WADAU HUU UTARATIBU WA PF3 KWANINI HAUBADILISHWI

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,396
1,784
PF3 ni form iliyojazwa polisi ili mtu aliyepata majeraha au kuumia aweze kupata matibabu hospitali.

Kuna wakati mwingine mtu anapata majeraha yanayohitaji huduma ya afya ya haraka sana,lakini mtu anapelekwa hospitali ili kuokoa maisha yake linakuja suala la pf3.Mtu huyo hawezi kupata matibabu hadi pf3 ipelekwe...Huu utaratibu kwanini usibadilishwe kwamba mtu aweze kupata matibabu hasa kwa walio na hali mbaya zaidi then pf3 ifuate,au kuna ugumu ambao mimi siuelewi maana kuna watu wanaokufa wakisubiri hizo pf3.

Naombeni sababu za huu utaratibu kutobadilishwa
 
Hio sio tz pekee ake nchi nyingi zina utaratibu huohuo sema ulioboreshwa
Utaratib huu ni muhimu hasa kwa polisi kupata taarifa za matukio mbalimbali ambazo kama isingekua pf3 wasingepata
Kubwa ni kwamba kuwe na utaratibu mzuri na wa haraka ili watu wasipoteze maisha
 
hata jambazi akija kwako kukupora vitu ukamuwahi na panga, ujue hatapata matibabu bila kuonyesha pf3, ndio maana majambazi wengi huwa wanaamua kujitibia majumbani kwao. pasingekuwapo hiyo pf3 ujue wala polisi wasingempata, ila kwa pf3 akijipeleka tu polisi anaweza kukamatwa. haijalenga watu wema, imelenga watu wahalifu. hivyo tutoe ushirikiano.

hata hivyo, nafikiri kuna umuhimu kuweka exceptions kwa waliopata ajali zinazojulikana, labda wafanyiwe njia ya uharakishaji zaidi pf3 wapate, ila lazima wawe nazo kwasababu wahalifu wengine watatibiwa wakisingizia ajali kumbe wamerushiana risasi au mapanga na raia/askari.
 
Ndio nakubaliana na ww ila there is no way ya kukataa pf3 labda iboreshwe huduma yake
 
Hio sio tz pekee ake nchi nyingi zina utaratibu huohuo sema ulioboreshwa
Utaratib huu ni muhimu hasa kwa polisi kupata taarifa za matukio mbalimbali ambazo kama isingekua pf3 wasingepata
Kubwa ni kwamba kuwe na utaratibu mzuri na wa haraka ili watu wasipoteze maisha
Hapa sio kuutoa bali kuuboresha ili huduma ya kupatiwa matibabu iwe inafanyika wakati huohuo police wakiwa wanataarifiwa kutoa pf3 na hapa ni kwa wale majeruhi walio katika hali mbaya,hii itasaidia kuokoa maisha ya watu mfano kuna taarifa ilitolewa kuwa hata yule mfanyakazi wa zantel aliyepigwa risasi juzi hadi anafikishwa hospital alikuwa hai ila matibabu hayakufanyika hadi pf3 ipatikane.Je haiwezekani matibabu yakaanza huku taratibu za pf3 zikiwa zinashughulikiwa?
 
Hio sio tz pekee ake nchi nyingi zina utaratibu huohuo sema ulioboreshwa
Utaratib huu ni muhimu hasa kwa polisi kupata taarifa za matukio mbalimbali ambazo kama isingekua pf3 wasingepata
Kubwa ni kwamba kuwe na utaratibu mzuri na wa haraka ili watu wasipoteze maisha

Utaratibu huu ni mbovu sana na haufai katika carne ya sasa, hasa panapokuwa na mgonjwa ambaye hali aliyonayo inaweza kumpotezea maisha yake haraka. Mfano mtu amepata ajali na damu inatoka kwa wingi. Kuna kile kitu inaitwa "The Golden Hour" ambayo ikizingatiwa mgongwa anaweza kuokoa maisha yake.

Option ambayo inaweza kufanyika ni kuweka dawati la PF3 kwenye hospitali, ili wagonjwa wasipotezewe muda mwingi wakiwa polisi wanasubiri PF3.
Maisha ya mwanadamu ni muhimu zaidi kuliko PF3, ambayo inaweza ikatafutiwa utaratibu mwingine.
 
Hapo waweke huduma za kwanza kwenye vituo vya polisi kwa ajili ya hizo PF3..
Huduma ya kwanza,mfano mgonjwa anatoka damu sana au tuchukulie hali ya Alphonce Mawazo jinsi ilivyokuwa,je huduma ya kwanza itaweza kusaidia kwa namna ile?
 
PF3 ni form iliyojazwa polisi ili mtu aliyepata majeraha au kuumia aweze kupata matibabu hospitali.

Kuna wakati mwingine mtu anapata majeraha yanayohitaji huduma ya afya ya haraka sana,lakini mtu anapelekwa hospitali ili kuokoa maisha yake linakuja suala la pf3.Mtu huyo hawezi kupata matibabu hadi pf3 ipelekwe...Huu utaratibu kwanini usibadilishwe kwamba mtu aweze kupata matibabu hasa kwa walio na hali mbaya zaidi then pf3 ifuate,au kuna ugumu ambao mimi siuelewi maana kuna watu wanaokufa wakisubiri hizo pf3.

Naombeni sababu za huu utaratibu kutobadilishwa
PF3 iwepo ila polisi wafungue dirisha hospitali ili watoe pf3 hapohapo.hii ndio solution pekee sababu pf3 haiwezi ondolewa inasaidia.
 
Sidhani kuwa hilo linawezekana kwasababu police wetu ni wachache sana na haya matukio si kwamba yapo mara kwa mara.

Hivi hospital i apokea mtu yupo mahututi kwa majeraha kukiwepo na sheria inayoitaka hospital kuhudumia wale majeruhi walio katika hatari ya kupoteza maisha wakati polisi wakiwa wanakuja kuandika hiyo pf3 kutakuwa na tatizo maana hata kama ni jambazi naye ana haki ya kupata matibabu ili aweze kupona na baada ya kuokoa maisha yake hayo mengine ni ya polisi.
 
Back
Top Bottom