Wadau Tusaidiane kwa hili

Wadau Tusaidiane kwa hili

MO11

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
19,553
Reaction score
41,467
House girl alitandika kitanda cha
bosi wake Kama Sehemu ya
jukumu lake la kila siku.
Alipomaliza akakitazama sana kile
kitanda cha bosi wake akasema
naweza kufa bure bila ya kulalia
kitanda kama hiki. Akasema ngoja
nijaribu kulala angalau kidogo.
Akavua nguo zote akaziweka chini,
akabaki na gagulo tu akawasha AC
akajifunika brangeti gubigubi
akalala. Kwa bahati mbaya usingizi
ukampitia kweli akalala fofofo.
Ghafla Mume wa bosi akarudi na
haikuwa kawaida yake kurudi Muda
huo. Alipoingia chumbani, akajua
hakika huyu ni mke wangu na kwa
kuwa jana tulikwaruzana atakuwa
amekasirika tu. Akaogopa
kumwamsha. Mwanamme
akasaula, akabaki na msuli naye
akajifunika hilo hilo blanketi kwa
taratibu sana kwa hofu ya
kumwamsha mke wake. Kwa
bahati mbaya naye usingizi
ukampitia, akalala fofofo .
Mkewe aliporudi, akaingia
chumbani, akakuta watu wawili
wamelala fofofo. Akafunua
blanketi kwa nguvu, akawakuta
wote wawili; yaani yule mfanyakazi
na mume wake wamelala pamoja.
Walipoulizwa kila mtu akaeleza
ukweli wake.


1. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo
yule mke wa bosi ungewaelewa?

2. Je, kama wewe ungekuwa ndiyo
yule mfanyakazi ungejitetea vipi?

3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule
bosi ungejitetea vipi?

4. Je hapo ugomvi utakuwa
umesababishwa na nani? Mke,
mume au mfanyakazi?
 
nisingewaelewa jasho la boss na h/grl tofauti mume asigundue hata hiyo tofauti ndogo?

Ndio ishatokea wewe utawaelewa au utakusanya vyako ulale mbele ?
 
Eti aliwasha AC na kijifunika blanketi gubi gubi,km alikuwa anasikia baridi aliwasha AC ya nini????
 
nisingewaelewa jasho la boss na h/grl tofauti mume asigundue hata hiyo tofauti ndogo?

Utachukua maamuzi gani ikiwa wewe ni
(1) mwenyenyumba mume amukufuata.
(2) mwenyenyumba ni mume
 
Hapoo inaitajika akilii ya kuzaliwa kusuluhishaa .ukiweka akili ya darasan unaaribu ndoaa
 
Kwanza mke na H/g ni tofauti, na hicho chumba kulikua na Giza Kama kaburi usione sura? Harufu ya mkeo huijui? Au urefu wa mkeo huujuii? Mkeo analalaje? Humkubatii hata mkigombana? Na huyo H/G hakuona siku ya kulala hapo mpaka siku hiyo? Mie apana hata sielewi, harufu ya Udi wangu perfume yangu mumewangu ata ijua hata nipite nimevaa ninja, nnavyo lala Atajuaa tuu Huyu ni mke wangu... Hayo Mashaka mengine atakua ame amua...
 
Kama hakukuwa na CCTV Camera humo ndani ya ku-prove wayasemayo basi hiyo yaweza kugeuka murder case.
 
Eti aliwasha AC na kijifunika blanketi gubi gubi,km alikuwa anasikia baridi aliwasha AC ya nini????

Hahahahahaaa Jestina bhana hem acha kutukata stimu....hata kama unahitaji baridi kujifunika muhimu lol
 
Last edited by a moderator:
Haya mambo ya kufikirika bwana ngumu sana kuyatransform kwenda kwenye reality halafu ukapata majibu
 
Ningemwambia "hakyanani waif sijamla bekitaraa,hebu mkague! kama unabisha saula!" nampiga waif show ya kufa mtu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom