Wadada wenzangu samahanini lkn kwa hili naomba nimsapot mtoa mada. Ukweli kwenye hili wengi wanashindwa. Wadada wanahusudu kuvaa tu lkn miili yao kuitunza wanasahau sana. Hili mm nimeliona kwa wanawake wenzangu, kwapa nyeusi, na zimefanya marinda/makunyanzi, kuishia kunyoa tu sio solution, harufu nayo pia lazima ifanyiwe kazi, kama ni maradhi tiba si zipo? Na tuache kutumia deodorant za ajabu mana wengine huona wanakata harufu kumbe hujipaka madude ya kukirihisha wenzao. Na kwenye deodorant spray ni nzuri zaidi kuliko rolls au sticky. Spray zinasaidia kuweka dry muda mrefu. Dada kama una uwezo fanya waxing ya Kwapa kuliko kutumia wembe au shaving mashine. Waxing inasaidia kuepusha weusi na vinywele vinachelewa kuota. Al udi na udi nao vinasidia kukufanya uwe unanukia vizuri full time. Mwanamke kweli ukiwa safi inapendeza zaidi, hao wanaume sisi ndo tuwasaidie kuwa wasafi.