Wadaiwa Sugu HESLB msako utakuwa hivi

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,381
1,760
Grace period again!

=====

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imewapa siku 30 kuanzia Novemba 14, mwaka huu wadaiwa wake sugu 154,000 kurejesha fedha wanazodaiwa.

Vinginevyo, imesema watakamatwa na kulazimishwa kulipa madeni na gharama za kuwasaka.

Kwa mujibu wa bodi hiyo, wadaiwa wote wanaoangukia katika mkumbo huo, watatangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari Novemba 13, siku moja kabla ya kuanza kwa notisi hiyo ya siku 30, isipokuwa kwa wale ambao watakuwa tayari wamelipa.

Akizungumza na gazeti la Habari Leo ijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul Razaq Badru alisema wadaiwa hao ni wa kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa ambao madeni yao yameiva.

Alisema hadi sasa serikali inadai Sh trilioni 2.6 kutoka kwa wadaiwa hao ambao walikopeshwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu lakini hawajarejesha mikopo hiyo na hivyo kuleta changamoto kwa waombaji wapya.

“Bodi itatangaza majina ya wadaiwa sugu wa kuanzia mwaka huo ambao madeni yao yameiva, majina yao tutayaweka hadharani Novemba 13, mwaka huu baada ya hapo tutawapa siku 30 kulipa, baada ya muda huo, hatua za kisheria zitachukuliwa na wahusika watalipia gharama za kuwasaka,” alisema Badru.

Alisema wadaiwa hao sugu wanapaswa kukumbuka kuwa kutolipa madeni yao ni kuvunja Mkataba na Sheria ya Bodi hiyo Namba 9 ya mwaka 2004, 19 (1).

Sheria hiyo ya mwaka 2004 Kipengele cha pili kinasema mdaiwa atapewa penalti ya asilimia tano juu ya ile asilimia tano iliyokuwa ikitozwa kabla, kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo. Aidha, kipengele cha tatu kinasema mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni lililoingiwa na bodi.

Vipengele vingine kwenye sheria hiyo vinasema mdaiwa atawekwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote.

Pia mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa serikali au udahili wa masomo ya juu kwenye vyuo vyovyote ndani na nje ya nchi. Kadhalika, maelezo yao yatapelekwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kitengo cha Uhamiaji na balozi zote ambako watakataliwa safari zozote za kwenda nje ya nchi.

Badru alisema awali selikali ilitoa mikopo hiyo kwa wanafunzi, kwa kuweka bayana kwamba fedha walizopewa ni mikopo na wala si msaada au ruzuku, hivyo zinapaswa kujereshwa mara baada ya mdaiwa kuhitimu masomo yake; au pindi atakapositisha masomo yake kwa sababu mbalimbali.

Source: Bongo5
 
Waache mbwembwe zao...Watoe majina ya wadaiwa kisha wawape muda wa kulipa.....Habari za ndani zinasema hawana database ya wadaiwa wao so wanaishia kupiga kelele kama toothless dogs.

By the way.....Hivi waliosoma kuanzia 1961 mpaka 1993 walilipiwa pesa na wazazi wao?...Serikali ilikuwa haisomeshi hao watu? Kama walisomeshwa na serikali kwanini walipaji iwe from 1994? Au hao walikopeshwa na serikali ya tanganyika na hawa wa 1994 wamekopeshwa na serikali ya tanzania? Double standards at works.

Swali lingine la kizushi...Hivi ukikopa mwaka 94 sheria ya mkopo ikabadilishwa 2004 na mie mkataba wangu na wewe tulikuwa na terms zetu 1994 wewe unajibadilishia na kugeuza grant kuwa loan bila kunishirikisha ...Serikali haioni kuna kosa la kisheria hapo?
 
WAACHE MBWEMBWE ZAO...WATOE MAJINA YA WADAIWA KISHA WAWAPE MUDA WA KULIPA.....HABARI ZA NDANI ZINASEMA HAWANA DATABASE YA WADAIWA WAO SO WANAISHIA KUPIGA KELELE KAMA TOOTHLESS DOGS.

BY THE WAY.....HIVI WALIOSOMA KUANZIA 1961 MPAKA 1993 WALILIPIWA PESA NA WAZAZI WAO?...SERIKALI ILIKUWA HAISOMESHI HAO WATU? KAMA WALISOMESHWA NA SERIKALI KWANINI WALIPAJI IWE FROM 1994? AU HAO WALIKOPESHWA NA SERIKALI YA TANGANYIKA NA HAWA WA 1994 WAMEKOPESHWA NA SERIKALI YA TANZANIA? DOUBLE STANDARDS AT WORKS.
SWALI LINGINE LA KIZUSHI...HIVI UKIKOPA MWAKA 94 SHERIA YA MKOPO IKABADILISHWA 2004 NA MIE MKATABA WANGU NA WEWE TULIKUWA NA TERMS ZETU 1994 WEWE UNAJIBADILISHIA NA KUGEUZA GRANT KUWA LOAN BILA KUNISHIRIKISHA ...SERIKALI HAIONI KUNA KOSA LA KISHERIA HAPO?
Tena wengi wao waliodoma miaka hiyo ya nyuma ndio waliopata kazi nzuri serikalini na mashirika yake na pia ndo viongozi wakubwa katika nchi hii,ilibidi walipe wao kwanza kuonesha kama mfano.

Sidhani kama kuna mtu alimaliza miaka ya 1996 kurudi nyuma then hakupata kazi nzuri serikalini.
 
Ndo utajitokeza au unasubiri kuona jina lako kwanza,lisipokuwepo basi.

hakuna mdaiwa anayejipeleka na hasa kipindi hiki pesa ya kutafuta kwa tochi...wao wataje majina(kama wanayo kweli hayo ya 1994 kisha wawe tayari ku-defend madai yao ikiwamo sehemu niliyotia saini kuwa nimeomba mkopo wa kiasi fulani na waonyeje walinipatia hizo pesa kwa awamu ngapi na account ipi....waache ubabaishaji wawe serious.
 
WAACHE MBWEMBWE ZAO...WATOE MAJINA YA WADAIWA KISHA WAWAPE MUDA WA KULIPA.....HABARI ZA NDANI ZINASEMA HAWANA DATABASE YA WADAIWA WAO SO WANAISHIA KUPIGA KELELE KAMA TOOTHLESS DOGS.

BY THE WAY.....HIVI WALIOSOMA KUANZIA 1961 MPAKA 1993 WALILIPIWA PESA NA WAZAZI WAO?...SERIKALI ILIKUWA HAISOMESHI HAO WATU? KAMA WALISOMESHWA NA SERIKALI KWANINI WALIPAJI IWE FROM 1994? AU HAO WALIKOPESHWA NA SERIKALI YA TANGANYIKA NA HAWA WA 1994 WAMEKOPESHWA NA SERIKALI YA TANZANIA? DOUBLE STANDARDS AT WORKS.
SWALI LINGINE LA KIZUSHI...HIVI UKIKOPA MWAKA 94 SHERIA YA MKOPO IKABADILISHWA 2004 NA MIE MKATABA WANGU NA WEWE TULIKUWA NA TERMS ZETU 1994 WEWE UNAJIBADILISHIA NA KUGEUZA GRANT KUWA LOAN BILA KUNISHIRIKISHA ...SERIKALI HAIONI KUNA KOSA LA KISHERIA HAPO?
UTAKUNA UNA DENI LOAN BOARD SIO BURE, KALIPE ILI NA WENGINE WAKOPE.UJANJA UJANJA MWINGIII UTAKUTOKEA PUANI
 
Nauliza wanadai ada tu au pamoja pia na accomodotion meals allowance
 
Tena wengi wao waliodoma miaka hiyo ya nyuma ndio waliopata kazi nzuri serikalini na mashirika yake na pia ndo viongozi wakubwa katika nchi hii,ilibidi walipe wao kwanza kuonesha kama mfano.

Sidhani kama kuna mtu alimaliza miaka ya 1996 kurudi nyuma then hakupata kazi nzuri serikalini.

hii mizee yetu inayofanya maamuzi serikalini ni mihuni ya kutupa....ilivyovuka mto ikabomoa draja alilojenga nyerere ili watanzania wote tunaokuja nyuma yao tusivuke kwenda waliko. HAKUNA MTANZANIA ALIYESO MA KWA PESA YA BABA YAKE KABLA YA MWAKA 1994...wooote mpaka kina warioba na sitta walisoma chuo kikuu kwa hela ya mwalimu ambayo ni kodi ya baba na babu zetu...hawajalipishwa iweje sie leo tulipishwe kama hatulipii kodi?
WAACHE UHUNI...KAMA ELIMU ILIKUWA BURE NA IENDELEE KUWA BURE NA SERIKALI IWALIPIE WATU WAKE KUSOMA...NA KAMA ELIMU NI YA KULIPIA TUANZE MARA MOJA KILA MTU ALIPIE KUANZIA PRIMARY NDIO TUTAJUA KODI YETU KAZI YAKE NI NINI KAMA SIO KUTUPA ELIMU NA MATIBABU WANANCHI WAKE....
 
UTAKUNA UNA DENI LOAN BOARD SIO BURE, KALIPE ILI NA WENGINE WAKOPE.UJANJA UJANJA MWINGIII UTAKUTOKEA PUANI

KAMA WANANIDAI WASEME WANACHONIDAI...DAWA YA DENI KULIPA ILA UWE NA USHAHIDI KUWA UNANIDAI..TENA WA MAANDISHI.
 
Mbona simple, watangaze tu kuwa wote waliosoma kuanzia 1994 mpaka leo wahakikiwe kama wamelipa mikopo na wapewe stakabadhi ili waendelee na ajira zao wasiofanya hivyo Serikali iwatimue makazini hata kama wapo sekta binafsi, fedha ikipatikana watoto wetu wote wapate mikopo mwakani bila kujali fani au shule aliyosoma ili mradi amefaulu
 
KAMA WANANIDAI WASEME WANACHONIDAI...DAWA YA DENI KULIPA ILA UWE NA USHAHIDI KUWA UNANIDAI..TENA WA MAANDISHI.
Mimi binafsi nashangaa sana wanapotaka tulipe loan wakati sisi tunaofanya kazi private sectors hiyo PAYE tu ninayokatwa unakaa chini utoe machozi then wanataka nilipe na hela niliyopewa chuo loooooh
 
  • Hivi ni kwanini HESBL inadai Interest kwenye mikopo ya wanafunzi wakati zile pesa za mkopo sio za biashara?
  • Kwanini wanadai adminstration charge wakati wanaendesha board kwa fedha za serikali?
  • Hivi ni kwann wadai pesa kwa watu tunaolitumikia taifa huku tukikatwa kodi (PAYE) kwenye mishahara yetu.
Dah hawa ndo watu wanafanya tujute kuzaliwa na kuishi Tanzania.
 
Mtu ana degree, kazi hana, full kubangaiza alafu unamuongezea stress za kulipa mkopo si kumtia uchizi, mwengine ana kazi lkn mshahara hauvuki laki tano, ukitoa kodi na hiyo ela ya bodi, utajikuta mwezi mzima umelifanyia kazi tumbo, ktk hili serikali inatakiwa kuwa makini, watu wengi wako mtaa wanasota kila wanaposhika panateleza, wajaribu kutumia busara ktk hili jambo.
 
UTAKUNA UNA DENI LOAN BOARD SIO BURE, KALIPE ILI NA WENGINE WAKOPE.UJANJA UJANJA MWINGIII UTAKUTOKEA PUANI
Nijibu maswali haya kwanza mkuu.

Je kuna mtu unayemfahamu ambaye alisoma miaka ya 1970 hadi 1993?

Ni nani aliyemaliza chuo mwaka 1670 hadi 1993 unayemfahamu ambaye amelipa deni HESLB.
 
Nauliza wanadai ada tu au pamoja pia na accomodotion meals allowance
Zote mkuu,hela yoyote uliyosaini kwa mkono wako au kama hujijui yawezekana ulisainiwa unatakiwa uirudishe ikiwemo ada,stationary,meals & accomodation,field,special facult n.k
 
Mtu ana degree, kazi hana, full kubangaiza alafu unamuongezea stress za kulipa mkopo si kumtia uchizi, mwengine ana kazi lkn mshahara hauvuki laki tano, ukitoa kodi na hiyo ela ya bodi, utajikuta mwezi mzima umelifanyia kazi tumbo, ktk hili serikali inatakiwa kuwa makini, watu wengi wako mtaa wanasota kila wanaposhika panateleza, wajaribu kutumia busara ktk hili jambo.
Mie nasubiri wasio na kazi wabugudhiwe tuone watu wanavyojifanya kama yule jamaa graduate wa Tunisia.
 
Back
Top Bottom