Wadada wazuri mnatufanya wakaka tuwahi maofisini

benteke

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
1,305
1,066
Kha..! yaani nadamka mpaka najishtukia...najikuta nimeshavaa kila kitu nikitaka kutoka naona giza nje..nakumbuka kuangalia saa..eti ndo saa kumi na moja kasorobo. Inabidi nirudi nikae nizuge kidogo angalau nitoke saa kumi na moja na robo hivi.Nafika ofisini nafikiri nimewai naangalia parking nakuta kuna wenzangu wanne washafika, nachoka kabisa. Yaani haya mateso yoote ya kudamka alfajiri na kuwai ofisini ni kwa sababu ya kuflirt kidogo na hawa warembo kabla mda wa kazi...tuko wengi hata wazee wapo pia .....ni raha sana. Wadada wazuri hasanteni sana mnatuliwaza na kututoa stress kabla ya kazi...Sizungumzii uzuri wa umbo na sura tu, hata wa moyoni pia... unaweza kuwa mzuri wa umbo ukawa na roho mbaya, ni mwiba ofisini. Tunawapenda wadada endeleni na moyo huo, maana mnatufanya tunaipenda kazi hata kama mshara ni mdogo.
 
Duuuh mimi ambavyo sipendi kuongea ongea asubuhi sasa
Kuna mmoja huwa hapendagi kuongea kama wewe...basi mimi huwa nasikia raha nikimtengenezea chai...nikimpa basi huwa anacheka...na mimi naona raha sana.
 
Unakuaga huna kazi ya kufanya au kuandaa chaio ndio kazi zako hapo ofisini kwenu?
 
Kha..! yaani nadamka mpaka najishtukia...najikuta nimeshavaa kila kitu nikitaka kutoka naona giza nje..nakumbuka kuangalia saa..eti ndo saa kumi na moja kasorobo. Inabidi nirudi nikae nizuge kidogo angalau nitoke saa kumi na moja na robo hivi.Nafika ofisini nafikiri nimewai naangalia parking nakuta kuna wenzangu wanne washafika, nachoka kabisa. Yaani haya mateso yoote ya kudamka alfajiri na kuwai ofisini ni kwa sababu ya kuflirt kidogo na hawa warembo kabla mda wa kazi...tuko wengi hata wazee wapo pia .....ni raha sana. Wadada wazuri hasanteni sana mnatuliwaza na kututoa stress kabla ya kazi...Sizungumzii uzuri wa umbo na sura tu, hata wa moyoni pia... unaweza kuwa mzuri wa umbo ukawa na roho mbaya, ni mwiba ofisini. Tunawapenda wadada endeleni na moyo huo, maana mnatufanya tunaipenda kazi hata kama mshara ni mdogo.

Tunatofautiana. Yaani mimi uhusiano wangu na msichana mzuri ni ama mambo ya kazi ama kumpiga dushe tu. Zaidi ya hapo sipendi kuongeaongea nao.
 
Sasa kama pananuka nnapokuwa nimetoka kupiga mswaki mchana si ndio zaidi?
teh! teh! teh!Kama umepiga lakini hutumii dawa je? si ndo umeichokonoa harufu. Kupiga mswaki sio hoja. Hoja umepigaje mswaki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom