Wadada acheni hii tabia ya kuuliza 'ndoa lini'

Wadada acheni hii tabia ya kuuliza 'ndoa lini'

lazima ukae

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Posts
791
Reaction score
417
Unakuta umeingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na msichana na mahusiano yenu hayana hata miezi miwili lakini kutwa kucha msichana anaulizia masuala ya ndoa. Mnatakiwa mtambue kwamba ndoa si jambo la mzaha na kukurupuka, ndoa inahitaji wawili kujuana kwanza kitabia.

Hii tabia ya kuulizana "ooh baby lini unakuja kuleta barua ya posa nyumbani" bwana weeeee mbona una haraka hivyo, mambo ya ndoa hayahitaji papara.

Kama una tabia nzuri huna sababu ya kulazimisha mambo ya ndoa, ukiona binti analazimisha masuala ya ndoa jua kuna tatizo ndani yake hivyo hafai kuwa wife material. Kama nina nia ya kukuoa nitakuoa na kama sina nia hata ufanyeje hauwezi kunibadirisha mawazo yangu labda uniendee kwa sangoma.

Kingine tabia ya kuombaomba pesa kila mara mpunguze otherwise mtaishia kukimbiwa kila siku. Kupata mpenzi haimaanishi umepata ajira au kitega uchumi kwamba matatizo yako yote umalizie kwake.

Tunatambua kwamba mnamahitaji yenu kama wanawake na tunapaswa kuwatimizia ila mpunguze tamaa kwamba kila unachomuona nacho swahiba wako basi na wewe lazima uwe nacho hapana hatuwezi fika kwa staili hiyo.

Binafsi huwa napenda nimuhudumie msichana pasipo yeye kuniomba sababu najua ni jukumu langu kumpendezesha na kumtimizia mahitaji yake.

Yangu ni hayo tu
 
wanakwambia ndoa ni kama gereza, unapewa tu nafasi ya kuchagua ni mfungwa gani uishi nae selo moja sasa ni bora kumpata yule mnaeendana kitabia, zaidi ya hapo huwezi pata tamu ya ndoa zaidi ya kuzeeka na kufa mapema kwa stress
 
Na nyie muache kuwapa wachumba zenu majukumu ya ndoa!!!! Mara kufua kupika sheria kibao,,,akati huna mpango nakua naforce nisiendelee kuwa mtumwa wako mwisho wa Siku unabwaga...ahhhhh kwanini nisijue hilo ili nijiongeze mapema???? Unaishi na dada wa watu miaka 4 huoi, miaka 30 ndiiii inagonga ukiwa naee duh mwisho wa SKU unamwacha mnaanza kuwasema mbona hawaolewiiii....lazima kuuliza...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_2017-08-17-13-02-14.png
 
wanakwambia ndoa ni kama gereza, unapewa tu nafasi ya kuchagua ni mfungwa gani uishi nae selo moja sasa ni bora kumpata yule mnaeendana kitabia, zaidi ya hapo huwezi pata tamu ya ndoa zaidi ya kuzeeka na kufa mapema kwa stress
Lafu ukichunguza wanaume ndio wanakufa sana maaana kwa haraka wajan ninao wajua mimi kam14
 
Back
Top Bottom