Wadau wa usafirishaji

Abby Senior

Senior Member
Feb 14, 2015
154
60
Habari zenu wadau,

Ninaomba kufahamishwa juu ya hizi mizani za mkeka, utakuta gari ya mzigo (semi trailer) zinapita mizani zote bila kuzidi uzito, lakini katika mizani za mkeka lazima kwenye difu excel moja inazidi, unaambiwa ulipe faini, unapohoji unaambiwa kwa zile mizani za group ni sawa.

Ila kwa hizi za mkeka imezidi, na ukijaribu kupanga usawa wa mizani za mkeka, ukipima kwenye group inazidi kwenye difu, hivi huu ni mpango wa makusudi kutukomoa au vipi?Mizani zinazosumbua kwa mtindo huu ni Kihonda na Dodoma. Sasa tufuate mpango upi?

Naomba mwenye ufahamu zaidi anisaidie.
 
Back
Top Bottom