Wadada 'smart' mna gharama sana

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
28,809
39,015
Wadada smart tunawapenda sana, na tunathibisha mna utamu wa kipekee; popote pale pongezi ziwafikie.

Changamoto kubwa mliyonayo; mnatutesa sana sisi wanaume; hela haikai, muda wote tunapokuwa na nyie, pesa huwa inateketea sana.

Mara wigi laki sita, hujakaa sawa nataka niende saluni kusafisha kucha, mara nimeona kisuruale pale, mara ile raba nimeipenda, mara nataka nikabadilishe mtindo wa nywele n.k

Kwa mazingira hayo; nyie hamfai kuolewa, tutakuwa tunawapa kampani ya kupelekeana moto tu
 
Kila mbuzi ale usawa wa kamba yake...
Mwanaume mwenyewe wa siku hizi ukijigeuza kikoba kila siku mahitaji mapya anakukimbia kweupeeee. Yani wanaume wa siku hizi wanapenda upendeze kwa gharama zako yeye akija anafaidi utamu tuu asiojua umependezaje...

Bora nibaki na utamu wangu asee. Raha ya mwanaume uhudumie mwanamke wako apendeze hata akiwa ametangulia unajiskia ufaharii
 
Wadada smart tunawapenda sana, na tunathibisha mna utamu wa kipekee; popote pale pongezi ziwafikie.

Changamoto kubwa mliyonayo; mnatutesa sana sisi wanaume; hela haikai, muda wote tunapokuwa na nyie, pesa huwa inateketea sana.

Mara wigi laki sita, hujakaa sawa nataka niende saluni kusafisha kucha, mara nimeona kisuruale pale, mara ile raba nimeipenda, mara nataka nikabadilishe mtindo wa nywele n.k

Kwa mazingira hayo; nyie hamfai kuolewa, tutakuwa tunawapa kampani ya kupelekeana moto tu
Tafuta wa size yako mbona simple tu, wewe mtu mmetongozana Insta baada ya kufuatilia picha zake kila siku kwa mwezi mzima na kila siku picha mpya na nguo mpya, sasa wewe ukijiingiza hapo unataka kumlilia nani?

Au hujui kuna binadamu wanajiita wao ni brand?
 
Hasaaa hizo sifa ni za ma slay queen...a.k.a.wadangaji

Smart hatuombi ombi hela kizembe. .zembe....
Yani kusafisha kucha niombe hela...usafi wangu mweenyewe???
Huku field ndio kuko hivyo mkuu, na wanachagua saluni ya kwenda
 
FB_IMG_16512346365169915.jpg
mpeni pongezi mwamba kavaa JF anasambaza upendo
 
Kila mbuzi ale usawa wa kamba yake...
Mwanaume mwenyewe wa siku hizi ukijigeuza kikoba kila siku mahitaji mapya anakukimbia kweupeeee
Yani wanaume wa siku hizi wanapenda upendeze kwa gharama zako yeye akija anafaidi utamu tuu asiojua umependezaje...
Bora nibaki na utamu wangu asee
Raha ya mwanaume uhudumie mwanamke wako apendeze hata akiwa ametangulia unajiskia ufaharii
Tatizo mnatufanya tunakuwa masikini
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom