Wachimbaji wawili wafariki dunia kwa kuporomokewa na udongo Singida

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
mgodi(3).jpg



Wachimbaji wawili wa madini wamefariki dunia baada yakuporomokewa na udongo wakati wakiwa kazini kuchimba madini mkoani Singida.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,ACP Simion Haule,amewataja wachimba madini hao kuwa ni Mwidosi Ramadhani(44) na Michael George (30) wote wakulima na wakazi wa kijiji cha kijiji cha Mgongo, tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.

Ameisema wachimbaji madini hao walifariki dunia Juni 19 mwaka huu saa nne asubuhi wakati wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Iramba, ili waweze kupatiwa matibabu.

Haule amesema siku ya tukio,wachimbaji hao waliingia eneo la madini linalomilikiwa na kampuni ya Barick ambayo imelimiliki eneo hiyo kwa ajili ya utafiti mwaka 2006.

Kutokana na eneo hilo kutokuendelezwa kwa muda mrefu na kampuni ya Barick,wakazi wanaolizunguka eneo hilo wamekuwa na utamaduni wa kulivamia kwa ajili ya kuchimba madini,ili kujitafutia riziki.

Kaimu Kamanda huyo,ametoa onyo kali,kwamba wananchi waache mara moja tabia ya kuchimba madini bila ya kuwa na kibali halali cha wizara ya madini na nishati,vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom