Wadada wa kanisani na mini sketi

lup

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
2,514
Reaction score
2,744
Toka nianze kusali makanisa hasa yanayoongoza ibaada kwa lugha iliyokuja na ndege na yale ya mjini kati, kuna kitu kiukweli huwa kinanipa shida sana hasa pale unakuta umekaa na mdada ana min sket inayopita magoti halafu na juu amevaa nguo inayoishia kiunoni tu.

Halafu unakuta hana hata kile kitambaa cha kujifunika hana, shida inaanzia pale anapoanza kuingia rohoni kwenye nyimbo za kuabudu, Mara ananyosha mikono, Mara anainama, Mara anapiga magoti hapo kiuno nje na kama anashanga ndio basi tena akili inasoma mbali ya kijana rijali.

SAA ya mahubiri yuko bize na simu yake ya sumsang na hajali kama amekaa na kijana wa kiume hapo halafu mapaja yako nje balaa, kwa kweli nahisi nitaanza kuwa nawatongoza tu kwani uvumilivu unataka kunishinda.

Au kwenye darasa cha sunday school maana hapo viti vinaangaliana bila hata uoga dada unamwangalia mapaja hata hajali.

NB; WAPO WATAKAOSEMA KANISANI UNAENDA KUABUDU NA SIO KUANGALIA MTU, lakini ukweli ni kwamba macho hayana pazia DADA ZETU TARATIBU KWENYE NYUMBA ZA IBADA. Kwani hata maombi ya kutafuta mke bado sijajibiwa sasa kazi sana.
 
kuna vitu vingine hata roha hana cha kusaidia yaani kitu paja na kiuno Mara shanga.... dah..kile andiko la amtazamae mwanamke akamtamani.... naona hapo linanihukumu kabisa
wanamsingizia tuu roho wa watu,wala hawataki wao wafanye hvo
 
Reactions: lup
wanamsingizia tuu roho wa watu,wala hawataki wao wafanye hvo
nahisi na wao huwa wako kwenye mauzo....nitaanza kuwatokea..
 
kwani msaada ni lazima utambulike??
 
Reactions: lup
kwani msaada ni lazima utambulike??
rafiki Niko kwenye Maombi ya kutafuta mchumba,sasa Siku nikitaka kuoa sitapata kampani nzuri ya kanisa ndio naandaa mazigira
 
rafiki Niko kwenye Maombi ya kutafuta mchumba,sasa Siku nikitaka kuoa sitapata kampani nzuri ya kanisa ndio naandaa mazigira
unashindwa kutongoza???
 
Reactions: lup
Shetani yupo hata makanisani akiwinda. Mimi huwa natafuta sehemu nyingine ya kukaa na nikikosa basi afadhali niondoke. Kuna mdada mmoja nadhani hata chupi hakuwa nayo nilimwambia aondoke na jambo la kushangaza kweli akatii na kutoka nje.
 
Mkuu unaabudu wapi nije this Sunday[emoji4]
 
Dhumuni la uzi huu ni kutaka kusema kwambaaaa "kwa kweli nahisi nitaanza kuwa nawatongoza tu kwani uvumilivu unataka kunishinda" huko koote ulikua unazunguuka tu baba lup
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…