Wachumi toka Vietnam na China: Uchumi wa Tanzania una siasa nyingi kuliko vitendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachumi toka Vietnam na China: Uchumi wa Tanzania una siasa nyingi kuliko vitendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Mar 29, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wachumi kutoka nchi za china na vietnam wanashangaa umaskini wa tz na kwenda mbali zaidi na kusema viongozi wetu wanamaneno mengi kwelli kuliko uhalisia wa kiuchumi hilo limemfanya hadi waziri mkuu Pinda kukiri kuwa uchumi jinsi unavyozungumzwa hauna uharisia na hari jinsi ilivyo. Wachumi hao wameenda mbali na kudai Tanzania haitakiwi kuwa kkt hari hii kwa kila kitu inacho.

  my take

  kawa wageni wasocialist wenzetu wa zamani wanatuonea huruma hivi watanzania tumelogwa kiasi hiki na viongozi wetu walioko madarakani mbona ZAMBIA,KENYA, MALI nk wameweza? vp LIBYA, MISRI nk wao wananini na sisi tunashindwa na nn?

  source tanzania daima na mwananchi
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni ukweli usiopingika.
   
 3. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mashambulizi kila kona!! Mwanzo ilikuwa toka Magharibi, sasa mashariki. Tutaenda wapi kuomba mikopo na misaada??????:crazy:
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wachumi wenyewe Sampuli ya Mwigulu....
   
 5. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Bongo longo longo ndio mpango.

  Toka iuanze kusikia daraja kigamboni miaka mingapi?

  Toka ianze kusikia fluy overs miaka ngapi?

  Toka uanze kusikia mapinduzi ya kijani?

  Na hili la mabasi yaendayo kasi?

  Umeme wa uhakika? Tukaambiwa mgao utakuwa historia

  Hiyo ndio bongo bana! Kasi zaidi ari zaidi
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  huwa simpendi pia huyu jamaa lakini nasita kuwalaumu viongozi badala yake nawalaumu Watanzania (mimi mwenyewe) kwa kushindwa kutumia hata njia mbadala ili kuwafanya viongozi wafikiri au hata kuwaondoa madarakani.

  Ninavyoandika hapa umeme umekatika.
  Sababu wanasema ni Agreko inaidai Tanesco lakini ukiangalia kiasi wanachodai ni dhahiri kingeliweza kununua generator zao wenyewe. Na hapo ni section moja ya utawala tulionao sasa, tuamke watanzania!

   
 7. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza rudisha ubalozi na Israel ili kuondoa laana
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata kama ila sisi tunachoongelea ni wanachokiongelea ni kweli? Na tufanyeje?
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wachumi wetu na viongozi wako kwenye mchakato na upembuzi yakinifu kujua kwa nini tanzania ni maskini na wakimaliza kuandaa report yao wataiwakilisha kwenye baraza lka mawaziri kujadiliwa na kufanyiwa upembuzi wa kina
  Wabongo bado tuko kwenye mchakato wa kujiuliza klwa nini ni maskini
   
 10. b

  bantulile JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,439
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hilo sio jipya. Imekwisha semwa sana, Afya siasa, Elimu, Ufundi nk ni siasa tu. Hata uteuzi wa watendaji inatawala siasa sio utendaji.

  Wanasiasa walikwiaambiwa kuwa wanaingilia hata wasichokijua. Wanajua tatizo lao.
  Hoja mpya ingekuwa tufanye nini ili wanasiasa wasiingilie kila kitu. Nadhani tatizo ni uchanga wa siasa kudhani ukuwa ukiisha kuwa mwanasiasa, ghafla unakuwa Afisa manunuzi, Daktari, Mchumi, Mhandisi hata bila kusomea. Hawa wanasiasa watokeje hapo? Tukifanikiwa kuwatoa hapo, uchumi utakua, elimu bora afya bora nk.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Wachumi waipiga kombora Serikali mbele ya Kikwete [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 28 March 2012 20:54 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Rais Jakaya Kikwete, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba,baada ya kufungua warsha ya siku mbili ya kujadili Mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini nchini iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Kupunguza Umasikini (REPOA) jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix

  NI WA KUTOKA CHINA NA VIETNAM, WASHANGAA MFUMUKO WA BEI WASEMA TATIZO NI VIONGOZI KUWA NA MANENO MENGI KULIKO VITENDO
  Raymond Kaminyoge
  WACHUMI kutoka China na Vietnam wamesema umasikini unaoikabili Tanzania unatokana pamoja na mambo mengine, viongozi kuwa na maneno mengi kuliko vitendo.Walisema hayo jana mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kukosoa mchakato wa ubinafsishaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu ambao umebinafsisha na kuua viwanda vingi vya msingi.

  Wakichangia mada katika mkutano wa 17 wa mwaka wa Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umasikini Tanzania (Repoa), wachumi hao waliokuwa wamealikwa kueleza uzoefu wao katika masuala ya kuondoa umasikini, walisema Tanzania haikuwa nchi ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani, bali ilipashwa kujitegemea.

  Akitoa uzoefu wake, Profesa Do DucDinh wa Taasisi ya Kimataifa ya Uchumi ya Vietnam alisema inasikitisha kuona Tanzania ina kila rasilimali lakini ni masikini wa kutupwa.

  "Nchi imebinafsisha viwanda bila ya umakini na matokeo yake viwanda vingi vimekufa. Kwetu suala la ubinafsishaji tulikuwa makini na Serikali inamiliki viwanda vingi ambavyo vinatoa ajira," alisema Profesa DucDinh na kuongeza:

  "Vietnam hatulimi korosho lakini tuna viwanda vingi vya kubangua korosho, tunategemea malighafi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania."

  Profesa DocDinh aliishangaa Tanzania ambayo inalima korosho lakini ikabinafsisha viwanda vya kubangua zao hilo ambavyo vingi vimekufa.

  "Utabinafsisha vipi viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao ya kilimo ambacho kinategemewa na zaidi ya asilimia 80 ya wananchi?" alihoji.

  Alisema kama Tanzania ina nia ya dhati ya kupunguza umasikini wa wananchi wake, inatakiwa kujipanga na kusaidia kuikuza sekta ya kilimo.

  "Sekta ya kilimo iboreshwe kwa kupewa kipaumbele cha kwanza kwa kujenga miundombinu na wakulima kutumia mbegu bora na mbolea," alisema.

  Kwa upande wake, Profesa Li Xiaoyung wa Kituo cha Kimataifa cha Kuondoa Umasikini cha Beijing alisema maisha magumu yanayolalamikiwa na wananchi yanatokana na mfumuko wa bei hasa vyakula… "Ugali ni chakula kikuu lakini bei ya unga ni kubwa ambayo wengine wanashindwa kumudu, unategemea nini?"

  "Nilipokuja mwaka jana nilikuta kilo moja ya mchele inauzwa kwa Sh1,200 lakini nimeshangaa sasa inauzwa kwa Sh2,500! Huu ni mfumko wa ajabu."

  Alisema mfumko huo kwenye bidhaa za chakula ndio unaowasababishia wananchi umasikini kwa sababu ni bidhaa wanazozihitaji katika matumizi ya kila siku.

  Mchina huyo alisema sekta za mawasiliano na madini ambazo zinakua kwa kasi haziwezi kuwaondolea umasikini Watanzania kama kilimo hakitapewa kipaumbele.

  JK anena

  Awali, akifungua mkutano huo wa siku mbili, Rais Kikwete alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya kilimo ili kuwanufaisha wananchi na wawekezaji akisema kinachotakiwa ni wananchi kubadili mtizamo wa kudhani kwamba wawekezaji wapo kwa ajili ya kupora mali za wananchi.

  "Tukiendelea kudhani kwamba wawekezaji wapo kwa ajili ya kupora mali wakakasirika na kuondoka zao, tutaendelea kuwa masikini," alisema.

  Rais Kikwete alisema Serikali iliamua kuacha kufanya biashara na kuiachia sekta binafsi na yenyewe kubaki na kazi ya kujenga na kuboresha huduma za jamii.

  "Serikali ilikuwa inauza viberiti na nyama tukabinafsisha viwanda na sasa tumebaki kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji," alisema.

  Mkurugenzi Mkuu wa Repoa, Profesa Samwel Wangwe alisema mkutano huo utawasaidia watafiti wa masuala ya uchumi kubadilishana mawazo kwa lengo la kufanikisha ajenda muhimu ya kuondoa umasikini nchini.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  My take:

  Afadhali waseme hawa maana tukisema sie tutaambiwa chadema tu wale!!!! Haya ni matatizo ya wachumi kuwa wanasiasa na wanasiasa kujifanya ni wachumi ndio maana tunasuasua.
   
 12. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Watanzania amkeni, kwa hali hii hatutafika kamwe!
   
 13. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  "Tukiendelea kudhani kwamba wawekezaji wapo kwa ajili ya kupora mali wakakasirika na kuondoka zao, tutaendelea kuwa masikini,"

  maneno haya ya jemedari wetu yameniacha taabani.
   
 14. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  jk-lipumba.jpg jamaa anaambiwa haya yote lakini bado anacheka tu!? ....au hii picha ni ya maktaba?
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  heeee aliyasema haya???? mkuu huwa simsikilizi mtu huyu kila asemacho huwa ananiudhi tuu!
  POLE TANGANYIKA YANGU!
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  jamaa angekuwa mwanamke huyu hahahahah sipati picha aiseee!
   
 17. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,529
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  JK anasema eti..""tukiendelea kudhani kwamba wawekezaji wapo kwa ajili ya kupora mali wakakasirika na kuondoka zao, tutaendelea kuwa masikini," na pia eti....""Serikali ilikuwa inauza viberiti na nyama tukabinafsisha viwanda na sasa tumebaki kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji,".........Yaani huyu ni rais ambaye amekabidhiwa dhamana ya kuliongoza taifa kuondokana na umaskini anakuja na maneno haya.....ina maana yeye akishawakabidhi kila kitu wawekezezaji hilo linatosha......ana assume kila kitu kitakuwa sawa....kinachofanywa na hawa wawekezaji kwake si hoja......no wonder hawajui kinachofanywa na wenye migodi yetu ya dhahabu.....wao serikali cha msingi kwao ni uwepo wa wawekezaji wa nje nchini period.....yaani serikali inafurahia kujitua mzigo wa kumiliki viwanda!!!wapi unaweza kuliona hili duniani??hamna yaani....JK anaona bora kununua kiberiti toka china kuliko kutengeneza vya kwetu kwa kutumia miti yetu iliyojaa kila kona......what a president with vision we have eh!!
   
 18. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mwisho mtaomba hadi misaada ya kuingiliwa wake zenu. Naona aibu kwa kuwa taifa la ombaomba.
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  napata hasira hasa ninapoambiwa ninafursa zote za kuendele lakini bado maskini wa kutupwa.!
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna jamaa nilimsikia akisema Tanzania Blah Blah,mineno mingi!
   
Loading...