Wachina wa kampuni ya Chico watuhumiwa kumtesa mlinzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina wa kampuni ya Chico watuhumiwa kumtesa mlinzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by macho_mdiliko, Jun 15, 2009.

 1. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  WACHINA kutoka Kampuni ya Chico Construction Limited wanadaiwa kumfanyia unyama wa kutisha mlinzi wao wa ,Kundwa Asakay (42) kwa kumpiga shoti ya umeme sehemu zake za siri,mateke,fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za wizi.

  Wachina hao wapatao saba wanadaiwa kufanya unyama huo juzi usiku ambapo walimtuhumu Asakay kuiba ‘nondo’ mbili kwenye lindo lake ambapo baada ya kubaini kuibwa kwa vifaa hivyo walichukua sheria mkononi kwa kumuadhibu vikali mlinzi huyo.

  Pamoja na kumwandhibu mlinzi huyo, wanadaiwa walimfungia kwenye kontena bila ya kumpa chakula, maji na wala kumruhusu kwenda haja baada ya kumfunga kamba hadi jana walipombadilishia adhabu kwa kumning’iniza mithili ya Yesu.

  Akizungumza baada ya kuokolewa na polisi waliofika kwenda kambi hiyo ya wachina ambao ni wajenzi wa barabara iliyopo eneo la Mruki wilayani Babati huku akionyesha majeraha makubwa akiwa ndani ya gari la polisi, Asakay alisema anahisi maumivu makali.

  Hata hivyo polisi waliofika kwenye kambi hiyo ya Mruki wakiwa na gari lao wanadaiwa walizuiwa kutoka nje ya uzio na wachina.


  “Sisi tumefika hapa asubuhi na tumemkuta huyu mmasai ananing’inia huku amefungwa kamba kwenye nguzo za taa ya umeme, tulimnasua na kutaka kutoka naye ili kumpeleka hospitali, lakini wachina walituzuia kutoka,”alisema mmoja wa polisi ambaye jina linahifadhiwa.

  Licha ya kuzuia gari la polisi kutoka nje ya uzio, wachina hao wanadaiwa kuwapiga picha askari huku wakipiga simu eneo la Magugu kwenye kambi yao kubwa kuomba gari la kubeba mizigo ili kulibeba gari la polisi.

  Akizungumzia zaidi kitendo hicho cha kutundikwa kama yesu mlinzi huyo alisema,wakati wa usiku akiwa amelala mlinzi mwenzake aliyemtaja kwa jina la Michael alifika kwenye eneo lake yeye akiwa amepitiwa na usingizi ambapo alimuibia nondo.

  Alisema ghafla alishtuka usingizini na akaona wachina wakipiga kelele na kumfukuza Michael, lakini aliwazidi nguvu hawakumkamata na kumrudia yeye na kuanza kumshambulia kwa kumpatia mateso hayo makali huku akiwa hana mtetezi.

  Jana hiyo kamati ya ulinzi na usalama ilikaaa kujadili tukio hilo chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa wilaya ya Babati Dk Ian Langiboli ambapo mazungumzo yalichukua zaidi ya dk 45.

  Akizungumza mara baada ya kutoka kwenye kikao na wawakilishi hao wa kampuni hiyo ya kichina inayojenga barabara Minjingu-Singida,Dk.Langiboli alisema amewasihi wachina hao kutojichukulia sheria mkononi na amewataka kujenga mahusiano mazuri na watanzania.

  Kuhusu hatua ambazo zitachukuliwa dhidi ya tatizo hilo Mkuu huyo wa wilaya alisema ni jukumu la muathirika kutoa taarifa na kufungua kesi polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa maelezo kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

  Hilo ni tukio la pili , wachina kushambulia watu hususan wafanyakazi wao kwa tuhuma za kuiba vifaa tangu walipoingia wilaya ya Babati mkoani Manyara kufanya shughuli ya ujenzi.

  From Mwananchi news paper
  Mwananchi Read News
   
 2. Kamjingijingi

  Kamjingijingi JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Huyo Mkuu wa wilaya anamatatizo gani ? Haelewi kwamba kuna jinai imetendeka hapo ? Au ndio mambo ya kitu kidogo. Yuko tayari kuona sheria inachezewa na yeye anaishia kuita mikutano ya kujadili ! Dr. Slaa upo wapi ?
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Hebu fikiria ndio angekuwa ni Mtanzania yupo China na kafanya vile.... ohoo My God sitaki kufikiri. Mkuu Dr Slaa atashuhulukia mangapi? Na Viongozi wetu wako kwa ajili ya nini? Tatizo ni sisi wananchi hatutaki kuwawajibisha!!!!
   
 4. R

  Rikab Mikail Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao WaChina wawajibishwe.
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sheria ichukue mkondo wake.
   
Loading...