Wadau naombeni mtazamo wenu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau naombeni mtazamo wenu....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Planner, May 14, 2011.

 1. Planner

  Planner JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni jumamosi nyingine, siku ambayo naamini tulio wengi tunaipenda. Kabla ya kuwatakia week end njema wadau nimekuwa nikijiuliza baadhi ya maswali kuhusu baadhi ya mambo. Jambo la kwanza ni kuhusu wimbo wa Taifa, una maneno mengi na mazuri yanayotia moyo, MUNGU anaombwa awabariki viongozi wetu, alibariki bara letu la Afrika, awape hekima na vitu vingine muhimu kwa viongozi ambao nyuma yao kuna kundi kubwa la watu waliokata tamaa huku wakitegemea uadilifu, hekima na busara za viongozi ili wafanikiwe kimaisha.

  Pamoja na maombi yote hayo Bara la Afrika bado limegubikwa na migogoro isiyokwisha, ule umoja tunaomwomba MUNGU umekuwa utengano na ubaguzi. Ile hekima tunayowaombea viongozi wetu imekuwa kinyume chake, viongozi wamekuwa wajasiriamali, kila fursa wanayoipata wanaitumia kujinufaisha wao na familia zao. Baadhi ya viongozi wetu wameacha kutumia vichwa kufkiri bali wametanguliza tamaa na njaa ya matumbo yao! Tukiangalia katika muktadha huo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kwamba MUNGU HASIKII SALA ZETU?

  Kwa upande mwingine nimekuwa nikijaribu kujiuliza kuhusu bendera yetu ya Taifa, hasa zile rangi zake na mantiki iliyo nyuma za zile rangi. Nakumbuka tuliambiwa kwamba ile rangi ya njano inawakilisha uwepo wa rasilimali muhimu za madini. Kwa kasi hii ya uchimbaji inayoendelea na usimamizi (ili kufaidi rasilimali) usioridhisha (kufaidi kuna uwezekano mkubwa sana baada ya muda si mrefu rasilimali hiyo ikaisha kabisa hasa tukizingatia kwamba rasilimali madini sio RENEWABLE wanasema wale waliosoma bure kwa kodi za walala hoi. Hapa napata kaswali ka kizushi, hivi itakapofika siku wataalamu wetu wakatuambia kwamba sasa hivi madini kushnei Tanzania, ile rangi ya njano kwenye bendera itaondolewa? Na kama itabaki itakuwa inawakilisha madini au YANGA?:dance:
   
Loading...