Wadau nishaurini kwa hili

Wadau nishaurini kwa hili

Bartazar

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
1,049
Reaction score
571
Nimeishi na Mwanamke huu ni mwaka wa tano, japo haikuwa ndoa rasmi. Baada ya taratibu za mahari tu nilimsogeza japo sijafunga naye ndoa ya kidini wala kiserikali. Miaka minne iliyopita, nikiwa mwanafunzi wa chuo UDSM, na yeye nikimwacha nyumbani (Mkoani), niliporudi likizo moja, rafiki zangu walinitonya kuwa yf alikuwa anamegwa na jamaa mmoja ambaye namfahamu alikuwa dereva wa jirani yangu.

Sikumwambia kuhusu maneno niliyoyasikia, ila niliazimia kufanya upelelezi wa kimya kimya, ili nigundue kama kulikuwa na mawasiliana yoyote kati yao, sikufanikiwa. Nikajiaminisha kuwa kama yf alikuwa anafanya hayo, lazima alikuwa smart sana. Baada ya likizo ile nilirejea Dar kuendelea na shule. Likizo nyingine niliporudi, nakumbuka ilikuwa march 12, 2010 nilirudi na unyumba uliendelea kama kawaida. Sikukaa sana, nikarudi chuo, na nilipomaliza chuo mwaka huo, yaani july 2010 nilirudi nyumbani na nikamkuta ni mja mzito, japo muda wote niliokuwa chuo hakuwahi kunieleza kuwa ni mjamzito. Nilifurahi kwa kuwa nilijua sasa nitaitwa baba. Hesabu ziliniambia, miezi tisa ingetimia kuanzia desemba 12, 2010. Mwezi November mwaka huo huo nilikwenda kwenye mahafali Dar, siku tatu tu baada ya kuondoka, kwa mshangao nilipigiwa simu kuwa yf aliugua uchungu wa kujifungua, hiyo ilikuwa November 18,2010.

Kwa hiyo alijifungua mwezi mmoja kabla ya tarehe niliyoitarajia. Hiyo haikunisumbua sana kwa kuwa nilikuwa najua akina mama huwa wanajifungua mimba zikiwa na umri wa miezi saba, japo sijawahi kusikia akina mama wenye mimba zenye umri wa miezi 8 wakijifungua na watoto wakaishi, wangu alijifungua bila tatizo lolote na mtoto akiwa perfect.

Hivi majuzi rafiki yangu kanipa stori ambapo imenitonesha kumbukumbu zangu hizo, aliposema bora aniambie ukweli anaoujua siku nyingi kuwa yule mtoto nimechomekewa. Kwamba kimsingi, mtoto ni wa yule mtuhumiwa wangu. Na pia kwamba wakati sipo, yf alitoa mimba nyingine ya huyo jamaa. Nikiunganisha dots napata picha kuwa kuna ukweli flani hapo ukizingatia mtiririko wa matukio ulivyokwenda. Na kaniambia mjini pale watu wanaijua sana hii stori na wananionea huruma tu na kunisikitikia. Sasa wanabodi nadhani mnanielewa ninachosema, nishaurini tafadhali, nisije nikafanya vitu vya ajabu kwa kuwa moyo wangu umejaa hasira, ila sasa hivi nipo mbali naye sababu ya majukumu. Kabla sijarudi nishaurini nifanye nini!
 
Hapo ushauri gani unataka ndugu yangu? Piga chini haraka sana kama una vithibitisho vya kutosha.
 
ulichunguza hukuambulia kitu.....

Halafu huyo rafiki yako alijuaje kama mkeo alitoa mimba? Yeye ndo daktari? Alimsindikiza kwa daktari?

Ni vyema ukachunguza taratibu pamoja na kuchunguza mwenendo wa mkeo kimya kimya

Pia katika marafiki zako woooooooooooote ni huyo tu mwenye info za mkeo?

Yaani hata nduguzo hawakujua kama mkeo katoa mimba? Hawajui mkeo anatembea na dereva ilhali mtaa mzima wanajua na wanakuhurumia?

Chunguza kaka inawezekana kuna ukweli au hakuna ukweli au rafiki yako ndo mbaya wako

Ingawa kwa ninj mkeo apate mimba asikuarigu?
Kwa nini hata nduguzo wasizungumzie mimba ya mkeo?
 
Asante BADILI TABIA.
Wewe unajitaftia ulcers. Mimba hutungwa siku isiyojulikana na ndo maana dr wanategemea izaliwe wiki 2 kabla ama baada ya tarehe iliyokisiwa. Hapo tofauti ya siku ingekuwa miezi 3 tungesema. Na acha na stori za mtoto wa miezi 8 haishi, sayansi ilishashinda hayo.

Maneno ya kuambiwa yatakutia wazimu na kukukosesha raha ya maisha. Utasikiliza maneno mangapi? Hebu uishi na mkeo mfurahie mafanikio. Kama kuna lililojificha sali muambie Mungu nionyeshe yaliyofichika. Kama kuna jambo utaliona tu na sikushauri kujigeuza mbwa wa polisi kila siku kumchunguza mkeo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hiyo iko wazi kabisa,huyo rafiki yako anakujali ingawa wengine watamuona muongo,mmbeya.Hapo amua moja piga chini uanze upya au endelea nae huku ukijua siyo mwaminifu.Pole sana,uaminifu katika ndoa siku hizi umekuwa nadra sana.
 
Nimeishi na Mwanamke huu ni mwaka wa tano, japo haikuwa ndoa rasmi. Baada ya taratibu za mahari tu nilimsogeza japo sijafunga naye ndoa ya kidini wala kiserikali. Miaka minne iliyopita, nikiwa mwanafunzi wa chuo UDSM, na yeye nikimwacha nyumbani (Mkoani), niliporudi likizo moja, rafiki zangu walinitonya kuwa yf alikuwa anamegwa na jamaa mmoja ambaye namfahamu alikuwa dereva wa jirani yangu.

Sikumwambia kuhusu maneno niliyoyasikia, ila niliazimia kufanya upelelezi wa kimya kimya, ili nigundue kama kulikuwa na mawasiliana yoyote kati yao, sikufanikiwa. Nikajiaminisha kuwa kama yf alikuwa anafanya hayo, lazima alikuwa smart sana. Baada ya likizo ile nilirejea Dar kuendelea na shule. Likizo nyingine niliporudi, nakumbuka ilikuwa march 12, 2010 nilirudi na unyumba uliendelea kama kawaida. Sikukaa sana, nikarudi chuo, na nilipomaliza chuo mwaka huo, yaani july 2010 nilirudi nyumbani na nikamkuta ni mja mzito, japo muda wote niliokuwa chuo hakuwahi kunieleza kuwa ni mjamzito. Nilifurahi kwa kuwa nilijua sasa nitaitwa baba. Hesabu ziliniambia, miezi tisa ingetimia kuanzia desemba 12, 2010. Mwezi November mwaka huo huo nilikwenda kwenye mahafali Dar, siku tatu tu baada ya kuondoka, kwa mshangao nilipigiwa simu kuwa yf aliugua uchungu wa kujifungua, hiyo ilikuwa November 18,2010.

Kwa hiyo alijifungua mwezi mmoja kabla ya tarehe niliyoitarajia. Hiyo haikunisumbua sana kwa kuwa nilikuwa najua akina mama huwa wanajifungua mimba zikiwa na umri wa miezi saba, japo sijawahi kusikia akina mama wenye mimba zenye umri wa miezi 8 wakijifungua na watoto wakaishi, wangu alijifungua bila tatizo lolote na mtoto akiwa perfect.

Hivi majuzi rafiki yangu kanipa stori ambapo imenitonesha kumbukumbu zangu hizo, aliposema bora aniambie ukweli ambao anaujua siku kuwa yule mtoto nimechomekewa. Kwamba kimsingi, mtoto ni wa yule mtuhumiwa wangu. Na pia kwamba wakati sipo, yf alitoa mimba nyingine ya huyo jamaa. Nikiunganisha dots napata picha kuwa kuna ukweli flani hapo ukizingatia mtiririko wa matukio ulivyokwenda. Na kaniambia mjini pale watu wanaijua sana hii stori na wananionea huruma tu na kunisikitikia. Sasa wanabodi nadhani mnanielewa ninachosema, nishaurini tafadhali, nisije nikafanya vitu vya ajabu kwa kuwa moyo wangu umejaa hasira, ila sasa hivi nipo mbali naye sababu ya majukumu. Kabla sijarudi nishaurini nifanye nini!

kapime DNA
 
hizi habari za kuambiwa mtoto sio wako bila vipimo vya DNA usiziamini,fanya uchunguzi wa kina!! marafiki tunao lakini sio wote wanatutakia mema, alafu hii tabia ya kusikiliza maneno ya watu wa nje na kuyaamini haraka haraka ni moja ya vitu vinavyopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi.
 
ulichunguza hukuambulia kitu.....

Halafu huyo rafiki yako alijuaje kama mkeo alitoa mimba? Yeye ndo daktari? Alimsindikiza kwa daktari?

Ni vyema ukachunguza taratibu pamoja na kuchunguza mwenendo wa mkeo kimya kimya

Pia katika marafiki zako woooooooooooote ni huyo tu mwenye info za mkeo?

Yaani hata nduguzo hawakujua kama mkeo katoa mimba? Hawajui mkeo anatembea na dereva ilhali mtaa mzima wanajua na wanakuhurumia?

Chunguza kaka inawezekana kuna ukweli au hakuna ukweli au rafiki yako ndo mbaya wako

Ingawa kwa ninj mkeo apate mimba asikuarigu?
Kwa nini hata nduguzo wasizungumzie mimba ya mkeo?

Wewe nawe.... unafikiri kila mtu ana guts za kusema hii makitu. Kuna swahiba wetu anamegewa mkewe na kichalii flani na wote tunajua. Hakuna anayethubutu kumwambia. Tukaona isiwe tabu tukatafuta baunsa moja akakapige mkwala kale kachalii. Jamaa akaja na jibu kachalii kamemwambia "braza ingekuwa njema ungemfuata yule maza umwambie kwa kuwa ni yeye ndie anayetaka"

Mambo kama haya ukimpata mtu mwenye uthubutu wa kukwambia, mshukuru Mungu na chukua hatua. Namwonea huruma swahiba anavyopita kitaa kila mtu anamchora.

Mi huwa nakasikaga chapchap sana.
 
Asante BADILI TABIA.
Wewe unajitaftia ulcers. Mimba hutungwa siku isiyojulikana na ndo maana dr wanategemea izaliwe wiki 2 kabla ama baada ya tarehe iliyokisiwa. Hapo tofauti ya siku ingekuwa miezi 3 tungesema. Na acha na stori za mtoto wa miezi 8 haishi, sayansi ilishashinda hayo.

Maneno ya kuambiwa yatakutia wazimu na kukukosesha raha ya maisha. Utasikiliza maneno mangapi? Hebu uishi na mkeo mfurahie mafanikio. Kama kuna lililojificha sali muambie Mungu nionyeshe yaliyofichika. Kama kuna jambo utaliona tu na sikushauri kujigeuza mbwa wa polisi kila siku kumchunguza mkeo.

We mrembo acha kumdanganya chalii. Analea kibudu huyo. Tena amshukuru aliyemwambia mapema kabla hajaanza kulea wajukuu kharam.

Mara nyingi sana lisemwalo lipo.
 
Last edited by a moderator:
Wema usizidi uwezo

Asante BADILI TABIA.
Wewe unajitaftia ulcers. Mimba hutungwa siku isiyojulikana na ndo maana dr wanategemea izaliwe wiki 2 kabla ama baada ya tarehe iliyokisiwa. Hapo tofauti ya siku ingekuwa miezi 3 tungesema. Na acha na stori za mtoto wa miezi 8 haishi, sayansi ilishashinda hayo.

Maneno ya kuambiwa yatakutia wazimu na kukukosesha raha ya maisha. Utasikiliza maneno mangapi? Hebu uishi na mkeo mfurahie mafanikio. Kama kuna lililojificha sali muambie Mungu nionyeshe yaliyofichika. Kama kuna jambo utaliona tu na sikushauri kujigeuza mbwa wa polisi kila siku kumchunguza mkeo.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja ampige chini afu baada ya miezi 3 wife anahamia kwa mshkaji huyo huyo. Patanoga balaa. Unless amechunguza na kuwa na uhakika hapaswi kuchukua hatua
Mkuu hiyo iko wazi kabisa,huyo rafiki yako anakujali ingawa wengine watamuona muongo,mmbeya.Hapo amua moja piga chini uanze upya au endelea nae huku ukijua siyo mwaminifu.Pole sana,uaminifu katika ndoa siku hizi umekuwa nadra sana.
 
bartazar hata ushauriwe vp. kama umeshajirzsha na shuhuda hzo, mbmuz unayo mwenyewe kaka uctegemee m2 . masuala ya ndoa ni magumu sana. ningekua mimi ningeshatimua muda mrefu sana
 
wee chakufanya hapo ni kwenda home na kumweka kitimoto yf na kudemand ukweli wa mambo. baada ya hapo unamwita yule njemba aje alafu mnamgegeda na kumla tigo huyo yf
 
ulichunguza hukuambulia kitu.....

Halafu huyo rafiki yako alijuaje kama mkeo alitoa mimba? Yeye ndo daktari? Alimsindikiza kwa daktari?

Ni vyema ukachunguza taratibu pamoja na kuchunguza mwenendo wa mkeo kimya kimya

Pia katika marafiki zako woooooooooooote ni huyo tu mwenye info za mkeo?

Yaani hata nduguzo hawakujua kama mkeo katoa mimba? Hawajui mkeo anatembea na dereva ilhali mtaa mzima wanajua na wanakuhurumia?

Chunguza kaka inawezekana kuna ukweli au hakuna ukweli au rafiki yako ndo mbaya wako

Ingawa kwa ninj mkeo apate mimba asikuarigu?
Kwa nini hata nduguzo wasizungumzie mimba ya mkeo?

Ngugu zangu wapo mbali na ninapoishi. Huyu aliyeniambia safari hii, ni tofauti kabisa na wale wa awali, ni rafiki yangu wa siku nyingi na haishi jirani sana na mimi ila anaamini waliomwambia hawawezi kuzua. Hadi yeye kajua hii stori, ni wazi yamezungumzwa mengi sana mitaani.
 
acheni kusikiliza maneno ya kuambiwa, ooohooo! mie sisemi sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom