Wachezaji Mesut Ozil na Paul Pogba, Kulipia Matibabu ya Upasuaji wa Watoto 22 wa Kitanzania

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Katika Mashindano yanayoendelea Euro 2016 michuano, Mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil na Mchezaji wa Ufaransa Paul Pogba wameungana kwajili ya kulipa ankra za matibabu ya watoto wa Afrika.

Kwa kushirikiana na kampeni ya Upendo ya Big Shoe11, Ozil na Pogba wataweza kulipia matibabu ya vijana wenye mahitaji barani Afrika.

Big Shoe ni Mpango ambao ulianza katika kombe la dunia 2006. Kimsingi, hii kampeni ya BigShoe11 nia yake ni kupata wachezaji wa mpira wa kulipwa ambayo Wataweza kulipia gharama za watoto wenye mahitaji.

Mesut Ozil na Paul Pogba wote watalipia ankra kwa ajili ya upasuaji wa Watoto 22 wa Kitanzania. Vile vile watasaidia watoto wengine nchi za kiafrika.
35871AFE00000578-0-image-m-11_1466756985921.jpg

Mesut Ozil
357617DA00000578-0-image-a-12_1466756994209.jpg

Paul Pogba


Nine more international stars will follow.


While the Euros are going on, 11 football players will cover the costs of surgery for 22 children in Tanzania, through the charity BigShoe11.

The first two players to get involved were Germany’s Mesut Ozil and France’s Paul Pogba.

The surgeries are for children with burn injuries and club foot – prevalent issues in developing and newly industrialised countries.

BigShoe began at World Cup 2006, when the Togo national team got together to fund a young Togolese girl’s operation.

Source: Mesut Ozil and Paul Pogba paid for surgery for 22 children in Tanzania
 
Ilikuwa nafasi kwa yule mchezaji wa Genk kujoin forces.
 
TunaShukuru sana, na ni mfano mzuri wa kuigwa...
ila nasiye tujititimue kidogo katika ustawii wa jamii... tumekaa kuombaomba na kuombewa kama TZ kilema!!
 
M/zimungu awazidishie kila jema duniani na akhera amen.
Lakini hii sio sifa kusaidiwa mm naamini tukilipa kodi inavyo stahiki na tukisimamia vyema pesa zinazo kusanywa na tukitumia kwa matumizi stahiki haya mambo ya kuomba misaada yatakuwa historia tu.
Leo unakuta shule haina hata matundu ya choo.
Ukiaangalia gharama ya ujenzi wa matundu hayo ni sawa na mafuta ya vx ya mkurugenzi wa halmashauri ya mwezi mmoja tu.
Sasa kunafaida gani ya kuwa na mkurungenzi na gari vx wakati shule za halmashauri yake hazina matundu ya vyoo?
Lazima tuangalie nini la muhimu ndio tugharamie tena kwa gharama stahiki.
Sio kitu cha tsh 10000 kinanunuliwa tsh20000 eti tu ni serikali ndio mnunuzi.
 
Safi sana Ozil & Pogba. Sio hawa wa kwetu kipato kikiongezeka wanaoa mke wa pili, tatu na kuendelea na kuendekeza michepuko
 
Back
Top Bottom