Wachina kujenga daraja la Kigamboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachina kujenga daraja la Kigamboni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIROJO, Jan 10, 2012.

 1. K

  KIROJO Senior Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMPUNI ya China Railway Constraction Engeering Group kwa kushirikiana na Kampuni ya China Bridge imeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni ambapo ujenzi huo utachukua miaka mitatu kukamilika.
  Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo ulisainiwa jana na mwakilishi wa kampuni ya hiyo, Shi Yiqian, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jami (NSSF), Dk. Ramadhan Dau.
  Akizungumzia ujenzi huo, Dau alisema kuwa ndoto imetimia ambapo kazi iliyobaki ni utekelezaji kwa kampuni hiyo kuanza kujenga.
  Alisema kuwa shirika limehangaika sana katika kufanya kazi kutafuta mkandarasi mshauri wa mradi huo ambapo limechukua kipindi kirefu hadi kufikia kumpata.
  Dau alisema katika ujenzi huo NSSF inatoa asilimia 60 ya mradi mzima na serikali itatoa asilimia 40 ambapo mradi mzima utagharimu sh 214, 630,40,000. Naye, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alimtaka mkandarasi kufanya kazi kwa nguvu ili ujenzi wa daraja hilo uwe umekamilika ndani ya miezi 36.

  Dk. Magufuli alisema katika ujenzi huo hakuhitajiki siasa kutokana na Watanzania kuchoshwa na mambo hayo badala yake watu wanataka daraja kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo.
  Alisema kuwa kuendekeza siasa kutawafikisha pabaya Watanzania na kukosekana kwa maendeleo na kuacha kutumia fursa zilizopo.
  “Watu wamechoka na siasa zisizo za vitendo na badala yake watu wafanye kazi kwa masilahi ya taifa ili kuweza kufanikiwa kwa miradi ambayo serikali imedhamiria kuifanya,” alisema Dk. Magufuli. Aliwataka Watanzania kujitokeza kuomba kazi pindi ujenzi huo utakapoanza bila kujali itikadi zao za vyama lengo ni kuweza kujikwamua na umaskini.
  source Tanzania daima
  Hapo kwenye bolded ndo majibu ya magufuli kwa wabunge wa dar kama hajuwi
   
 2. survivor03

  survivor03 JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 225
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mambo vipi wakubwa mimi ni new comer just joined . Je kutokana na daraja la kigamboni ina maana ile project kuhusu ule mji mpya kujengwa bado itakuwepo?
   
 3. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Ngoma ikilia sana mwisho wake ni kupasuka", nadhani sasa Magufuli bado kidogo atabaki uchi kwa jamii. Pamoja na kuwajibu wabunge wa Dsm kuwa waache mambo ya siasa katika kutekeleza shughuli za maendeleo, hebu tumwulize Mgaufuli anayeendekeza siasa badala ya kutuletea maendeleo ni nani kama si yeye na serikali yake. Wakati wanaomba kura mwaka juzi kuanzia Jk na wabunge wote wa ccm walitoa ahadi lukuki ambazo zinatakiwa zitekelezwe ndani ya miaka mitatu iliyosalia.

  Mpaka sasa na wamebakiza miaka mitatu tu lakini hakuna lolote ambalo limeshafanyika katika kutekeleza ahadi zao. Sana sana tunashuhudia mitandao kibao ndani ya ccm ya kutafuta urais wa 2015. Ndo maana nasema Magufuli atuambie anayeendekeza siasa badala ya utendaji ni nani kama si serikali ya ccm.

  Pili serikali ya ccm ilwahi kuwaambia watz kuwa ndege ya rais nilazi,a inunuliwe hata kama tutakula nyasi, na hawakutuomba samahani kwa kejeli hiyo, juzi Magufuli tena anawaambia watz kuwa asiyeweza kulipa nauli ya 200/- ya Kigamboni "apigembizi" mpaka ng'ambo nyingine, hii nayo nikejeli nyingine kwa watz na ni ulevi wa kupindukia wa madaraka........wananchi ndo wanaowaweka hawa waheshimiwa madarakani, halafu wanageuka wanakejeli haohao waajiri wao.........watz tutafakari kwa kuchukua hatua hasa 2015
   
 4. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  kulijenga hilo daraja wa2 watapiga pesa za kuchakachua kama hawana akili vizuri.
   
Loading...