Viongozi wetu wanachoweza saaaana ni mipasho, kuchekacheka na kulialia na kulala hotelini na vimwana (wanaibiwa au wanafia humo)
JK na Pinda hawajui kwa nini sisi ni masikini unategemea nini? Huwezi kutatua tatizo ambalo hujui chanzo chake
Ukisema uchumi haukui watakwambia hata US na EU kuna mdororo wa uchumi hivyo tusishangae
Ukisema hatuna umeme wa uhakika watakwambia hata Kenya na SA kuna mgawo
So tuwape muda kidogo mpaka mwisho wa mwaka huu watakuwa wamefanya upembuzi yakinifu na kuandaa mchakato maalum ili kiliingiza taifa kwenye uchumi thabiti na endelevu kwa kasi ari na nguvu mpya chini ya serikali madhubuti ya mpendwa mtukufu wetu JK..