Nafikiri andiko lako linakosa nguvu,ungejitahidi kuwa specific juu ya kile unachohitaji kufahamishwa.Kwa mfano labda bei,brand gani ni zuri zaidi kwenye ufanisi,lakini pia ninavyofahamu mimi hizi mashine zipo tunazotengeneza wenyewe hapa nyumbani lakini pia tuna ambazo tunaagiza kutoka nje.
Pia zipo ambazo ni automatic na nyingine ni mannual na hasa kwa hizi ambazo tunazitengeneza wenyewe.Nafikiri hapa kwa upande wa mashine nitakua nime cover kwa baadhi ya maeneo.
Baada ya hapo utahitaji kufahamishwa namna ya uendeshaji wake.Mfano mayai yakuwekwa kwenye mashine yanatakiwa yawe yametagwa ndani ya wiki moja,Lakini pia uhifadhi wa haya mayai huwa yananamna yake yakuhifadhi ile ncha ya yai inatizama juu kwa kawaida.Lakini pia ni vema ukawa na standby generator kwani umeme wetu haina uhakika.
Kwa anayefahamu vizuri basi atakufahamisha vizuri hasa kwenye nyanja hizo.