. Yaani Watanzania wengine zaidi ya 44 million hawana umeme halafu nchi ikauze umeme nchi za nje.

Priority kubwa ingekuwa ni kuhakikisha umeme wa bei nafuu unasambazwa nchi nzima ili Watanzania walio wengi waweze kunufaika na nishati hiyo badala ya kuwanufaisha wananchi wa nchi jirani.
 
Kila
mwananchi alie na nyumba apate umeme.. Baada ya hapo ndiyo muuze...
 
Back
Top Bottom