Wachimbaji Mererani waliamsha dude

Wachimbaji Mererani waliamsha dude

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Wamiliki wa migodi 10 ya madini ya Tanzanite iliyopo Mererani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara iliyofungiwa kufanyakazi baada ya kubainika kutobokeza kwenye mgodi wa kitalu C kinyume cha sheria na kanuni za madini wamedai wameliamsha kwa kudai kufungiwa kwao kunaupendeleo.



Migodi iliyofungiwa ni ile iliyopo mkabala na mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na Kampuni ya Tanzanite One baada ya kugundulika kuwa wamiliki wa migodi hiyo wameingia mgodi wa Tanzanaite One kwa zaidi ya mita 600 wakichimba madini kinyume cha sheria na kanuni .



Mmoja wa wamiliki wa migodi hiyo ambae aliomba kuhifadhiwa jina lake alisema kuwa hatua ya kufungia migodi hiyo ilichukuliwa na Afisa Madini Mfawidhi wa Kanda ya Mererani Daud Ntalima mapema mwanzoni mwa mwezi huu ina kila dalili za upendeleo na sitofahamu.



Alisema kuwa kuna baadhi ya migodi haijafungiwa na makosa yanafanana na bado wamiliki wa migodi hiyo wanachimba ndani ya mgodi wa Tanzanite One kimakosa lakini viongozi wa Wizara ya Madini Kanda ya kaskazini wako kimya.



‘’Mimi binafsi siwezi kuvumilia hili ntahitaji majibu kwa afisa wa Madini Mererani Ntalima vinginevyo ntalalamika ngazi za juu ‘’



Mmiliki mwingine ambaye anachimba kitalu C yeye alikiri kutoboza Kitalu C na kusema kuwa hilo liko sana katika migodi na kamati za usuluhishi kufanya kazi yake ya kumrudisha nyuma mtoboaji lakini katika suala la kitalu C liko tofauti.



Alisema Migodi iliyofungiwa inafanana na ile ambayo haijafungiwa na Afisa Madini Mfawidhi Daud Ntalima na kutokana na hilo kuna kila dalili za Rushwa katika ofisi hiyo.



Gazeti hili lilimtafuta Ntalima kuzungumzia hilo hakukanusha wala kuthibitisha juu uamuzi wa kufungia migodi hiyo bali hakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia uamuzi wake na kuomba kupigiwa baada ya dakika kumi ili aweze kutoa sababu zaidi za kufungiw akwa migodi hiyo.



‘’Hilo suala nipe kama dakika kumi ntakupigia au unipigie kwa sasa niko kwenye gari na watu na ntakupigia mwenyewe nikupe taarifa ‘’alisema Ntalima



Hata hivyo Afisa Madini huyo hakupiga ndani ya muda huo na alipopigiwa simu yake ya kiganjani hakupokea tena simu yake ya kiganjani hadi tunakwenda mtamboni.



Kwa mujibu wa nakala za barua ambayo gazeti hili imeiona,Ntalima alidai kuwa kufungiwa kwa migodi hiyo ni kufanya kosa la kutoboza kwa zaidi ya mita 600 ndani ya kitalu C kinachomilikiwa na Tanzanite One kimakosa.





Mwanzoni nwa mwaka huu aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Madini ambaye kwa sasa ni Waziri ,Dotto Biteko aliwahi kumwagiza Afisa Madini Mkadhi wa Kanda ya Mererani Daudi Ntalima kuhakikisha anaufungua mgodi wa Gem and Rock Venture na kuanza kufanya kazi mara moja lakini kwa kufuata masharti ya leseni,kanuni,mipaka na sheria za uchimbaji na sio vinginevyo.





Biteko alinukuliwa kuchukuwa uamuzi huo baada ya kupokea taarifa za pande zote mbili juu ya mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kampuni ya Gem and Rock Venture iliyopo kitalu B kutoboa mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na Kampuni ya Tanzanite One.





Waziri alimtaka Ntalima kabla ya kuwaruhusu Gem And Rock Venture kuhakikisha anakaguwa mgodi huo kwanza ili ajiridhishe ikiwa ni pamoja na kuangalia usalama wa mgodi,wamiliki wa mgodi wanafuata sheria ya leseni yao ya uchimbaji,kanuni na mipaka ya mgodi na wakifuata masharti hayo wanapaswa kuruhusiwa kuanza kazi.





Biteko katika ziara hiyo Mererani alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya madini, Professa Simon Msanjila na katibu huyo alisema kuwa ofisi yake itahakikisha inaangalia mipaka ya mgodi wa kitalu C na Mpaka wa kitalu B kama yote iko kisheria na nani anastahili kuifuata lengo ni kutaka kuepuka migogoro isiyokuwa na tija kwa wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo wadogo.



Alisema serikali iliyo chini ya Rais Dkt John Magufuli haiko katika kumnyanyasa mtu yoyote bali iko katika kuhakikisha kila mchimbaji kote nchini anapaswa kufuata sheria ya lesseni aliyopewa ,mipaka na kanuni na ikikiukwa serikali haitakuacha salama.








IMG-20190719-WA0002.jpeg
 
Wanatafuta huruma ya baba hao.

Mwenzako kaweka mpaka kikazi uishie hapa, wewe unavuka unaambiwa unasema hapana huku ni eneo huru au mpaka mwisho pale haya, unapogonga nyundo huku tunasikia tukikwambia, unaleta timbwili, nini unataka wewe?
 
Back
Top Bottom