Wadau nishaurini kwa hili

Wadau nishaurini kwa hili

hivi nyie mnaomshauri aachane na mkewe mnataka awaoe yie??? Agrrrrh! Mbona kama hujiamin ndugu? We ulifanya uchunguz hukugundua chochote, leo kwa kuambiwa unaanza kupaniki. Maneno ya kuambiwa kwenye ndoa kuwa nayo makini sana
 
mkuu hebu tuwe wa kweli....

hivi muda wote uliokuwa chuoni HUKUCHAKACHUA??

ushairi wangu ACHA TABIA YA KUKAA MBALI NA MKEO. Fimbo ya mbali haiui nyoka.

Kiukweli kabisa nimechakachua, ila hata yeye nilimwambia, ilikuwa hivi, baada ya kudeliver, aligoma kabisa kugegedana mwaka mzima kwa madai kuwa analea. Nikamwambia ananiwekea mazingira magumu, asije akanilaumu nikitafuta kidumu. Akanambia bora tu nikatafute kidumu kuliko yeye kugegedana. Mie nikafanya kweli, alipokuja kusikia kawa mbogo, nikamkumbusha nilipomtahadharisha mapema kabisa. Niambie hapo nilikosea?!
 
Kitanda hakizai haramu mzigo wako huo, ulee tu kaka.

Si rahisi kaka kama unavyodhani, heri nisingejua kabisa! Najua wengi wapo kama mimi, wanalea watoto si wao ila hawajui.
 
sitaki kusutwa mie.....ila kwanini unaishi na mchumba?
 
Nimeishi na Mwanamke huu ni mwaka wa tano, japo haikuwa ndoa rasmi. Baada ya taratibu za mahari tu nilimsogeza japo sijafunga naye ndoa ya kidini wala kiserikali. Miaka minne iliyopita, nikiwa mwanafunzi wa chuo UDSM, na yeye nikimwacha nyumbani (Mkoani), niliporudi likizo moja, rafiki zangu walinitonya kuwa yf alikuwa anamegwa na jamaa mmoja ambaye namfahamu alikuwa dereva wa jirani yangu.

Sikumwambia kuhusu maneno niliyoyasikia, ila niliazimia kufanya upelelezi wa kimya kimya, ili nigundue kama kulikuwa na mawasiliana yoyote kati yao, sikufanikiwa. Nikajiaminisha kuwa kama yf alikuwa anafanya hayo, lazima alikuwa smart sana. Baada ya likizo ile nilirejea Dar kuendelea na shule. Likizo nyingine niliporudi, nakumbuka ilikuwa march 12, 2010 nilirudi na unyumba uliendelea kama kawaida. Sikukaa sana, nikarudi chuo, na nilipomaliza chuo mwaka huo, yaani july 2010 nilirudi nyumbani na nikamkuta ni mja mzito, japo muda wote niliokuwa chuo hakuwahi kunieleza kuwa ni mjamzito. Nilifurahi kwa kuwa nilijua sasa nitaitwa baba. Hesabu ziliniambia, miezi tisa ingetimia kuanzia desemba 12, 2010. Mwezi November mwaka huo huo nilikwenda kwenye mahafali Dar, siku tatu tu baada ya kuondoka, kwa mshangao nilipigiwa simu kuwa yf aliugua uchungu wa kujifungua, hiyo ilikuwa November 18,2010.

Kwa hiyo alijifungua mwezi mmoja kabla ya tarehe niliyoitarajia. Hiyo haikunisumbua sana kwa kuwa nilikuwa najua akina mama huwa wanajifungua mimba zikiwa na umri wa miezi saba, japo sijawahi kusikia akina mama wenye mimba zenye umri wa miezi 8 wakijifungua na watoto wakaishi, wangu alijifungua bila tatizo lolote na mtoto akiwa perfect.

Hivi majuzi rafiki yangu kanipa stori ambapo imenitonesha kumbukumbu zangu hizo, aliposema bora aniambie ukweli ambao anaujua siku kuwa yule mtoto nimechomekewa. Kwamba kimsingi, mtoto ni wa yule mtuhumiwa wangu. Na pia kwamba wakati sipo, yf alitoa mimba nyingine ya huyo jamaa. Nikiunganisha dots napata picha kuwa kuna ukweli flani hapo ukizingatia mtiririko wa matukio ulivyokwenda. Na kaniambia mjini pale watu wanaijua sana hii stori na wananionea huruma tu na kunisikitikia. Sasa wanabodi nadhani mnanielewa ninachosema, nishaurini tafadhali, nisije nikafanya vitu vya ajabu kwa kuwa moyo wangu umejaa hasira, ila sasa hivi nipo mbali naye sababu ya majukumu. Kabla sijarudi nishaurini nifanye nini!

kaa na mkeo myamalize usipende fanya maamuzi kwa story za kusikia
 
Hata huyo aliyekuletea hayo maneno naye vile vile ni swatana. Kuoa mke na kumwacha muda mrefu nayo pia ni mbaya. Kupima dna hata wewe utadhoofika kwa kuwa moja kwa moja siyo mwanao. Chukua uamuzi mgumu wa kusema na mkeo. Akiomba msamaha maisha yaendelee tu. Hata ukaoa mwingine hawa watu tabia hazipishani sana. pole mtoto wa kiume be strong.
 
why suffer msomi mzima umeenda shule kufanya nini
...........go for DNA broda
 
sitaki kusutwa mie.....ila kwanini unaishi na mchumba?

Hii kitu ingetokea nikiwa nimefunga ndoa, ningekuwa na hali ngumu zaidi. Kwa maneno mengine, imenisaidia kupunguza msongo kwa kuwa najua ikithibitika habari ni za kweli, kutakuwa na options nyengine kirahisi!
 
Hata huyo aliyekuletea hayo maneno naye vile vile ni swatana. Kuoa mke na kumwacha muda mrefu nayo pia ni mbaya. Kupima dna hata wewe utadhoofika kwa kuwa moja kwa moja siyo mwanao. Chukua uamuzi mgumu wa kusema na mkeo. Akiomba msamaha maisha yaendelee tu. Hata ukaoa mwingine hawa watu tabia hazipishani sana. pole mtoto wa kiume be strong.
ikiwa ndoa zenyewe ndo hizi bora kutokuoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom