Wachina wavamia eneo, waanza kuchimba vifusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina wavamia eneo, waanza kuchimba vifusi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Aug 29, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Jumatano, Agosti 29, 2012 05:57 Na Pendo Fundisha, Mbeya

  KAMPUNI ya Wachina ya CICO inayoendelea na ujenzi wa barabara za Mbeya, imedaiwa kuvamia eneo la wananchi na kuanza kuchimba vifusi vya udongo kinyume cha utaratibu katika eneo la Machinjioni, Kata ya Ilomba.

  Imeelezwa kuwa kampuni hiyo imetapeliwa na watu wanaojitambulisha kwamba wao ni wamiliki halali wa ardhi hiyo, hivyo kuingia mkataba bandia uliosababisha kuwapo kwa mgogoro mkubwa na mmiliki halisi wa eneo hilo.

  Kitendo cha kampuni hiyo kuingia katika ardhi hiyo na kuanza kufanya kazi kilisababisha wakazi wa eneo hilo kufanya vurugu zilizoambatana na kupiga mawe mitambo na magari ya Wachina hao.

  Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, Kenneth Mwang’amba, anayedai kulimiliki eneo la kiwanja hicho chenye hati miliki yenye namba 2459, alisema kitendo walichofanya Wachina hao kufanya shughuli za uchimbaji katika eneo lake ni ukiukwaji wa sheria.

  “Hili eneo mimi nalimiliki kihalali, licha ya kuwapo kwa mgogoro na skauti ambao awali walinyang’anywa eneo hili baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya vigezo na kukabidhiwa kwangu,” alisema Mwang’amba.

  Alisema eneo hilo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yake na Skauti Mkoa wa Mbeya waliovamia eneo hilo bila kufuata taratibu, huku mamlaka zinazohusika zikishindwa kutoa ufafanuzi kuhusu nani ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.

  Alisema baada ya kukosa maelewano, Halmashauri ya Jiji iliamua eneo hilo lichukuliwe na Skauti ambapo pia walitakiwa kulipa fidia kwake baada ya makubaliano kutokana na uharibifu uliokuwa umetokea.

  Alisema kutokana na Skauti kushindwa kulipa fidia, hawakuwa na uhalali wowote wa kuendesha shughuli ya aina yoyote katika eneo hilo kutokana na kushindwa kulipa fedha walizokuwa wakidaiwa.

  “Kisheria hawa watu wa Skauti hawakutakiwa kufanya shughuli zozote katika kiwanja hiki, kwa sababu mimi ndiye mmiliki halali wa eneo hili hadi hapo watakapokuwa wametimiza masharti ya kunilipa fidia kwa sababu awali kulikuwa na tofali ambazo ziliharibika kutokana na mgogoro,” alisema Mwang’amba.

  Kwa upande wake, Msemaji wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Uswege Mwaitebele, alisema waliwaruhusu Wachina kuchimba eneo hilo kwa makubaliano ya kuwajengea kituo cha kufundishia skauti, hivyo hawakuona sababu za kusubiri.

  Kuhusu mgogoro uliopo kati ya Skauti na Mwang’amba, alikiri kuwapo kwa mgogoro huo na alisema eneo hilo linamilikiwa kihalali, ingawa walishindwa kulipia fidia kama walivyokubaliana.

  Alikiri kutofuata taratibu za kuruhusu uchimbaji wa vifusi pasipokuwa na kibali kutoka katika halmashauri husika, ambapo yeye alifanya hivyo bila kuwahusisha viongozi wenzake kwa madai yeye ni kiongozi wa Skauti wa Kanda, hivyo haina ofisi na yeye amekuwa akijitolea kuhifadhi nyaraka katika ofisi yake.

  Naye, Ofisa Ardhi wa Jiji la Mbeya, Ephraimu Mkumbo, alikiri kuwapo kwa mgogoro wa eneo hilo huku akiwatupia lawama Skauti kwa kufanya shughuli zao kinyume na taratibu.

  Alisema Skauti waliamuliwa kulipa fidia za eneo hilo kwa mhusika kama watahitaji kulimiliki kihalali.

  “Ukweli ni kwamba hadi sasa mmiliki halali wa eneo hili ni Keneth Mwang’amba, hivyo Wachina hao wanapaswa kuondoka na kusitisha shughuli zao,” alisema Mkumbo.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  kumbe wanajengea barabara ya huko kwenu . sasa tatizo liko wapi . nilidhani wanaiba au wanachimba madini . kakojoe ukalale
   
Loading...