Wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakutana na Waziri husika kujadili marekebisho ya Sheria ya NGOs

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazaa na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imeandaa mkutano na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs) lengo likiwa ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali kupitia Sheria ya marekebisho Namba 3 ya 2019

Miongoni mwa waliopo meza kuu ni Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri Faustine Ndugulile, Mwenyekiti wa NACONGO, Nicholaus Zacharia, Katibu Mkuu wa Wizara, John K. Jingu.

M/Kiti NACONGO

Sisi kama NACONGO hatuna shaka na sheria hii. Nimetoa agizo elimu ikatolewe mikoani kuhusu Sheria hii. Tumepata taarifa kuwa zipo baadhi ya NGO za kimataifa zilizopelekewa maneno kuhusu sheria, na sasa wanataka kuondoka ama kufanya kazi kutoka nje.

Naomba niseme hakuna kitu kama hicho na ningependa kuwatoa hofu wawakilishi wa NGO hizi.

Mwenyekiti Bodi ya Uratibu wa NGO

Bodi ya uratibu wa NGO inafarijika na utayari wa wadau kukutana, kujadili na kuelewa pamoja.

Kupitishwa kwa sheria hii nina imani kutaongeza ufanisi na kutuwezesha kutimiza wajibu wetu

Naipongeza Serikali na nina imani changamoto za kutokuwa na usajili chini ya sheria moja zitatatuliwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, John K. Jingu

Lengo la leo ni kujadiliana kuhusu mabadiliko ya sheria hususani panapohusu NGOs sababu nimesikia kuna wadau wana wasiwasi.

Sisi kama wasimamizi wa sheria zinazohusu NGO tutaeleza utekelezaji tunapanga kuufanya namna gani ili twende pamoja.

Naamini baada ya kikao sintofahamu zitaondoka.

Nasikia kuna asasi za kiraia za nje zimeambiwa kuwa zitafutwa zisiwepo kabisa. Hili si kweli.

Mgeni Rasmi, Dkt. Ndugulile

Kama Serikali tunathamini, tunatambua na tunauenzi mchango wa NGOs

Mmekuwa mkitusaidia kutusogeza pale Serikali inapoishia. Pia mmetoa ajira, tunatambua mchango wenu.

NGOs zimeongezeka sana kuanzia 2005 ambapo zilikuwa 404, hadi sasa tuna 9,310. Ni mwitikio huu ndio umepelekea tuone kuna maeneo yana changamoto.

1. Mojawapo ya maeneo yenye changamoto ni usajili. Wengine wanaenda kujisajili BRELA, RITA, Wizara ya Mambo ya Ndani lakini wanafanya kazi za NGO. Tukaona mkono wetu unashindwa kuwafikia wale. Vilevile NGO nyingine zikawa zinafanya biashara.

2. Lingine limetupa changamoto ni kuwa sisi tunasimamia NGOs lakini tunapata shida kupima mchango wa NGOs katika uchumi. Tunakuwa hatuna taarifa sometimes.

Tunataka tuwe tunatambua, inawezekana hata kwenye bajeti mna mchango wenu lazima tujue kwa kupima.

3. Mmekuwa mkihimiza uwazi na uwajibikaji kwa Serikali na tunashukuru kwa hilo lakini na sisi tunataka tufanya upande wenu. Pesa mnazopokea ni kwa niaba ya watanzania.

Mnakuja kuomba barua kwetu( endorsement letter); tutawaandikiaje ikiwa hatujui mfanyacho?

4. Vipaumbele

Kuna maeneo yana mrundikano wa NGOs na sehemu nyingne hazina NGOs ilhali watanzania ni wale wale.

Unakuta NGO 5 zinajenga uwezo kwa watumishi wa afya kwenye wilaya moja.

Tumeanza kuandaa database ya NGOs ambayo itakuwa na taarifa za mko wapi mnafanya nini ili akija mtu mpya tutakubaliana aende wapi, akafanye nini kwa vipaumbele vipi. Hii ni kwa sababu imefika mahali tunakanyagana wakati nchi ni kubwa.

Kama Serikali lazima tukiri kuwa tulilega kidogo tulikuwa hatuna Bodi, Msajili kwa muda mrefu. Sheria na Sera viendane na mazingira.

Tumeteua Bodi, Rais Magufuki ameteua Msajili na Mkurugenzi wa idara. Sasa tunataka kuimarisha mifumo ya kisheria ikiwemo mabadiliko haya ya sheria.

Kama ulisajiliwa huko kote na unafanya kazi za Asasi za Kiraia tunatoa kipindi cha mpito mje kujisajili huku kwenye NGOs. Kama uko huku na unaona malengo yako yanaangukia kwingine ondoka.

Natoa taarifa hizi maana kunapokuwa na ombwe la taarifa watu wanaanza kutengeneza taarifa zao.

Tutaanza kufanya uhuishaji wa usajili kwa taasisi

1. Wote waliokuwa wamejisajili vyombo vingine na wanataka kuja huku, usajili unaanza leo. Kuna fomu zina taarifa rahisi tu kujaza.

2. Wanaotaka kusajili NGO mpya pia wanaweza kujisajili.

Awamu ya pili

Kutakuwa na usajili awamu ya pili baada ya miaka 10 ya usajili. Wengine wanatoa vyeti vya mwaka mmoja ama miwili lakini sisi tunatoa miaka 10 hatukugusi. Kuna watu wanakuwa na uoga ambao haupo

Zoezi la usajili litaanza Kanda ya Mashariki kwa siku 9 katika majengo ya Wizara hapa Dar es Salaam.

Kanda ya Kati usajili utakuwa Dodoma katika ofisi za Wizara UDOM.

Kanda ya Kaskazini ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa

Kanda ya ziwa Mwanza ofisi ya Katibu Tawala

Nyanda za juu Kusini ofisi ya Katibu Tawala

Mtu anaweza pata huduma popote kutokana na urahisi wake.

Maagizo kwa Watendaji wa Wizara

Nataka zoezi liende vizuri wadau wasipate shida. Fomu ziwe electronic, nataka baada ya muda mfupi system iwe tayari mtu ajaze fomu, aweke attachments na alipe huko. Natoa wiki mbili. Haileti maana mtu atoke Mtwara aje Dar kukusanya karatasi.

Pia mfumo wa kutoa taarifa na Ripoti kwa NGOs uwe online.

Kama kuna mtendaji wa Wizara ambaye hatatoa ushirikiano naomba mje kwangu.

Ufafanuzi wa Marekebisho ya Sheria kutoka kwa Mwanasheria wa Wizara

Sheria hii imefanyiwa marekebisho kwenye vifungu takribani 6.

Kifungu cha 28 kimetambua NGO kuwa ni zile tu zinazolenga kunufaisha jamii(kutofautisha maslahi binafsi), pia taasisi za kijamii kuwa miongoni mwa NGO.

Malengo ya serikali ilikuwa kuweka wigo wa kutambua nini ni NGO na nini si NGO.

Serikali imeweka majukumu ya ziada kwa msajili kwenye kifungu cha 30. Hii ni pale Asasi inapokiuka masharti.

Imeongeza jukumu la msajili kufuatilia taarifa za activities za NGO kila robo mwaka.

Kuruhusu/kumpa nguvu msajili aweze kushirikia na vyombo vya dola/vyombo vingine.

Imeongeza masharti ya matumizi ya cheti(uhuishaji wa cheti cha kujisajili na si kujisajili upya)

Sheria imeeleza taarifa za mapato na matumizi zinatakiwa kuwekwa bayana.
 
Back
Top Bottom