Wachimba mchanga wamkamata mtuhumiwa wa mapango ya Amboni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,388
Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini,Paul Chagonja,ametoa taarifa kuwa mtuhumiwa mmoja anaehusishwa na wale waliokuwa katika mapango ya Amboni amekamatwa na wachimba mchanga wa Mleni wanaofanya shughuli zao karibu na mapango hayo ya Amboni.

Mkuu huyo ameongeza kuwa, silaha moja iliyoibwa katika kituo kimoja cha polisi nayo imepatikana baada ya kumuhoji mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo,bwana Chagonja amesema hawezi kutaja jina la mtuhumiwa huyo kwa sasa.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Wanaokamtwa na wachimba mchanga ndio wakusumbua Jeshi la Wananchi?!
====================

Mmoja kati ya watuhumiwa wa uhalifu amekamata na vijana wanaochimba mchanga pembeni ya mapango.

Baadhi ya vijana wanaojihusisha na uchibmaji mchanga pembeni mwa mapango ya mleni maji moto yanayodaiwa kuhifadhi makundi ya uhalifu, wamefanikiwa kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa wa uhalifu kisha kumkabidhi kwa vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Kamishna wa operesheni wa jeshi la polisi nchini afande Paul Chagonja amesema baada ya kukamatwa kwa mmoja wa watuhumiwa jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha aina ya Shot gun pamoja na risasi 20 zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya shimo katika mapango.

Hata hivyo jeshi la polisi limewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwao kwa sababu jitihada za kukanbiliana na uhalifu zinaaanzia kwa wananchi hivyo ni vyema wakaitikia wito ili hali ya usalama iweze kuimarika.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanaoishi eneo la mleni maji moto wameliomba jeshi la polisi kuimarisha hali ya usalama kwao baada ya kumkamata mmoja wa wahalifu na kumkabidhi kwa vyombo vya dola kisha kuishauri serikali kuchukua eneo lililoingiliwa na makundi hayo yanayoitwa na jeshi la polisi kuwa ni majambazi kisha kuwamegea wananchi wanaohangaika maeneo ya kilimo ili waweze kulima mazao ya chakula badala ya kufuga vichaka ambavyo vimesababisha kuwa pango la uhalifu.
 
Hahahahahaha hawa jamaa hata hawaoni aibu na kuamua kupotezea mambo mengine.? Issue ishabuma wakaushe kimtindo tuu mambo yasonge.

Ile thread ya Lema sijui wameiweka wapi Mods, Kwamba jamaa bado haamini kama Rais keshachagua IGP.
 
drsma xinaendelea. hivi wale maadkari waliojeruhiwa wanafahamika kwa majina?ni hatari huu usanii kwa nchi yetu. ile video ya magaidi jamaa anataja eti ealiteka ushirombo. mbona wale wa udhirombo walikamatwa geita? chagonja anapashwa ajipange kea hizi tastifa. afande kashsi rpc yuko wapi? kwanini naibu rpc ndie alitoa tamkovjana. yeye alikuea wap kama mkuu wa operation?
 
.... as bogus an episode as that of Mulundi, a purportedly Kenyan, the same comedian police implicated to have kidnapped Dr. Ulimboka
 
Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini,Paul Chagonja,ametoa taarifa kuwa mtuhumiwa mmoja anaehusishwa na wale waliokuwa katika mapango ya Amboni amekamatwa na wachimba mchanga wa Mleni wanaofanya shughuli zao karibu na mapango hayo ya Amboni.

Mkuu huyo ameongeza kuwa, silaha moja iliyoibwa katika kituo kimoja cha polisi nayo imepatikana baada ya kumuhoji mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo,bwana Chagonja amesema hawezi kutaja jina la mtuhumiwa huyo kwa sasa.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Wanaokamtwa na wachimba mchanga ndio wakusumbua Jeshi la Wananchi?!
Kasema bunduki hiyo ni Kati ya zile Mbili walizoporwa Polisi Tanga
Jina la mtuhumiwa haliwezi kutajwa kwa sababu za kiusalama kwani uchunguzi unaendelea
 
Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini,Paul Chagonja,ametoa taarifa kuwa mtuhumiwa mmoja anaehusishwa na wale waliokuwa katika mapango ya Amboni amekamatwa na wachimba mchanga wa Mleni wanaofanya shughuli zao karibu na mapango hayo ya Amboni.

Mkuu huyo ameongeza kuwa, silaha moja iliyoibwa katika kituo kimoja cha polisi nayo imepatikana baada ya kumuhoji mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo,bwana Chagonja amesema hawezi kutaja jina la mtuhumiwa huyo kwa sasa.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Wanaokamtwa na wachimba mchanga ndio wakusumbua Jeshi la Wananchi?!

Muvi linaendelea, chagonja na fiksi zake za mchana kweupe
 
Hahahahahaha hawa jamaa hata hawaoni aibu na kuamua kupotezea mambo mengine.? Issue ishabuma wakaushe kimtindo tuu mambo yasonge.

Ilethread ya Lema sijui wameiweka wapi Mods, Kwamba jamaa bado haamini kama Rais keshachagua IGP.
Hizi zitakuwa hujuma za Chagonjwa tuu usanii mtupu
 
yaani natamani siku moja mpate misukosuko kama tajiri wa kisesa r.i.p aliyeuwawa kwa kupigwa risasi ya tumbo wakitafta vocha alizotoka kununua mwanza.

ipo siku mtajua maana ya ulinzi. modes futeni post niliyoanzisha kuhusu issue hii
 
drama zinaendelea. hivi wale maaskari waliojeruhiwa wanafahamika kwa majina?ni hatari huu usanii kwa nchi yetu kuuacha uendelee. ile video ya magaidi jamaa anataja eti alieteka ushirombo. mbona wale wa udhirombo walikamatwa geita? chagonja anapashwa ajipange kwa hizi taarifa. afande kashai rpc yuko wapi? kwanini naibu rpc ndie alitoa tamko jana?yeye alikua wap kama mkuu wa operation hadi msaidizi wa rpc atoe taarifa?
 
Back
Top Bottom