Shirika la majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) limedhamiria kuwafikisha Mahakamani wadaiwa sugu wa Ankara za Maji hususani waliolimbikiza madeni ya nyuma kuanzia kipindi cha mwezi mmoja na kuendelea.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo hivi karibuni imesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kubaini kipindi cha mwaka mpya wa serikali kinaanza huku fedha na madeni mengi yakiwa mikononi mwa wananchi.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa Dawasco imetoa muda wa siku kumi kuanzia tarehe 01 mwezi wa sita hadi 10 mwezi wa sita kwa wadaiwa wote ikiwemo watu binafsi, Taasisi za serikali, Taasisi binafsi na mashirika ya umma kuwa wamelipa madeni yao.
Wamewaomba wananchi kuwaunga mkono katika zoezi hilo na wenye maswali kupiga huduma kwa wateja dawasco 080011006400 (Bure)