Wadau wa Usindikaji tukutane hapa

Mkuu napenda unijuze juu ya hatua za usindikaji wa unga wa mahindi/sembe. Pia kuna tofauti kati ya unga wa viroba au sembe iliyo sindikwa na ile ya kukoboa nyumbani, tofauti hizi zipo katika ung'aavu na pia hata katika kiasi kitumikacho wakati wa kupika ugali, mfano ni kuwa sembe ya viroba hutumika kidogo na kutoa ugali mkubwa tofauti na ule wa kukoboa nyumbani. Lakini pia hata katika utunzani au muda wa kuharibika ni kuwa unga wa viroba unakaa kwa muda mrefu.
Je, nini cha ziada katika unga huo? pia je kuna kemikali zozote au virutubisho vya ziada?
 
Tofauti ni pale mahindi yanapokobolewa mengine husagwa muda huo huo na mengine kwa matumizi ya nyumbani huyaloweka kwa siku moja mbili kisha kuyaanika na kusaga. Unga huo Iringa huitwa kivelege. Ni mweupe na ladha ya pekee
 
Je, unafahamu njia bora za kusindika juisi ya matunda, na kuifanya ikae kwa muda mrefu bila kuharibika!
 
vyakula vingi huaribika mapema kutokana na sbabu mbalimbali ikiwemo, vijidudu, vimeng'enyo au uchafuzi wa aina mbalimbali.
Juisi ya matunda ni kati ya bidhaa ambazo zinahitaji umakini mkubwa ili isiharibike.
vitu vya muhimu vya kuzingatia katika uandaaji wa juisi ni hivi vifuatavyo;
  1. USAFI-usafi wa msindikaji, vyombo na mazingira ni muhimu ukadumishwa ili kupunguza uwezekano wa vijidudu na uchafu kuingia kwenye juisi yako. Vijidudu vinapokuwa vingi husababisha juisi kuharibika mapema zaidi
  2. MATUNDA-matumizi ya matunda mabovu au yaliyoharibika huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa juisi. kuna usemi wa kingereza unasema 'Gabbage In Gabbage Out'...usitegemee kupata juisi yenye ubora kwa kutumia matunda mabovu.
  3. kufuata kanuni za usindikaji kama vile kuchemsha juisi na matumizi ya preservatives. Juisi iliyochemshwa na kufungashwa inaweka kukaa kwenye friji wiki mbili hadi mwezi mmoja bila kuharibika...wakati juisi iliyochemshwa na kuwekewa preservatives inaweza kukaa miezi sita hadi mwaka bila kuharibika.
Preservative inayofaa zaidi kwenye juisi ya matunda ni Sodium Benzoate au Potassium Sorbate.
Na nyuzi joto zinazofaa kuchemshia juisi ni degree 80-90 C, kwa dakika 20.
 
Khasante mkuu! Ila niliwai kusikia eti wataalamu wanasaga juisi alafu wanabadilisha unakuwa ungaunga wa matunda ya kusagwa alafu wanahifadhi inakaa muda mwingi kabla ya kutengeneza juisi ya biashara?
 
Asante kwa utaalam, ningependa kusaga unga wa majani mfano mlonge muarobaini hata mbogamboga ili itumike kwa kinga na chakula kwa mifugo na binadamu. Je mashine ya kusaga nafaka itafaa au? Nitumie procedure gani kuhifadhika muda mrefu. Asante
 
Khasante mkuu! Ila niliwai kusikia eti wataalamu wanasaga juisi alafu wanabadilisha unakuwa ungaunga wa matunda ya kusagwa alafu wanahifadhi inakaa muda mwingi kabla ya kutengeneza juisi ya biashara?
yah..itz possible but cha kuwa nacho in mind ni kwamba unapokausha maji huondoka so kama ulikua na kilo 10 za pulp unaweza pata kilo 5 za unga au chini zaidi..so kama unataka kukausha ni vyema ukafanya mchakato huu kipindi cha msimu au maeneo yenye matunda mengi...
 
Asante kwa utaalam, ningependa kusaga unga wa majani mfano mlonge muarobaini hata mbogamboga ili itumike kwa kinga na chakula kwa mifugo na binadamu. Je mashine ya kusaga nafaka itafaa au? Nitumie procedure gani kuhifadhika muda mrefu. Asante
unaweza tumia but haitakupa matokeo mazuri...nakushauri tafuta mashine kama zile zinazosagia spices/ viungo
 
Mkuu vip kuhusu maziwa fresh nayenyewe yanasindikwaje?
Sawa mkuu..zipo njia nyingi zakusindika maziwa kulingana na matakwa ya msindikaji...maziwa fresh yanaweza kusindikwa yakabaki fresh au yakatengeneza bidhaa mbalimbali kama vile; MTINDI, YOUGURT, MAZIWA YA UNGA, UHT-MILK. CHEAZE,BUTTER, au yakabaki fresh kama yalivyo au yakaondolewa mafuta (Low fat)
 
Back
Top Bottom