Wadada Wazuri hawajui kuvaa Vizuri

Kuvaa vizuri kwa macho yako unakutafsiri vipi?! Kwangu mtu akivaa simple, kiasi kwamba nikifanya mahesabu ya vitu alivyotupia havifiki hata elfu 10, kwangu atakuwa amevaa vizuri provided vimemtoa na kumfanya awe comfortable!

Ukiwa na makalio makubwa halafu ukanivalia jinzi ya kubana kwangu hujavaa vizuri na utanikwaza kweli kweli wakati kwa mwingine, huyu atakuwa amevaa vizuri ile mbaya!

Ukiwa kimbau mbau na miguu kama cherewa halafu ukanivalia kimini; wakati wa kuondoka tukifika mbele nitakuambia "tangulia nitakukuta njiani" lakini kama umenipigia trouser simple; kwangu utakuwa umevaa vizuri!!!

Sasa wewe huko kuvaa vizuri unakutafsiri vipi ambako kwa bahati mbaya kabisa, kuvaa kuzuri kwako hakuwezi kuwa kuzuri kwa wengine!!!!
uko vizuri,japo kuna watu wazuri tu inajulikana kabisa kwa wengi..na kuna watu wanabebwa na mavazi wanayovaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom