Malata Junior
JF-Expert Member
- Nov 29, 2011
- 3,104
- 2,550
Serikali ya CCM imekuwa ikijivunia sana misaada kutoka serikali ya China na makampuni ya kichina mpaka kufikia kubeza na kudharau misaada kutoka Marekani na nchi za Ulaya hasa baada ya kunyimwa pesa za MCC.
Lakini kwa muda mrefu tumeona makampuni ya kichina na raia wa China wakifanya vitendo vinavyokiuka sheria za Tanzania na kuisababishia hasara kubwa huku mamlaka husika zikisita kuwachukulua hatua. Baadhi vitendo hivyo ni;
1.Ujenzi wa miradi chini ya kiwango hasa barabara
2.Uingizaji wa bidhaa feki zisizo na ubora.
3.Ujangili,biashara ya pembe na meno ya tembo pamoja na utoroshaji wa wanyama hai.
4..Biashara ya nyama ya punda ambao ni wanyama kazi kunakosababisha hatari ya wanyama hao kutoweka.
5.Uendeshaji wa viwanda vidogo visivyozingatia usalama,mazingira na haki za wafanyakazi.
6..Uchimbaji madini usiozingatia ulinzi wa mazingira kama tulivyoona huko Chunya.
7.Usafirishaji wa noti na sarafu za Tanzania kwenda china bila idhini ya benki kuu ya Tanzania.
8.Kufanya biashara ya umachinga na kazi nyingine zinazoweza kufanya na watanzania kinyume na kibali cha kuishi nchini.
9.Unyanyasaji wa raia wa Tanzania ikiwemo kutembeza kichapo.
10. Biashara ya uchangudoa ya wanawake wa kichina kwenye macasino.
Sasa hivi wachina wanachochea ugomvi kati ya watanzania na mataifa mengine wafadhili ili wabaki wenyewe na hapo ndipo wataamua kufanya lolote wanalotaka kwa sababu hatutakuwa na rafiki mwingine wa kumkimbilia.
Natoa rai kwa serikali ya CCM na mashabiki wao wafuata mkumbo waache kubeza misaada kutoka nchi nyingine kwa kuwategemea wachina hao kwa vitendo vyao wataiangamiza nchi hii.