Wadada Inawahusu hii

Wadada Inawahusu hii

Ndio upo busy sana. Kuanzia form one umesoma boarding hadi degree na baada ya hapo umepata kazi unatoka nyumbani sa12 unarudi sa 2 usiku. Lakini hii sio sababu ya kukufanya usijue kupika. Haipendezi msichana wa zaidi ya miaka 15 akiwa hajui kupika chakula kizuri watu wakala wakafurahi. Hauolewi ili uende kupika lakini kumbuka kila siku inawapasa kula. Kila msichana lazima ahakikishe anajifunza kupika, hakuna anayezaliwa anajua kupika ila ni kujifunza na kupika mara kwa mara. Usimtegemee tu dada wa kazi ndiye akupikie, hata akipika vibaya hutakuwa na ujasiri wa kumkosoa. Watoto na mume hujisikia vizuri wakipikiwa chakula mama/mke.



Kwa wale walioolewa hakikisha kila wiki kuna siku ambazo unapika wewe mwenyewe kwa ajili ya familia yako. Sio kila siku kila wiki kila mwezi ni dada wa kazi tu ndiye anayepika. Yani ufanye bidii uwe unajua kupika zaidi ya dada uliyenaye hadi ifike mahali ukipika chakula wote wajue mama leo aliingia jikoni na wakati mwingine wakuombe uwapikie kitu fulani maana wanajua wewe ndiwe mtaalamu.


Hata kama watakupinga wanawake wote humu jamvini ila uliloandika ni ukweli usiopingika. Binafsi nimeoa na naona furaha tunayoipata mimi na wanangu siku mke wangu akiingia jikoni. "Mkono wa mke ni mtamu kwa mumewe na watoto". My sister Snowhite, Kaunga, na wengine wote tafadhali mje mtujuze ili hekima na busara itawale hapa. Hizo bold ndio umenikosha zaidi japo ujumbe uko poa kwa pamoja.
 
Kuna watu wako very theoretical when it comes to ndoa.... Wao ukiwagusia hayo aliyoyasema binti2013, utawasikia... MFUMO DUME....... Na usishangae mtu kama Nivea, kala vyakula vya kupika mama yake mzazi mwanzo mwisho, lakini yeye anataka aje awalishe wanawe na mumea misosi ya house girl in the name of haki sawa.

Ningeelewa sana kama angalau
Nivea angesema mpike wote, yaani baba, mama na beki tatu.
Kuna ishu mbili/tatu hapa mkuu.Wanaosema kwamba kujua kupika kwa mwanamke wa kiafrika sio ishu....eidha:
1,Hawajui kupika
2,Hawajaolewa
3,wameachika kwa kutokujua kupika.
4,Uzungu mwingiiii....
 
Kuna ishu mbili/tatu hapa mkuu.Wanaosema kwamba kujua kupika kwa mwanamke wa kiafrika sio ishu....eidha:
1,Hawajui kupika
2,Hawajaolewa
3,wameachika kwa kutokujua kupika.
4,Uzungu mwingiiii....

kuna hizi sababu za dada mkumwa AshaDii nadhani zinawagusa sana hao watu

Sababu ni nyingi kwa kweli ambazo hupelekea hivo....

Malezi...

Wazazi wengi hasa Mama ambae ndio ana nafasi kubwa saana ya kumlea binti ili awe mwanamke kamilifu hua mara nyingi huchemka na kufikiri kwamb akimlea mwanae kisasa (kisasa hapa imekua defined vibaya) kua alelewe akiwa vidole juu.. bila kumfundisha kazi za msingi kama vile usafi wa nyumba... kufua nguo... mpangilio wa numbani na most importantly kupika.

Elimu

System ya elimu sasa hivi imebadilika saana... Na for the worse kwani watoto asilimia 95 ya maisha yake yamelenga tu elimu.... Mtoto toka grade one yupo boarding... mara anaesoma day anasoma na tuition (jamani imagine tuition ya darasa la kwanza)... Maisha yake yoote shule... Likizo akija anatafutiwa tuition na akirudi ajipumzishe na ajisomee... at the end of the day anakua a very great person careerwise but kupika hawezi...

Ushamba & Ulimbukeni...

Ladies wengine anaona sifa kusema kua hajui kupika... ili sijui aonekane matawi ama lah! sielewi.... For mie naelewa kua mtoto wa kike yeyote ambae amelelewa nyumba ya mama/mlezi anaejua kweli definition ya a true African woman... atamfundisha tu binti yeyote ndani kupika...awe mwanae ama lah ni muhimu mno.

Uvivu...

Kupika sio miujiza.... hata kama bahati mbaya ikatokea kua mtu hajui kupika ni muhimu akajituma na kujifunza na taratibu atajua.... Mwingine ni mvivu mno... ya akipika avavichemsha chemsha tu basi anaona kamaliza hakuna la ziada... Hata aende kwa mwenzie akapenda chakula hata kujisumbua na kuuliza vipi kapikaje habari hana kabisa!
 
Last edited by a moderator:
binti2013, nasema yategemea malezi, mila na desturi. Unaweza ishi bila kupika ......na nani aliyesema mwanamke ni LAZIMA ajue kupika ndio awe mama wa nyumba. KUPIKA au kuwa mpishi hodari na added advantage ya mwanamke lazima sio kigezo.

Nafikiri ungesisitizia mwanamke USAFI...unaweza ukawa mpishi mzuri usafi ukakushinda bibi, all your effort in drain maana hata chakula chako hygiene itakuwa problem. Na pia hiyo ni sifa ambayo inakipaumbele zaidi ya upishi.

Mwanamke tabia, ujue vipi kulea family yako na kufanya family bora.......

Mimi naamini swala la usafi ni la kilazima na kiafya hivyo ni wajibu kwa binadamu kuwa msafi kwa mazingira yanayomzunguka na usafi binafsi. Kwenye kupika siyo jambo la ulazima ila lipo kitamaduni zaidi, ukija kwetu Afrika mwanamke ili awe kamili kwa mazingira yetu lazima ajue kupika ila siyo lazima awe mpishi kama ilivyo unakuja kijana ni dereva mzuri japo hajawahi kumiliki gari au hata la familia. Ni vema mwanamke kujua 1 mbili za mapishi.
 
Ndo maana makaumuni yanaajiri watu wa PR mamaa(hao extras nao ni muhimu,unless kama hujaolewa bado).....wewe unafikiri uzuri na usafi tu ndo mambo ya msingi?Na unataka kutuaminisha kwamba ukiolewa kama hujui kupika ni poa tu?Believe me kama hujui kumpika mumeo na watoto vizuri hilo ni tatizo tena kubwa tu(labda kama umeolewa na mzungu)

Ndio mkuu ndo maana mi nilijiopolea mzungu wangu taratiiibu...hakuna cha wakwe sjui watakuonaje...sometimes huwa nakaa kwenye sofa nanyoosha miguu yeye anakarangiza. maisha burdaaani.
 
Nivea.....labda unaongelea utamaduni wa kizungu.Kwa waafrika ni muhimu mwanamke akajua kupika.Tena kupika vizuri.Ni aibu hata kwa wakwe zako kama hata kupika hujui infact hata huyo mume si ataanza kulalamika?
sijaolewa na wakwe ,kwangu its just a small staff!!
 
Waambie bwana manaake ni aibu kwa mwanake kutojua kupka .kama hujui kupka kwe2 huolew MAMAANGU HUWA ANAPENDA KUKAA NA WAKWE ZAKE B4 HUJAAMUA KUMWOA XO PALE ANAKUWA ANAMXOMA TABIA datz y nampenda my mum
 
Ndo maana makaumuni yanaajiri watu wa PR mamaa(hao extras nao ni muhimu,unless kama hujaolewa bado).....wewe unafikiri uzuri na usafi tu ndo mambo ya msingi?Na unataka kutuaminisha kwamba ukiolewa kama hujui kupika ni poa tu?Believe me kama hujui kumpika mumeo na watoto vizuri hilo ni tatizo tena kubwa tu(labda kama umeolewa na mzungu)
Hapo kwenye mabano nimepapenda maana panatupa suluhisho.
Ngoja nitafute mzungu mie.
 
kupika sio common need kwa binadamu kama wewe hujui wengine wanajua waajiri wakupikie ,ujue kila kitu isaidie nini wanaosomea chefs wafanye nini?kha

Ukiona hivi ujue ni mmoja wa walee wasioweza hata kuchemsha maji ya kuoga, aibu kweli kweli, african girl unable to cook, pathetic!
 
Back
Top Bottom