Wadau na Jukwaa muhimu zaidi ndani ya JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wadau na Jukwaa muhimu zaidi ndani ya JF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by firstcollina, Jun 18, 2010.

 1. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ama kweli wahenga walisema kwenye Miti hakuna wajenzi, sasa ndio naanza kutambua kuwa waliona mbali, nasikitika sana kuona waliondoka bila kutuachia namba za simu wala sanduku la posta huenda tungali wauliza mawili matatu nakufaidi zaidi.

  Nalazimika useyasema hayo mara baada ya kupata wazo la kufanya kautafiti kafupi hapahapa ndani ya JF hasa katika Jukwaa la Elimu (Education Forum). NInachojua ni kwamba founders wa JF waliona mbali sana na pia walikuwa na umakini na Ubora mkubwa sana katika kutengeneza hii Forum (JF) haya unaweza kuyaona katika muundo mzima na utaratibu wake katika shughuli za kila siku za JF. Kimbembe kinakuja pale members wanapo anza shughuli zao ndani JF.

  Ni ukweli kila mtu yupo huru katika kuchangia maada yoyote ile katika jukwaa analoona linamvutia, hilo mimi sina tatizo nayo, tatizo linakuja pale panapohitaji kupewa kipaumbele.

  Ikumbukwe kuwa, katika nchi inayohitaji kuendelea kama Tanzani, ni jambo lisio na kificho kwamba Elimu ni mojawapo ya jambo muhimu kabisa kuzingatiwa hasa ukichukulia kuwa Ujinga ni moja wapo ya adui mkubwa wa taifa letu na Elimu ndio tiba sahihi ya maradhi haya ya Ujinga. Kwa kuzingatia hayo ndipo nilipopata wazo la kuangalia mitazamo ya watu katika Taifa juu ya umakini na Juhudi za makusudi za mmoja mmoja katika kupambana na adui huyu Ujinga, kwa kuanza ni kaanza ndani kwangu (ndani ya JF the Home of Great Thinkers) mmh, nakuambia...! Kimbembe...!!

  Nilichokiona ni kitu rahisi sana lakini kikanipa mashaka na ndipo nilipoona umuhimu wa kuandika post hii ili tupate kuchangia na yeyote yule atakaye pata nafasi au bahati ya ku-view hii post.

  Nadharia
  Kinadharia, katika hali tete kama tuliyonayo ndani ya nchi yetu teule ya Tanzania, ili tupate kujikwamua ilikuwa ni lazima kuwekeza katika Elimu, jambo ambalo JF founders waliliona na katika hatua za makusudi kabisa za kulikabili ndipo walipoanzisha jukwaa la Elimu (Education Forum)

  Wajibu na Kujitambua
  Ilikuwa ni wajibu wa kila mtu anayependa mabadilko ya kweli kuchukua hatua za makusudi za kubambana na adui huyu Ujinga kama ambavyo hayati baba wa taifa Mwl. J.K. Nyerere alivyo chukua hatua na kulitangaza kuwa Ujinga ni moja ya janga la kitaifa. Hivyo katika hali ya kawaida kwa watu makini na wenye ufahamu na nia thabiti ya kulitokaomeza hili lazima kungekuwepo na juhudi za hapa na pale katika kuhakikisha tunajaribu kama sio tunafanikiwa katika kulitokomeza hili. Hivyo kutokana na hayo yote utakubaliana na mimi kwamba basi jukwaa hili la Elimu ndio jukwaa kuu kuliko yote kutokana na umuhimu mkubwa na nafasi lililonalo katika kuisaidia Tanzania katika kumtokomeza adui huyu Ujinga

  Observations
  Ukifungua jukwaa la Elimu utakuta kuna wastani wa thread 2 mpaka 3 katika wiki nzima, mbali na hayo katika kila thread kuna wastani wa watu 3 mpaka 5 kuichangia thread husika katika bases ya wiki, pia kuna wastani wa watu 37 mpaka 64 wanao-view thread husika katika wiki nzima. Ulinganifu mwingine waweza fanyika katika wastani huu hapa chini mpaka usiku wa jana 17/06/2010

  Forum Post Celebrities Forum 30,999 Mahusiano na Mapenzi 96,025 Habari na Hoja 117,353 mchanganyiko Elimu 12,175

  Kinacho nisumbua mwenzenu hivi kweli hii ni jamii ya watu makini kwelikweli?????? Are we really serious??
  Please advaice......
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jf tupo makini sana,suala la elimu ni muhimu sana kwa nchi masikini kama Tz,ndugu yangu tutachangia nini wakati hakuna anayekusikiliza?secta ya elimu imetawaliwa na wanasiasa kiasi kwamba imepoteza maana,ni sehemu muhimu sana lkn ndo sehemu ambayo mishahara yao ipo chini kuliko secta nyingine, mfano sasa hivi prof akistaafu kiinua mgongo chake ni kidogo kulinganganisha na mbunge anaenda kupiga umbea pale bungeni kwa miaka mitano,
   
 3. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hii ni mada nzuri sana, Kweli Elimu ni mhimu sn.ktk kila nyanja ya maisha.Kwa sehemu kubwa jamii yetu hatuko makini sana katika mambo mengi ya msingi.Zaidi tunatilia maanani mambo ambayo sio ya msingi sana.Hili ni tatizo kubwa sn ktk jamii yetu.Sie wote tumekuwa ni watu wa kulaumu tu,kulalamika tu,lkn hatuchukui hatua yeyote ya kuleta Mageuzi ktk Mifumo yetu ya kijamii,kisiasa,kiuchumi na kiutamadumi.

  Mimi naona ni vema mageuzi yaanzia kwa mtu mmoja mmoja kisha jamii nzima itabadirika.Pia Serikari nayo ijitaidi kuunga mkono juhudi za raia wake iboreshe mazingira ya upatikanaji wa huduma mbalimbali za msingi.Make SERIKARI ndiye BABA KATIKA FAMILIA.Baba akilegalega mambo yote hukwama pia.
   
 4. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa ndugu yangu, siasa imekuwa na nguvu kuliko utenda, pia viongozi wa kisecta wanachukua siasa kama kichaka cha kujifichia. Imekuwa ni jambo la kawaida mtu aliyepewa dhamana au madaraka anakuwa mbabaishaji badala ya kuwa mtendaji kamili. Lakini pamoja na haya yote ni vizuri tukaielewa nafasi yetu sisi kama watanzania katika jamii.

  Ndugu yangu MIke 1234, pamoja na ukweli kuwa hatusikilizwi lakini hicho siyo kigezo cha kutufanya kuamua kukaa kimya katika masuala nyeti kama haya. Mfano, Tanzania inakosa mitaala ya kueleweka katika mashule, mfano kwa kipindi kifupi tu cha miaka 7 iliyopita mitaala katika mashule yetu imebadilika kwa zaidi ya mara 3, nilini tutatengemaa kama hatuna misimamo katika mambo nyeti kama haya!? Nafasi ya watanzania ipo wapi katika hili!?

  Ikumbukwe kuwa kitu kikubwa ni nafasi chache tunazozipata au tulizonazo sisi watanzania nashindwa kuzitumia. Mfano mzuri ni huu, hadi sasa ninapoandika post hii, tayari hii thread imeshakuwa viewed na watu 65 lakini ni replies 2 ndio zimeonekana, na hapo ndio tatizo lilipo. Naomba nieleweke kuwa sio nalaumu ila hiki ndio kiini kabisa cha kuweka post hii hapa. Watanzania kushindwa kuwajibika katika mambo muhimu na nyeti lakini wapo tayari kupoteza nguvu na muda katika mambo yasiyo na kipaumbele wala tija sanifu. Kwanini!!!!!?
   
 5. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Niukweli mtupu huu.
  Lakini kwa ufahamu wangu mimi, jambo lolote lile hupewa kipaumbele sio tu kutokana na umuhimu wake, bali pia kutokana na Misukumo, Mashinikizo, Kero na na hata wakati fulani migomo kutoka pande nyingine.

  Hivyo kama nia ya dhati pamoja na ufahamu vitakuwepo ni lazima mabadiliko yaje taka usitake, ila hofu yangu kuu ni je watanzania wanafahamu kweli ni nini nafasi yao katika maendeleo ya taifa.....!?
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Contradiction tayari. Kabla hata sijafika Kimara hapo na kutoka nje ya mji, safari haijaanza vizuri tairi lishaingia bonge la pancha, the train of thought is incoherently dishonest if not an outight fabricated modesty sprinkled with undumilakuwili.

  Watu hapa kwa longolongo bwana.

  Either una kipaumbele sehemu fulani ambacho ungependa watu wakione hivyo, au unaheshimu uhuru wa kila mtu kuchangia sehemu anayotaka mwenyewe na huwasukumii watu wengine kipaumbele chako. Ukishaanza kuwaambia watu tu "this is better than this, and you guys should really concentrate on this" huwezi kusema unaheshimu uhuru wa watu kuchangia watakavyo, in fact utakuwa una impose your way of thinking over theirs, and this imposition can never attain a respectful level of conduct, at least to some of us who don't like condescension, especially if it is veiled under the garb of fake modesty and written over the disclaimer of understanding the freedom of individuals to participate as they wish.

  Sikatai kwamba unaweza kuwa na point kwamba watu hawachangii sehemu zinazotakiwa.Ninachosema ni kwamba, huwezi kuwafanya watu hapa kama watoto wadogo, kwamba "I will lecture you guys on what to do, and in that very lecture I will also tell you that I respect the freedom of every individual to do as they wish". If you understand this freedom, then why are you lecturing people who according to this freedom have done nothing wrong and are just enjoying their right of expression?

  Huwezi kuwa unaheshimu uhuru wa watu kuchangia wanachotaka wenyewe, halafu hapo hapo ukawa unawaingilia uhuru wao kwa ku push agenda yako kwa madai kwamba kuna sehemu zina kipaumbele.

  Ni sawa na scenario mmeenda kula wawili, halafu mmepewa menu, halafu unamwambia mwenzako, chagua chochote unachotaka, lakini ningependa uchague hiki. Hapo umempa uhuru wa kuchagua au hujampa?

  Kama unataka kuwatandika watu bakora kwamba hawafuatilii mambo unayoyaona kipaumbele, wewe watandike bar-abara tu, ukishaanza kuwa wishywashy kuhusu political correctness ya kuanza kusema "naheshimu uhuru wa mtu kuamua cha kuchangia lakini kipaumbele kiwe hiki" una ji contradict, kwa sababu kipaumbele chako si lazima kiwe kipaumbele cha kila mtu.

  Kwa hiyo kama unataka kusema watu si wasomi, sema tu, wala haina haja ya kuwa apologetic, kuuma na kupuliza, kusema unaheshimu uhuru wa watu kuchangia watakavyo, si kweli, ni unafiki.Ungekuwa kweli unaheshimu uhuru wa watu kuchangia wanavyotaka wala usingekerwa na watu kutochangia sehemu fulani, si unaheshimu uhuru wa watu bwana?

  Huwezi kuheshimu uhuru wa watu kinusunusu, either unaheshimu au huheshimu.It is all or nothing.

  Hatutaki contradictions, on the one hjand you are pretending to be holier than thou, on the other unataka kujiwekea insurance policy kutoka kwa watu watakaokusema kwamba unaingilia free speech na uhuru wa watu.

  You cannot eat your cake and still have it too, it is against the laws of nature.

  Inasikitisha kuona hata wale Mafarisayo wa kuinadi elimu hawako makini katika kitu kidogo kama hiki.
   
 7. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu uhuru unaheshimiwa kwa kumpa mtu uwezo wa kufanya kile anachokitaka bila kuvunja sheria, lakini kuheshimu huku hakukufanyi ushindwe kumshauri mtu au kumuelekeza juu ya umuhimu wa jambo fulani eti kwa kuogopa kuuingilia uhuru alionao. Hapa naona umechanganya mambo mawili kwa wakati mmoja.

  Naomba tufahamu kwamba siyo kweli kwamba nawalecture watu juu ya nini cha kufanya wala si kweli kuwa nawafanya watu ni watoto wadogo... La hasha! ninachofanya hapa ni kuwakumbusha watu kuwa katika jamii yoyote ile lazima kuna mambo yenye kipaumbele na umuhimu mkubwa na pia yapo ambayo kipaumbele chake si kikubwa na muhimu kivile. Hivyo nachukua jukumu la kuwakumbusha wenzangu juu ya mambo ambayo naona kwa waziwazi, tena kwa mifano kuwa katika hili hakika tunapotea na katika lile hatuendi sawa, hili laweza kufanyika bila kugusa uhuru wa mtu katika hali yoyote ile.

  Uhuru pekeyake bila maarifa ya namna ya kuutumia uhuru husika haitoshi, kama haitoshi sisi tunafanyaaje? Je, hatutajitoa muhanga katika kutafuta ama kuleta hayo maarifa ili yapate kutumika katika kuboresha kile tunachokiona kuwa hakiendi sawa? Kama hivi ndivyo, basi tunahitaji pia kukumbushwa juu ya mambo muhimu yanayohitajika kufanyika ndani ya uhuru tuliona nao. Katika hili hatuwaiti wale wanaotukumbusha au kutupa hayo maarifa kuwa ni wanafiki eti kwa minajili ya kwamba wanaheshimu at the same time wanaingilia uhuru wa watu.

  Hata huu unaoutumia wewe na mimi ni mojawapo ya ule uhuru tunaozungumzia hivyo si busara kujiweka nje ya stream hiyo iliupate kuzungumza bali ni busara kuwa ndani ya stream husika ili kukabiliana na kile kinachojiri ndani yake.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Huwezi kusema unaheshimu uhuru wa watu kufanya wanachotaka, halafu hapo hapo wakifanya wanachotaka ukaanza kuwaingilia na kuweka agenda zako.

  Kama unataka kuwaingilia na kuweka agenda zako, usiseme unaheshimu uhuru wa watu kufanya wanachotaka.

  Kama unaheshimu uhuru wa watu kufanya wanachotaka, huwezi kuwaingilia watu wakiamua kufanya wanachotaka.

  Huwezi kuchanganya viwili hivi pamoja, utakuwa mtovu wa uadilifu.
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sijui hii ni changamoto lakini sijui kwa mujibu wa mtoa mada SCOPE ya elimu yeye kwake ni nini. Binafsi habari za isiasa ,michezo,Afya, Mapenzi ,etc zote zinatumika na wachangaijai kutoa maoni ushauri, chanagamoto, taarifa za habari mbali mbali. Hizi thread zote zinatoa elimu.

  Ukumbuke kuwa JF ina watu wa TAALUMA, FANI UMRI , etc tofauti. Kwa hiyo UHITAJI na aina ya habari za Elimu kwa mwanafunzi aliyechuo au shule una tofauti na mahitajai na aina ye ELIMU anayohitaji mfanyabiashara au Mwanasheria anayefanya kazi.

  Vile Vile Kuna msemo katika fani ya IT unasema INFORMATION TO ONE PERSON CAN BE DATA TO ANOTHER PERSON.

  Kwa hiyo kifupi ni kuwa JF yote ni jukwaa la ELIMU.
   
 10. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unaweza kuwa sawa, endapo tu utakuwa umeamua kuweka mambo mengine yote constant, otherwise utakuwa hujaelewa kiini chake. Kinachozungumziwa. Hapa ni suala zima la umuhimu wa Elimu katika kuharakisha maendeleo ya kitaifa, Je watanzania tunatumia fursa tulizonazo ipasavyo katika hili?

  Ndugu yangu kama utakuwa umeangalia na kufikiria vizuri juu ya matatizo mengi yanayolikumaba taifa kwa sasa yanasukumwa mbele na ukosefu wa Elimu, Maarifa ama Uelewa mdogo katika kuchanganua mambo na mambo mengi yanayoendana na hayo, kitu kinachotokana na kutokuwa na mfumo au utaratibu mzuri toka awali juu ya Elimu na misingi yake katika taifa letu. Hilo ni jambo muhimu sana tena linalohitaji kupewa kipaumbele kama kweli tunahitaji mabadiliko, sasa inapokuja sehemu iliyosheheni watu wa matabaka mbalimbali kama hapa JF tulitegemea michango mingi sana kama njia mojawapo ya kupambana na hili.

  Haishangazi sana kuona watu wengi wakiwa na mtazamo kama wako kuwa, kwakuwa hii ni EDUCATION FORUM basi huu ni lazima utakuwa uwanja wa wanafunzi, kama inavyojionesha katika arguments zako. Hili unalipata kutoka katika comment zako, lakini ukweli unabaki kuwa huu ni mtazamo hasi. Hii ni Forum yenye uwezo mkubwa na wa haraka katika kusambaza elimu kwa mapana na marefu yake. Hilo linatokana na uwepo wa watu wengi tena wenye elimu, fani, taaluma, itikadi, mitazamo mbalimbali n.k hivyo kutokutumika ipasavyo ni upotevu wa rasilimali fulani fulani.

  Ukweli utabakia palepale kuwa JF ina watu wenye TAALUMA, FANI, UMRI mbalimbali hivyo kwangu mimi hivi ni vitu ambavyo kama vikitumika ipasavyo vinauwezo mkubwa sana katika kuchangia maendeleo ya taifa letu kwa haraka. Kinyume na matarajio ya wengi taaluma, fani, Umri na vinginevyo havionekani kutumika, hapa ndio kiini cha tatizo kilipo. Kama hatutasema haya mlitaka tuseme yapi? Je tushangilie daktari aliyeacha mguu na kupasua kichwa? Au yule aliyeacha mama mjamzito ajifungulie nje huku njia mbadala za kumsaidia zikwepo? Tusemenini basi, tukae tuu na kulaumu viongozi kwa ufisadi na uzembe wao... au turudi humu tuambizane juu ya uwezo wa ELIMU katika ubora wa maisha yetu na watoto wetu hapo kesho?

  Ninachokiona hapa haijalishi wewe ni nani, Mfanyabiashara, Mwanasheria, Mwanataaluma au raia, wote kama hatuhitaji kupokea pasi tunahitaji kutoa mchango wetu katika Forum hii kutokana na kile tunachokiita ELIMU NI MSINGI WA MAISHA.
   
 11. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu, hayo maneno ndiyo yanayokufanya unashindwa kuielewa maada. Labda niombe msaada wa ufafanuzi juu ya neno KUINGILIA ama KUWAINGILIA. Unaweza ukawa huru katika njia potofu ama ukawa potofu katika njia huru, hivi vyote viwili havina maana sawa. Utakapo mwambia mtu wewe ni mtu potofu katika njia huru haina maana kuwa umemuingilia katika uhuru wake, maana kuingilia uhuru wa mtu ni kutaka kumkataza mtu pasipo haki kufanya kile kilicho haki. nadhani sasa KIRANGA utakuwa umenipata vizuri. Nafurahi pia kuwa kupitia haya wengi wanaona kile kilichojificha.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Usitake kuleta semantics hapa.

  Either sema hujali swala la watu kuwa na uhuru wa kufanya chochote kama wanavyoona sawa within the established code of conduct, kwamba unataka ku impose views zako bila apology. Unataka kutu condescend.

  Au sema unajali uhuru wa watu kujiamulia wapi wachangie, na uombe radhi kwa kuwafanya watu watoto wadogo na kuanza kuwapangia nini ni cha muhimu kuchangia.

  Huwezi kuchukua positions hizi mbili kwa mkupuo mmoja, ni sawa na kula tunda lako halafu utegemee liwepo pale pale. Kamwe haiwezekani.

  Hapa kuna label wameweka juu "Where We Dare To Talk Openly" kama unaona watu wanachemka na hawajachangia mjadala muhimu kwako, wewe wablast tu, usianze kuwablast halafu katika kuwablast ukaleta vimchongo vya phoniness na fake modesty hapa, wengine hatutaki fake modesty tutakubalasa.

  La kama unataka modesty ya kusema "najua kila mtu ana uhuru wa kuamua cha kuchangia anavyotaka" then kaa na modesty hiyo, jua hivyo, heshimu uhuru huo, usianze kujifanya unaujua uhuru huu, unaukubali kwa mkono wa kulia, halafu unataka kuuondoa kwa mkono wa kushoto na kuanza kutu lecture. We will see you for what you are, a manipulating person.

  Acha hizo.

  Now which is it, unaheshimu uhuru wa watu kuamua nini wachangie au huheshimu?
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mdau wewe ulitaka kifanyike nini? Maana sijakusoma vyema.
   
Loading...