Wadada leo mnisamehe kidogo

Wadada leo mnisamehe kidogo

Mada ya kikubwa nimepata point hapa sijutii kuupitia huu uzi thanks mkuu
 
Aisee mulemuleeeeeee atakae bisha limempata la kisogo
 
Tena wengine watakuja kuusifia huu Uzi na kuongezea ya kwao lakini nao wamo kwenye hiyo kadhia
 
Kweli vyuma vimekaza yaani kutwa nzima mnawaza kuwasema wanawake kwa mabaya yao.... Badilikeni bhana.
 
Wanawake wengi wa siku hizi wamevurugwa na vyuma kukaza,hata uwaambie nini na maneno gani yenye hekima na busara hawatakuelewa ni sawa mbuzi kumpigia gita,wanachohitaji ni pesa na maisha ya anasa na sio maisha yenye neema ya Mungu,Wanawake wengi wanaamini pepo yao ipo Duniani ndio Maana sio Wavumilivu wa Shida,Wanaangalia leo hawaangalii kesho,wanasema huna pesa leo sikupendi ukipata pesa kesho nakupenda!,nashauri ukiwa kama mwanaume ukikosa mwanamke mwenye mapenzi ya kweli na umri unaona unaenda tafuta Mwanamke yoyote Mzalishe halafu mpige chini kisha uchukue mtoto wako umlee bora stress za kulea mtoto kuliko stress za kulea jitu zima lisilojielewa!
Umenena vema huwa wana kamsemo kao...eti maisha yenyewe mafupi...
 
Uko sahihi mtoa mada ila shida moja ni kwamba, huyo asiye na kitu unamvumilia leo na kumu ecourage akipata sasa anahamia kwa slay gueens wewe unawekwa kipolo. Yaani na yeye akishakuwa njema anatafuta wale wadada wanaokula bila kutafuta hii ndo shida. Wanawake wengi leo hii wanalia wanaume zao wanatoka nje ya ndoa na wadada wa mjini kiasi kwmba nyumbani matunzo hafifu hela anapeleka kwa mchepuko!?

So hebu mjitathmini nyie wanaume kwanza kabla hamjawasema na kuwananga wanawake. Bila nyinyi kuwapa kipaumbele na good times unadhani wangekubali kuwa nyumba ndogo zenu? Na kama mkeo amekuvumilia from nothing to something, hao michepuko wa kazi gani?

Nawasilisha
 
Uko sahihi mtoa mada ila shida moja ni kwamba, huyo asiye na kitu unamvumilia leo na kumu ecourage akipata sasa anahamia kwa slay gueens wewe unawekwa kipolo. Yaani na yeye akishakuwa njema anatafuta wale wadada wanaokula bila kutafuta hii ndo shida. Wanawake wengi leo hii wanalia wanaume zao wanatoka nje ya ndoa na wadada wa mjini kiasi kwmba nyumbani matunzo hafifu hela anapeleka kwa mchepuko!?

So hebu mjitathmini nyie wanaume kwanza kabla hamjawasema na kuwananga wanawake. Bila nyinyi kuwapa kipaumbele na good times unadhani wangekubali kuwa nyumba ndogo zenu? Na kama mkeo amekuvumilia from nothing to something, hao michepuko wa kazi gani?

Nawasilisha
Kwa upande mwingine hawa hawa ndio wanaoleta ukakasi.

Kama ulivyosema wajitathmini kwanza kabla ya lawama zilizo nyingi kumuangushia mwanamke.
 
Kwa upande mwingine hawa hawa ndio wanaoleta ukakasi.

Kama ulivyosema wajitathmini kwanza kabla ya lawama zilizo nyingi kumuangushia mwanamke.
Umeona eeh, hawa wanaume ndo chanzo. Wangekuwa wanathamini mchango wa mwanamke wake katu kusingekuwa na nyumba ndogo. Na pia wasingehudumia hzo nyumba ndogo naamini zingepungua kwa kiasi kikubwa au kwisha kabisa na pia pengine wangetulia na kuwavumilia hao wasio nazo
 
Umeona eeh, hawa wanaume ndo chanzo. Wangekuwa wanathamini mchango wa mwanamke wake katu kusingekuwa na nyumba ndogo. Na pia wasingehudumia hzo nyumba ndogo naamini zingepungua kwa kiasi kikubwa au kwisha kabisa na pia pengine wangetulia na kuwavumilia hao wasio nazo
Pia naona kuna kachembe chembe ka ubaguzi hilo la kutiana moyo ni kwa wote na sio mwanaume pekee eti ndio atiwe moyo huku mwanamke kabweteka ukitegemea akifanikiwa atakuwa mwenzio ila mwisho wa siku unaachwa kwenye mataa.

Unakuta mtu ana nyumba ndogo kibao kisa tu kafanikiwa na kumsahau aliyekuwa naye bega kwa bega kwenye safari yake ya mafanikio.

Hatukatai ila wanaume wawe ni wenye kukumbuka sababu walio wengi huwa wanakuwa wasahaulifu na mwisho wa siku mwanamke ndio anaonekana hafai katika jamii.
 
Inasikitisha sana....
Wamekuelewa tatizo binadamu ni wabishi sana...

Kuna msemo unasema "To every successful man there is a strong woman behind"

Kwa hiyo mwanamke anayempapatikia mwanaume ambae tayari ana mafanikio, kuna uwezekano kwamba huo mwanaume tayari ana mwanamke aliyetoka nae mbali mpaka kufikia hayo mafanikio, ila wewe ukawa kiburudisho tu kwake...



Cc: mahondaw
 
What a beautiful msg... Barikiwa zaidi upate na mapacha duble duble
 
WADADA MNISAMEHE KIDOOOGO!

Simwongelei mtu ni ujumbe kutoka kwa mdau wa masuala ya wanawake anaitwa
Lu-Patie!

Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi WA kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto WA kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja..anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!

Una mpuuza Na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume WA Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa. Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanawake?

Umegombana Mara ngapi na Huyo HB wako kisa usaliti na bado upo nae?? Wanaume wangapi wenye pesa mvuto na kila kitu ndani lakin wamekutumia na kukuacha? Lakini bado hujifunzi aina ya mwanaume wa kuwa nae?

Japo vyema acha kujidharau u mrembo onesha kwamba unajipenda kuanzia MAVAZI NA KAULI !
Marafiki zako wangapi waliolewa na wanaume WA kawaida lakin Leo wana mafanikio? Kwa nini usiige..weka uzuri pembeni simama imara kama MKE na MAMA bora WA kesho. Mtie moyo mmeo ajisifu kuwa Na wewe, si kila mara dharau Na kumbeza!!

Kifupi hakuna mwanamme anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya !! Encouragement matters most kwa mwanamme yeyote mwenye akili timamu!
Umenena vyema mkuu
 
Back
Top Bottom