Wachimbaji wadogo waiangukia serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachimbaji wadogo waiangukia serikali

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kamachumu Town, Jul 13, 2012.

 1. K

  Kamachumu Town Guest

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Joseph Zablon

  SERIKALI imetakiwa kuyafanyiakazi mapendekezo yaliyotolewa na wachimbaji wadogo wa madini kupitia Chama cha Wachimba Madini Wanawake (TAWOMA), wakati wa mkutano baina ya wadau hao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo yaliyofanyika Dodoma hivi karibuni.

  Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na mwenyekiti wa Tawoma Eunice Negele ilisema anaamini kuwa walichokubaliana kitafanyiwakazi kutokana na ukweli kuwa wachimbbaji wadogo miaka mingi sasa wamekuwa wakigeuzwa daraja na wachimbaji wakubwa.

  Alisema wachimbaji wadogo katika maeneo ambako ndipo wanapopatia ridhika zao wamekuwa wakifukuzwa na kisha kupewa wawekezaji ambao wana mitaji mikubwa hivyo kuwafanya wabakie wakihangaika bila kuwa na uhakika wa kile ambacho wanakifanya.

  Imesema sehemu ya taarifa hiyo kuwa kitendo cha waziri kutaka kuonana nao kujadili changamoto zinazowakabili kimeonysha jinsi gani anavyotaka kushughulika na matatizo yao tofauti na ilivyokuwa kwa watangulizi wake lakini hata hivyo ana wasi wasi na mwenendo usioridhisha wa serikali katika kushughulikia changamoto tofauti za wananchi wake.

  "Tulipozungumza nao alikiri kutambua changamoto ambazo zinawakabili wa chimbaji wadogo ambao mazingira ya biashara yaliyopo hayawapa nafasi ya kujinasua kutoka katika umaskini" inasema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa waziri aliwataka wajadili njia muafaka za ufanyaji wa biashara zao kisha wampatie mependekezo.

  Taarifa hiyo ilizitaja changamoto ambazo zinawakabili wachimbaji wadogo kuwa ni pamoja na umiliki wa maeneo kwa ajili ya shughuli zao, elimu, mitaji kwa ajili ya kununua vifaa vya kisasa vya uchimbaji na masoko.

  Changamoto nyingine imetajwa kuwa ni mapigano baina yao na wamiliki wa migodi mikubwa na ilisema taarifa hiyo kuwa yote hayo yanawezekana kuwekwa sawa iwapo milango ya majadiliano itafunguliwa jambo ambalo alisema kupitia taarifa hiyo kuwa linawezekana.
   
Loading...