Wachina hawa wafukuzwe mara moja nchini

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,020
Mwigulu anasa Wachina 72 wakiishi kinyemela nchini

Mwigulu Nchemba

Na ALEX SAYI, GEITA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza katika Mgodi wa Dhahabu wa Nyamahuna mkoani Geita na kukuta Wachina 72 kati ya 100 wakiishi na kufanya kazi bila vibali.

Akizungumza katika mgodi huo unaomilikiwa na Mtanzania, Andrew Obole, Mwigulu alisema alifika hapo kutokana na kuona taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya jamii.

Mwigulu alisema taarifa hizo zilimuonyesha Masanja Shokera akicharazwa bakora na raia wa mmoja wa China, Lee Swii, kwa madai ya kuiba mawe ya dhahabu Julai 6, mwaka huu.

“Nimefika kuthibitisha nilichokisikia kwamba kuna raia wa kigeni wanachapa watu hapa. Nimemuona mtuhumiwa wa udhalilishaji na kushangazwa na kukuta wafanyakazi wa China hapa wapatao 100 kwenye mgodi huo,” alisema.

Alisema taarifa alizonazo ambazo zipo uhamiaji zinaonyesha kuwa raia wa China waliopo mgodini hapo ni 28 ambao wana vibali halali vya kuishi nchini.

Waziri alisema kwa sababu hiyo, aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita kuwaweka chini ya ulinzi Wachina wengine 72, walinzi saba na Kaimu Meneja Uzalishaji, Richard Joachim.

“Wakati hawa wakiwa chini ya ulinzi naiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita kuchunguza uhalali wa raia hao wa China kuishi nchini bila ya kuwa na vibali.

Vilevile huyo anayeitwa Lee ambaye anatuhumiwa kumdhalilisha Mtanzania mwenzetu awekwe chini ya ulinzi na walinzi saba na kumpiga na kumjeruhi,”alisema.

Masanja Shokera ambaye anayedaiwa kudhalilishwa, , alisema siku hiyo alivamiwa na walinzi wa mgodi huo akituhumiwa kuiba mawe ya dhahabu.

Alisema walimpiga na kumfunga mikono na miguu na kuendelea kumwadhibu hali iliyosababisha apoteze fahamu.

“Walionipiga wote nawatambua, ni hawa walinzi wa Kimasai wote walinishambulia na huyu Mchina alikuja pia kunipiga wakati nimefungwa kamba… alianza huyu mkuu wa ulinzi, Sitta Dotto kuwaamrisha nikaguliwa kunipiga kichwani,” alisema.

Mkurugenzi wa mgodi huo, Andrew Obole alisema anachotambua Wachina waliopo kwake ni 28 na kwamba hao wengine alikuwa hawatambui.

CHANZO: Mtanzania
 
Naam huyu naye akamatwe mara moja kwa kukiuka sheria za ajira za nchi. Alikosa Watanzania wa kuwaajiri hadi aajiri Wachina!? Jibu wote tunalijua.

Mmiliki wa mgodi ashtakiwa kwa kuajiri wageni pasipo vibali.
 
Watafukuzwaje wakati wao ndio wafadhili na marafiki wa kweli ukiwaacha wanya rwanda?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naam huyu naye akamatwe mara moja kwa kukiuka sheria za ajira za nchi. Alikosa Watanzania wa kuwaajiri hadi aajiri Wachina wenzie!? Jibu wote tunalijua.
Labda isiwe tanzania
 
Si ndiyo sababu ile nguvu ya soda ya msako wa wahamiaji haramu katika awamu hii ya mihemuko na ukurupukaji ikaisha kimya kimya. Na hili nalo litapotea kimya kimya na hawa wataendelea kuishi nchini.

Watafukuzwaje wakati wao ndio wafadhili na marafiki wa kweli ukiwaacha wanya rwanda?
 
Wahamiaji haramu wako wengi sana serikali inapaswa kufanya operesheni kubwa kuwaondoa wahamiaji haramu
 
Si ndiyo sababu ile nguvu ya soda ya msako wa wahamiaji haramu katika awamu hii ya mihemuko na ukurupukaji ikaisha kimya kimya. Na hili nalo litapotea kimya kimya na hawa wataendelea kuishi nchini.
Nakubaliana nawe mkuu na utasikia siku siyo nyingi balozi wa china anaenda kufanya ziara mkoani geita na kuahidi msaada wa gari la kubebea wagonjwa basi tena hapo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Halafu huyu dikteta anazuga Watanzania kwamba atailinda mipaka ya nchi.

Nakubaliana nawe mkuu na utasikia siku siyo nyingi balozi wa china anaenda kufanya ziara mkoani geita na kuahidi msaada wa gari la kubebea wagonjwa basi tena hapo
 
Sipati picha mtanzania afanye unyama nchini china kama huu aliofanya mchina kwa huyo kijana wetu naamini sasa hivi angeshapigwa risasi kabisa
 
Mkurugenzi na yeye anashangaa hao wachina 72 wanaofanya kazi bila kibali
 
Back
Top Bottom