Wadaiwa Bodi ya Mikopo kusakwa majumbani usiku

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,140

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema kuanzia Januari mwakani itaanza kudai fedha za mikopo kwa kupita nyumba kwa nyumba, hasa muda wa usiku.

Mbali na hilo, HESLB wamesema kuwa wapo kwenye mpango wa kuzungumza na washereheshaji wa sherehe (ma-MC), hasa harusi na viongozi wa nyumba za ibada ili waweze kutumia maeneo yao kuwakumbusha wadaiwa hao walipe madeni yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru, alisema kuwa sasa ni wakati mwafaka kuhakikisha madeni yote yanalipwa kwa kutumia kila aina ya njia.

Aliwataka walionufaika na mikopo hiyo kuanza kujisalimisha wenyewe kulipa madeni yao kuepuka kusakwa majumbani na katika nyumba za ibada.

“Tumefanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kuwashirikisha washereheshaji katika shughuli mbalimbali pamoja na nyumba za ibada ili waweze kuwakumbusha wadaiwa wa bodi kurejesha mikopo na ifikapo Januari Mosi, mwakani majina na sura za wadaiwa sugu tutazichapisha gazetini.

“Si hilo tu, pia tutapita nyumba kwa nyumba nchi nzima, hasa muda wa jua linapozama ili kuweza kuwafikia wadaiwa wote ambao walipata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo. Mkopo si zawadi ni lazima ulipwe.

“Walipe ili na wengine waweze kunufaika na fursa ya mikopo. Na wale ambao watakaidi tutawafikisha mahakamani ambako watalipa gharama za uendeshaji wa kesi pamoja na deni wanalodaiwa,” alisema Badru.

Mkurugenzi huyo alisema hivi sasa wameanza utekelezaji wa marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ambapo kwa sasa wanufaika wa mkopo watalazimika kukatwa asilimia 15 badala ya asilimia nane ya awali.

Badru alisema sheria hiyo mpya imeipa meno bodi hiyo pia kuwawajibisha na kuwafikisha mahakamani waajiri endapo watashindwa kukata makato kwa waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo au kuchelewesha kuwasilisha fedha za makato hayo.

“Kwa mabadiliko haya ya sheria, mwajiri sasa ana wajibu wa kuwasilisha majina, kukata na kuwasilisha makato stahiki kutoka katika mishahara ghafi ya waajiriwa wake walionufaika na mikopo ya elimu ya juu,” alisema Badru.

Alisema kwa waajiri ambao hawatawajibika, watalipa faini isiyopungua makato hayo au kifungo cha miezi 36.

Badru alisema pia wametoa siku 14 kuhakikisha kila mwajiri anapitia kumbukumbu zake na kuangalia kiasi walichokata na kuwasilisha katika bodi hiyo kabla timu iliyoundwa kufuatilia madeni hayo haijaanza kufanya kazi.

Alitoa wito kwa waajiri na waajiriwa kuhakikisha wanakusanya kumbukumbu muhimu ili kuepusha usumbufu endapo wataajiri wadaiwa sugu wa bodi hiyo na wakakwepa kutoa taarifa zao mapema.

Alisema kuhusu wanufaika ambao hawapo kwenye mfumo rasmi na mikopo yao imeiva, watalazimika kulipa Sh 100,000 au asilimia 10 ya kipato kinachotozwa kodi kwa mwezi.

“Sheria hii imepita mikononi mwa wadau ambao wamejaribu kupunguza ukali wa maisha, ambapo kwa wanufaika ambao hawako kwenye mfumo rasmi watalazimika kulipa deni lao baada ya miaka miwili badala ya mmoja wa sasa na kwa wale ambao wana ajira wataanza kulipa mara baada ya kuajiriwa,” alisema Badru.

Sambamba na hilo, bodi hiyo imesema hadi sasa imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 140 kutoka kwa wanufaika wa mikopo iliyoiva. Awali deni lilikuwa ni Sh bilioni 300.

Mkurugenzi huyo alisema kiwango cha makusanyo ya mikopo ambayo awali yalikuwa ni Sh bilioni 2 kwa mwezi, hadi kufikia Novemba, mwaka huu yameongezeka na kufikia Sh bilioni 8 kwa mwezi.

Pia wadaiwa sugu waliojitokeza kulipa au kupunguza madeni yao wamefikia 42,700 kati ya 100,000 waliokuwa wanadaiwa awali.

“Katika kuhakikisha waajiri wanakusanya makato yetu, tumekutana na waajiri zaidi ya 10 na kuzungumza nao, ambao wengi wao walikuwa hawafahamu wajibu wao,” alisema Badru.

Kwa upande wa mwanasheria wa bodi hiyo, Luhano Lupogo, alisema mwajiri ana wajibu wa kupeleka makato ya mwajiriwa wake kwa bodi ndani ya siku 15, vinginevyo atalipa faini isiyopungua makato au kifungo cha miaka mitatu jela.

Alisema sheria hiyo ya mwaka 2004, namba 21 (2) imeanza kutumika Novemba 18, mwaka huu ambapo pia mwajiri ana wajibu wa kuwasilisha katika bodi orodha ya waajiriwa wake ambao ni wahitimu wa Stashahada au Shahada.

WANAFUNZI CHINA KUKOSA MIKOPO

Wakati huohuo, Mwandishi JOHANES RESPICHIUS anaripoti kuwa bodi hiyo imesema haitatoa mikopo kwa wanafunzi wote wa Tanzania waliofadhiliwa masomo katika nchi rafiki, ikiwamo China.

Hiyo ni kwa mujibu wa barua ya Desemba 20, mwaka huu iliyokuwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa imesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru, kwenda ubalozi wa Tanzania nchini China.

Barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Kuchelewa kwa Fedha za Malipo kwa wanafunzi wanaosoma nchini China’, ilisema kuwa bodi hiyo haikupanga mikopo kwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma China kutokana na maelekezo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

“Kupitia barua ya wizara Kumbu. Na FB.54/283/01A/82 ya Septemba 14, mwaka huu, ilielekeza wanafunzi wote watakaopata ufadhili wa masomo (scholarship) kutoka katika nchi rafiki watakuwa wanajitegemea katika kununua tiketi za ndege kwenda masomoni.

“Pia barua hiyo ilielekeza kwamba wanafunzi wanaosoma katika nchi hizo hawatanufaika na mikopo ya nyongeza ya ada (topping up loan) kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” ilieleza barua hiyo.

Ilieleza kuwa kutokana na maelekezo hayo, bodi imeshindwa kupanga mikopo kwa wanafunzi hao waliopata ‘scholarship’ kwa mwaka wa masomo 2016/17 na wale waliokuwa wakiendelea na masomo China hadi itakapopata maelekezo zaidi.

MTANZANIA lilimtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa HSELB, Badru ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala hilo.

“Siwezi kusema ndiyo ni ya kwetu au hapana kwa sababu barua hiyo sijaiona, kwanza bodi haina utaratibu wa kuweka barua kwenye mitandao ya kijamii.

“Kama ina taarifa yoyote inataka kuitoa huwa inatumia utaratibu wa kawaida wa utoaji taarifa na kama kuna umuhimu kuweka kwenye mitandao ya kijamii ndipo huweka,” alisema Badru.

Chanzo: Mtanzania
 
Kweli Tanzania imefilisika. Hivi mapato ya november vip? Nawashauri wauze ile migari ya jeshi la polisi walionunua kwa maandalizi ya uchaguzi 2015.

Wakishindwa ilo watafute mwekezaji wamkabidhi tanzania yote kwa miaka 99
 
Deni halimfungi Mtu jela, Ila katika hii awamu ya huyu Mtukufu (katika sauti ya Tundu Lissu), Jela lazima twende tu!
 
Yeah! I am still here Sasha Fierce doing my thing :):):), I have not seen you in years. I am good proceeding well with my routines. I am happy to see you and hopefully you'll stay for a little bit longer lol!

BAK Dude kumbe bado upo around?..How have you been?..Damn i haven't been here in years...
 
BAK mbona mkuu unapenda kuleta mada zinazo nitia hasira hivi?
Ni ukweli ulio wazi kuwa huko juu tumejaza mbumbumbu na serikali yetu imeishiwa fedha na mbinu kabisa kabisa. Hivi kweli mwaka mmoja tuu ndio hivi jee hiyo mingine minne hali itakuwaje? Tusishangae yale ya DRC watumishi hawana mishahara kisha askari wanaweka vizuizi barabarani kuchukua mchango wa maisha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yeah! I am still here Sasha Fierce doing my thing :):):), I have not seen you in years. I am good proceeding well with my routines. I am happy to see you and hopefully you'll stay for a little bit longer lol!

Hopefully 2017 might do miracle so i can stay....You cna't believe i even forgot my user name and password..LMAO!...So kila mtu is hear? akina Nyani Ngabu and others au watu wali-sepa na kijiji? (i love this word "sepa na kijiji"). Good to see you my friend, the coolest dude....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
....lol! labda naongeza speed ya mashetani kuifunga mitandao yote nchini Mkuu. Hatuwezi kuikimbia hali halisi ya nchi yetu iliyomfanya hata mstaafu Mwinyi ajitoe hadharani na kutamka, "Nchi inaenda kama gari bovu haina sukani"

BAK mbona mkuu unapenda kuleta mada zinazo nitia hasira hivi?
Ni ukweli ulio wazi kuwa huko juu tumejaza mbumbumbu na serikali yetu imeishiwa fedha na mbinu kabisa kabisa. Hivi kweli mwaka mmoja tuu ndio hivi jee hiyo mingine minne hali itakuwaje? Tusishangae yale ya DRC watumishi hawana mishahara kisha askari wanaweka vizuizi barabarani kuchukua mchango wa maisha.
 
BAK mbona mkuu unapenda kuleta mada zinazo nitia hasira hivi?
Ni ukweli ulio wazi kuwa huko juu tumejaza mbumbumbu na serikali yetu imeishiwa fedha na mbinu kabisa kabisa. Hivi kweli mwaka mmoja tuu ndio hivi jee hiyo mingine minne hali itakuwaje? Tusishangae yale ya DRC watumishi hawana mishahara kisha askari wanaweka vizuizi barabarani kuchukua mchango wa maisha.

Wanasema subira yavuta heri (hope nimesema sawa)...Lets wait and see its just one year. Lets not give up hope on our president and his government.
 
...lucky you that you're able to remember your pw. Nyani na wengine wengi bado wamo humu, but also we have lost few or maybe they made a decision to use new IDs. Welcome back my friend...lol! the coolest dude on JF hahahahaha I like that :):):) THANK YOU!

Hopefully 2017 might do miracle so i can stay....You cna't believe i even forgot my user name and password..LMAO!...So kila mtu is hear? akina Nyani Ngabu and others au watu wali-sepa na kijiji? (i love this word "sepa na kijiji"). Good to see you my friend, the coolest dude....
 
Attachments

  • Screenshot_2016-12-29-19-58-17.png
    Screenshot_2016-12-29-19-58-17.png
    72.7 KB · Views: 41
  • Thanks
Reactions: BAK
...lucky you that you're able to remember your pw. Nyani na wengine wengi bado wamo humu, but also we have lost few or maybe they made a decision to use new IDs. Welcome back my friend...lol! the coolest dude on JF hahahahaha I like that :):):) THANK YOU!

Leo nipo bored kwa jobo nikasema let me check out JF and wish ya"all Happy New year 2017...Stay Cool my friend...God Bless!...

So everyone is still using same name like steve Dii, Nyani Ngabu etc those are few i can remember user name zao....plus you ha ha ha !!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Thank you Happy New to you too my friend, majority of them they are still using the same IDs ila Dii anaonekana kwa nadra sana siku hizi. Usipotee sana nafasi ikikuruhusu au ukiboreka kazini lol! :):):) pita humu japo for few minutes to share with us your hekima na busara.

Leo nipo bored kwa jobo nikasema let me check out JF and wish ya"all Happy New year 2017...Stay Cool my friend...God Bless!...

So everyone is still using same name like steve Dii, Nyani Ngabu etc those are few i can remember user name zao....plus you ha ha ha !!
 
Deni halimfungi Mtu jela, Ila katika hii awamu ya huyu Mtukufu (katika sauti ya Tundu Lissu), Jela lazima twende tu!

hii suala la kumfunga mwajiri au kulipa fine sawa na Makato litafanya waajiri kuacha kuajiri wanufaika wa bodi ambao bado wana madeni. hasa kwa kampuni ndogo ambazo mishahara inaweza kuchelewa.
 
Yaani ni mambo ya kustaajabisha sana ambayo yanazidi kutishia ajira kwa waajiri kuogopa kuwaajiri wale wenye madeni ya elimu ya juu. Serikali nayo bila kuangalia repercussion ya hili tangazo kwenye uchumi na ajira imekaa kimyaaa! HAPA KAZI TU!

hii suala la kumfunga mwajiri au kulipa fine sawa na Makato litafanya waajiri kuacha kuajiri wanufaika wa bodi ambao bado wana madeni. hasa kwa kampuni ndogo ambazo mishahara inaweza kuchelewa.
 
hivi kabla ya Serikali kuchukua Uamuzi Huu, imetafakari kwanza Je! Hao Wadaiwa Sugu Baadhi Yao Wanaajira Tayari?

Au Unakwenda kumkamata Mtu Ambae Kutwa kucha Anazunguka na Vyeti Kutafuta Kazi?

Nawaza tu Kwa Sauti Jamani.
 
Serikali ya Mtukufu magufuli imeishiwa fikra ya kukusanya kodi mpaka imeamua kuwadai wa kwa nguvu. Hivi kama zile nchi za magharibi wangeifanyia hivyo Tanzania kwa kudai madeni yake kinguvu tungekuwa na nchi? Mdaiwa hafungwi na wasitutishe na ujinga wao wakutokufikiria ya jinsi ya kuwa na vyanzo vya kukusanya kodi. Naiona ile kodi ya kichwa kama enzi ya nyerere ikirudi.
Magufuli na genge lake limeishiwa fikra na na wala hawajui jinsi ya kukusanya kodi. Wamebakia kuwabana maskini
 
Wangekuwa wanawafanyia hivi wale wa ESCROE, EPA n.k tungefika mbali. Sera mbovu za chama na ubinafsi
 
wawahi kuja maana nina mpango wa kuongeza mbwa tena nawavutisha na bang sipendi ujinga mm.......
 
Back
Top Bottom