Wachezaji tunalogana wenye kwa wenyewe-peter mhina

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,139
KOCHA Msaidizi wa timu ya Majimaji ya Songea, Peter Mhina alinukuliwa mwishoni mwa msimu uliopita wa Ligi Kuu akisema kwamba kupuuzwa kwa tamaduni za zamani na u-CCM ndani ya klabu hiyo ndiyo sababu ya timu kufungwa mechi nyingi katika uwanja wake wa nyumbani.

Kuthibitisha kauli yake, alisema kuna mambo yaliyokuwa yakifanyika zamani, kwa wazee kuchinja mbuzi kabla ya mechi lakini kizazi hiki kimeona suala hilo si muhimu. Akasema kwa miaka hii, wale wazee waliokuwa wakipelekewa posho kwa ajili ya kazi hiyo wanachukia, hivyo wanaamua kukomoa!

Haya ni maneno ya mwalimu wa kandanda wa timu maarufu ya Majimaji yenye makazi yake mjini Songea, mkoa wa Ruvuma. Kama mwalimu anaamini ushirikina, wachezaji watakuwaje? Kuchinja mbuzi kabla ya mchezo kunasaidiaje ushindi wa timu?

Eti kwa kuwa siku hizi utamaduni wa kuchinja mbuzi umeachwa, basi wazee (waganga) waliokuwa wakipatiwa posho (fedha) kwa kufanya kazi hiyo, wanachukia, hivyo wanakomoa.

Kukomoa kunakosemwa ni waganga hao kufanya ushirikina ili timu isifanye vizuri na mwishowe wakumbukwe kwa kupewa kazi ya kuirogea timu ili ipate ushindi!

Biblia Takatifu inasema: “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema. Bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu,” (Yer. 17:5-6).

Ushirikina ni imani potofu si kwa klabu ya Majimaji tu bali kwa timu zote za michezo humu nchini. Mambo ya ushirikina yalianzia kwa Yanga na Simba tangu miaka ya mwisho ya 1950 na inaendelea mpaka sasa.

Nakumbuka kisa kimoja cha kipa wa timu iliyovuma sana miaka ya mwanzoni ya 1960, TPC ya Arusha Chini, Moshi, aliyeitwa Benedicto (Ben) Okoth. Huyu alikuwa anadaka mithili ya nyani na washambuliaji wa timu pinzani walipata shida sana kumfunga.

Wakati ule TPC ilipokuja jijini Dar es Salaam, mara nyingi ilicheza na wachezaji mchanganyiko wa timu za Dar es Salaam na kila mara ilishinda na watazamaji walipenda mchezo wao.

Katika moja ya mechi iliyomfanya Ben Okoth akatae kucheza mpira na kuamua kurudi kwao Kenya, ni ile iliyozikutanisha timu ya mkoa wa Kilimanjaro na Dar es Salaam kwenye Kombe la Taifa iliyochezwa Uwanja wa Ilala (sasa Karume).

Kwa kauli yake, Ben Okoth alisema kila alipopigiwa mpira, aliona mipira miwili na alipodaka, alidaka mpira hewa na ule halisi kuingia kimiani! Akasema hakuwa akiamini uchawi, lakini kwa mechi ile ndio mwisho wake wa kucheza mpira jijini Dar es Salaam na kweli ikawa hivyo.

Yanga na Simba, haziingii uwanjani ‘miguu mitupu’, yaani bila chochote wapewacho na waganga ili kupata ushindi. Kwa wale wanaohudhuria mechi za ‘vigogo’ hao wameona mara kadhaa baadhi ya wanachama wao wakiingia uwanjani na kunyunyiza ungaunga, kurusha njiwa na wachezaji kuingia uwanjani kwa kuruka ukuta.

Wakati mwingine hata baadhi ya viongozi wa vilabu hivyo huingia uwanjani kabla ya timu na kumwaga ‘vitu’ waziwazi huku wakishangiliwa na mashabiki wao! Kuna wakati moja ya timu hizi ilikuwa na mechi uwanja wa Taifa (sasa Uhuru).

Katikati ya uwanja panapoanziwa mpira (sipendi kutumia neno ‘dimba’) palifukiwa mbuzi. Ilikuwa bahati kwamba kituko hicho kiligunduliwa mapema na mbuzi yule akafukuliwa kabla ya mechi.

Ni mambo ya ushirikina, uchawi, juju, mazingaombwe, kachumbari … taja kila jina ulijualo katika ulozi. Wapo watu maalumu waitwao ‘wataalamu’ wa kandanda. Huchukuliwa kutoka mikoa mbalimbali na kufichwa kwenye nyumba za viongozi au wenyeviti wa kamati za ‘ufundi’ wanakofanyia shughuli zao humo.

Kuna wanaoroga kwa kutumia paka, vyura, kuku, njiwa na mayai viza. Pia kuna makafara ya kutupa baharini, njiapanda za barabara kuu, katikati ya masoko na kufukia makaburini kwa muda wanaopanga waganga, bila kupungua wala kuzidi kwani kufanya hivyo ni kuvunja mwiko!

Ni wakati wa waganga kuchuma na pia wanakamati ya ’ufundi’ kwani fedha wanazodai kupeleka kwa waganga hazifikishwi zote! Ndio sababu vilabu hupata shida kuweka wazi matumizi ya fedha zitokanazo na mechi au wapewazo na wadhamini.

Wachezaji wanaoonekana tishio ’hutengenezwa’ ili wasilete madhara, ingawa nao ’hufungwa’ na vilabu vyao ili kuwakinga na ’mabomu’ ya upande mwingine. Hii ndiyo sababu kuna wakati mchezaji mahiri hucheza chini ya kiwango na watu kulaumu kuwa kapewa fedha ili timu ishindwe, ingawa pia wapo wanaopewa fedha kwa ajili hiyo!

Ni kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Hata jezi wavaazo wachezaji hulazwa kwa ”mtaalamu” ili zifanyiwe kazi za kuleta ”ushindi!” Waamuzi nao hawaachwi nyuma kwani nao hurogwa ’kitaalamu’ au kwa ”uchawi wa kizungu” yaani fedha, alimradi timu ishinde!

Ushirikina umeenea kwa vilabu vya madaraja yote nchini. Hata wachezaji wa netiboli na mabondia, nao wameingia kwenye imani za kishirikina. Kama ushirikina unaweza kuziletea timu ushindi, mbona Nigeria inayojulikana kwa ushirikina hushindwa kwenye michezo yake?

Hapa nyumbani mbona timu za Mwanza penye eneo maarufu liitwalo ’Gambush’ kwa uchawi mwingi tu, hazijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Taifa? Tuseme nini kuhusu timu za mikoa ya Rukwa, Kigoma n.k. kunakosifiwa kwa uchawi?

Kwa kuwa tunategemea sana ushirikina, kila tunaposhindwa huwalaumu waamuzi na hali mbaya ya uwanja kana kwamba timu zetu zinapochezea uwanjani, timu pinzani huchezea hewani!

Lazima ieleweke kuwa ’uchawi’ wa kandanda ni mazoezi, kufuata maelekezo ya walimu na kujituma. Wachezaji wajiepushe na anasa kwa kujiona wanajua zaidi ya wengine kwa vile tu wanazichezea timu za Yanga na Simba!alienda zaidi na kusema kamuulize Mohamed Banka kisa cha kuondolewa ..yule bwana ni mzuri wakasajili wachezaji wa namba yake kila anaesajili mtu wake ile namba ya banka ama anaumia ama anaaga mpira umeshinda maskini wa mungu simba wakaamini yule jamaa ndie aliewaondolea wakina Echesa na wengine unafikiri mpira umeshuka hapana bana Banka anatisha ila imani chafu za watu wanaoamini kurogana ndio imemfikidhahapo

marobarnabas@yahoo.com 0784/0715 33 40 96 0756 85 53 14
 
Kwa mwendo huu, Tanzania tutakuwa kichwa cha mwendawazimu maisha.
 
Back
Top Bottom